Mtabibu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto katika Mpango wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi
kipaumbele Bw. Wilfred Mandala akiwaelekeza Wawakilishi kutoka Taasisi
ya Bill and Melinda Gate na The End Fund namna ya kusafisha mguu wa Bw.
Juma ambae ni mwasilika wa ugonjwa wa Matende
Afisa kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
katika Mpango wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi
kipaumbele Hope Rusibamayila akishirikiana na wanafunzi kutoka Shule ya
Msingi ya Kilari iliyo katika Wilaya ya Siha katika Mkoa wa Kilimanjaro
kutoa maelekezo kwa wawakilishi kutoka Taasisi ya Bill and Melinda Gate
na The End Fund namna ya Kibuyu Chirizi kikifanya kazi ya kuosha mikono
kwa sabuni baada yakutoka Chooni.
Wawakilishi kutoka Taasisi ya Bill and Melinda Gate na The End Fund
wakiendelea na ziara yao yakukagua baadhi ya miundombinu waliyoisaidia
katika Shule ya Msingi ya Kilari iliyo katika Wilaya ya Siha katika Mkoa
wa Kilimanjaro.
Wawakilishi kutoka Taasisi ya Bill and Melinda Gate na The End Fund
wakigawa kalamu za kuandikia kwa wanafunzi wanafunzi kutoka Shule ya
Msingi ya Kilari iliyo katika Wilaya ya Siha katika Mkoa wa Kilimanjaro
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Siha Dkt. Endrew Method akiongea na Wanafunzi
pamoja na Wageni kutoka Taasisi ya Bill and Melinda Gate na The End Fund
wakati walipotembelea katika Shule ya Msingi ya Kilari iliyopo katika
Wilaya ya Siha katika Mkoa wa Kilimanjaro
Afisa Elimu Wilaya ya Siha Rose Sandi akifanya utambulisho kwa Wanafunzi
pamoja na Wageni waliofika katika Shule ya Msingi ya Kilari iliyo
katika Wilaya ya Siha katika Mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni kutembelea na
kujionea maendeleo ya mchango waliotoa katika shule hiyo.
Mwanafunzi Kutoka Shule ya Msingi ya Kilari Vaileth Wilfred akimkabidhi
ujumbe Afisa Elimu Wilaya ya Siha Rose Sandi baada ya kumaliza Shairi
lao, kulia kwake ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Siha Dkt. Endrew Method na
wa mwisho ni Afisa Mipango wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi
kipaumbele kutoka Wizara ya Afya Bw. Oscar Kaitaba.
Picha yapamoja ya Watumishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto na Wageni kutoka Taasisi ya Bill and Melinda
Gate na The End Fund baada ya kumaliza shughuli ya kutembelea na kukagua
miundombinu katika Shule ya Msingi Kilari wilaya ya Siha Mkoa wa
Kilimanjaro.
Picha ya Pamoja ya Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Kilari wakionesha
kalamu zao juu kuonesha furaha zao baada ya kupokea kutoka katika
Taasisi ya Bill and Melinda Gate na The End Fund
DMO SIHA ASEMA KUWA UTOAJI WA DAWA ZA MINYOO MASHULENI YAFIKIA 97% KATIKA WILAYA YA SIHA.
Na WAMJW - SIHA KILMANJARO
Mganga
Mkuu wa Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Endrew Method amesema
kuwa Wilaya ya Siha imepiga hatua kubwa katika kukabiliana na changamoto
ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, huku akidai kuwa 97% ya
watoto tayari wameshapata dawa hizo za minyoo.
Ameyasema
hayo alipowapokea wageni kutoka Bill and Melinda Gate na THE END FUND
waliokuja kuangalia utekelezaji wa miradi waliyoifadhili na kufuatilia
namna ya wanufaika wanavyofaidika na miradi hiyo katika Wilaya ya Siha.
“Ukiangalia
utoaji wa Dawa za minyoo mashuleni kwa Wilaya tulifikia 97% jambo
ambalo linasaidia watoto kutopata changamoto za ugonjwa wa minyoo, hata
hivyo kwa wagonjwa wa n je tu matatizo ya minyoo yanafikia hadi nafasi
ya tatu hivyo kuna umuhimu mkubwa wa wa kuufanya uwe mkakati endelevu”
Alisema Dkt. Method
Dkt. Method aliendelea kusema
kuwa Taasisi ya Bill and Melinda Gate na THE END FUND wamekuja kuangalia
ni jinsi gani miradi hiyo imekuwa ikitekelezwa na namna ambavyo
matumizi ya fedha wanazotoa yamekuwa yakiwanufaisha wahusika.
“Wamekuja
kuangalia, ni jinsi gani yale mambo waliyokuwa wakititusaidia
tunatekeleza, na miongoni mwa mambo hayo ni unyweshaji wa watoto dawa
za minyoo kwaajili ya kukabiliana na minyoo mashuleni, usafi wa vyoo na
ujenzi wa vyoo bora katika mashule yetu ambayo tumefanya kwa zaidi ya
miaka Sita, pia wamekuja kuangalia namna ya kukabiliana na ugonjwa wa
trakoma”. Alisema Dkt. Method
Aidha, Dkt. Method
amewashukuru wafadhili hao kutoka Taasisi ya Bill and Melinda Gate na
THE END FUND kwa msaada mkubwa ambao wamekuwa wakitoa katika kuisaidia
Serikali ya Tanzania na jamii kwa ujumla kwaajili ya kupambana na
magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
Kwa upande
wake Afisa Mipango kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele
kutoka Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto Oscar
Kaitaba akieleza namna Taasisi ya THE FUND na Bill and Melinda Gate
ilivyosaidia Wizara amesema kuwa ;-
“THE END FUND
imekuwa ikishirikiana na Wizara ya Afya katika kudhibiti ugonjwa wa
Vikope (Trakoma) na ugonjwa wa Matende na Mabusha kwa kuwafanyia
upasuaji katika Mikoa ya Tanga, Pwani na sehem chache Mkoa wa Dar es
salaam”,Alisema Oscar Kaitaba
Oscar Kaitaba
aliendelea kuwa Kwa ugonjwa wa Trakoma wamesaidia kufanya upasuaji wa
Kope katika Mikoa ya Kilimanjaro katika Wilaya ya SIHA na Arusha katika
maeneo ya watu waliohathirika zaidi na ugonjwa huu.
0 on: "DMO SIHA ASEMA KUWA UTOAJI WA DAWA ZA MINYOO MASHULENI YAFIKIA 97% KATIKA WILAYA YA SIHA."