Naibu Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt
Faustine Ndugulile akitoa maelekezo kwa mhandisi wa Majengo wakati
alipofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa hospitali ya Mkoa wa Mara.
Naibu Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt
Faustine Ndugulile akisikiliza kero kutoka kwa mgonjwa aliyefika kupata
huduma za afya katika kituo chá Afya Nyasho Mkoani Mara.
Naibu Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt
Faustine Ndugulile akisikiliza maoni ya mama alipofanya ziara katika
wodi ya kujifungulia katika kituo chá Afya chá Nyasho Mkoani Mara.
Naibu Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt
Faustine Ndugulile akimjulia hali Mtoto aliyefika na mama yake katika
kituo chá Áfya chá Nyasho
Naibu Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt
Faustine Ndugulile akimsalimia moja kati ya wazee aliyefika kupata
huduma za afya katika kituo chá Áfya chá Nyasho Mkoani Mara huku
akimsisitiza kuwa matibabu ni bure kwa wazee wote wasio na uwezo
wakuchangia.
Dkt. Faustine Ndugulile (wakatikati) akiendelea na ziara yake ya kutembelea ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Serengeti.
SERIKALI YAIPATIA MKOA WA MARA BILION 5.9 KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA YA MAMA NA MTOTO.
Na WAMJW-MARA
SERIKALI
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto
imeupatia Mkoa wa Mara kiasi cha shilingi Bilion 5.9 ikiwaq ni moja ya
jitihada za kuboresha hali ya utoaji huduma za Afya kwa wananchi katika
mkoa huo.
Hayo yamesemwa
na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto
Dkt. Faustine Ndugulile mapema leo wakati akiwa katika ziara yake ya
Kukagua hali ya utoaji huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara.
“Mkoa
wa Mara umepokea Bilion 5.9 kwaajili ya kuboresha vituo vya kutolea
huduma za Afya 13, ikiwa ni jitihada za Serikali katika kuboresha hali
nya utoaji huduma kwa wananchi wake “ alisema Dkt Ndugulile.
Pia
Dkt. Ndugulile aliagiza kamati ya ulinzi ya Wilaya ya Tarime ikiongozwa
na Mkuu wa Wilaya Mhe. Vicent Naano kusimamia vizuri manunuzi ya Dawa,
huku akiagizi Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Mwanisi kuhakikisha dawa zote
zinunuliwe kutoka Bohari ya Dawa (MSD).
“Hutaratibu
wa kuagiza Dawa kwa mawakala sitaki kuusikia, MSD tuna dawa karibia
zote za msingi, utaratibu wa mawakala tuliuweka kama mbadala endapo MSD
watakosa aina Fulani ya dawa” Alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha,
Dkt. Ndugulile alisema kuwa mimba na ndoa za utotoni bado ni tatizo
kubwa ambapo mkoa wa Mara ni wa tano kitaifa kwa kuwa na asilimia 37.
“Serikali
imeandaa Mpango wa kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza ukatili dhidi ya
wanawake na watoto wa mwaka 2017/18-2021/22 na moja kati ya msisitizo
katika mpango huu ni kutokomeza ukatili wa kijinsia shuleni” alisisitiza
Dkt. Ndugulile
Aidha
Dkt. Ndugulile amekemea mahusiano ya kingono yaliyopo baina ya walimu na
wanafunzi na kuwataka wanafunzi kuacha kufanyiana vitendo vya ukatili
na kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili.
Kwa
upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt. Mwanisi alisema kuwa Idara
ya Afya ina upungufu mkubwa wa watumishi mkoani hapo ambao ni 3477 sawa
na Asilimia 60.9 ikilinganishwa na watumishi 2237 sawa na Asilimia 39.1
waliopo sasa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya hadi kufikia mwezi
Juni 2018.
Dkt. Mwanisi
aliendelea kusema kuwa hali ya maambukizi ya VVU yamepungua kutoka
Asilimia 4.5 mwaka 2011 hadi Asilimia 3.6 mwaka 2016/2017 kulingana na
utafiti wa kitaifa uliofanyika mwaka 2011-2012 na 2016-2017 huku
akisema kuwa wanaendelea kufanya juhudi mbali mbali za kupambana na
UKIMWI ili kuhakikisha maambukiz mapya yanaendelea kupungua.
Kwa
upande mwingine Mganga Mkuu wa Mkoa alisema hali ya chanjo hadi kufikia
Disemba 2017 kwa watoto chini ya mwaka mmoja waliomaliza chanjo zote
kimkoa ilikuwa Asilimia 143 ambayo ipo juu ya lengo la kitaifa ambalo ni
Asilimia 90.
0 on: "SERIKALI YAIPATIA MKOA WA MARA BILION 5.9 KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA YA MAMA NA MTOTO."