Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akiongea na
Wananchi wa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu wakati wa ufunguzi wa mradi
wa Tuwatumie ambao unawaajiri wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika
vijiji vyote vya halmashauri hiyo chini ya ufadhili wa AMREF
Wadau mbalimbali wa sekta ya afya walifuatilia hotuba ya mgeni
rasmi(hayupo pichani) aliyekaa kushoto ni Niall Morris Mkuu wa Arish
Aid,Dar.Aisa Muya -Kaimu Mkurugenzi Mkazi Amref Tanzania(katikati) na
kulia ni Dkt.Helen Senkoro Mkurugenzi wa Benjamin Mkapa Foundation
Wananchi waliojitokeza kushuhudia ufunguzi wa mradi huo ambapo watoa
huduma hao watakua kiungo kati ya wananchi na vituo vya kutolea huduma.
Waziri Ummy Mwalimu akifungua mradi huo
MARUFUKU KUAJIRI WATOA HUDUMA NGAZI YA JAMII NJE YA ENEO HUSIKA.
NA WAMJW-SIMIYU.
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imepiga marufuku kuajiri watoa huduma wa afya ngazi za jamii kutoka nje ya Halmashauri husika.
Katazo
hilo limetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa mradi wa TUWATUMIE
uliofanyika mkoani Simiyu wilaya ya Itilima.
"Nataka
kuwaambia viongozi wa Mkoa na Wilaya nchi nzima pamoja na taasisi
zisizo za kiserikali ni marufuku kuajiri wahudumu wa afya ngazi ya jamii
(CHW) kutoka nje ya makazi yao ili kusiwe na kutotofautiana
kimazingira,kwani wenyeji wanajua tamaduni na mila za wakazi wanapotoka"
alisema Waziri Ummy.
Waziri
Ummy amesema kuwa watoa huduma ngazi ya jamii wanatakiwa kuwa
kipaumbele katika kukinga kuliko kutoa tiba ili kupunguza idadi ya
wagonjwa na kuokoa fedha.
"Nataka
kuwaambia wahudumu wa afya ngazi ya jamii wanatakiwa kuweka kipaumbele
kinga kuliko tiba kwani mimi ni Waziri wa Afya na sio Waziri wa
wagonjwa,siwezi kusubiri watu wale ,nitawatumia CHW kuwakinga ama
kuwazuia wanaoumwa kupata matibabu" alisema Waziri Ummy.
Alisema
nchi ipo kwenye mikakati ya kufikia malengo endelevu ya millennia ya
kumfikia kila mtanzania kwa wakati na popote,hivyo kwa kuanza CHW
wanaanza eneo la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Amref Tanzania Dkt. Aisa Muya
amesema kuwa asilimia 50 ya miradi yao wanatumia watoa huduma za afya
ngazi ya jamii .
Aidha,
Dkt. Muya amesema kuwa wametoa mafunzo kwa watoa huduma 2,265 na mradi
huo utawaajiri watoa huduma 2,015 mbapo Wilaya ya Itilima watakuwa 102
na Misungwi 113 ambao wataenda kwenye vijiji vyote vya wilaya hizo.
Dkt.
Muya amesema kuwa matarajio ya mradi huo ni kuwatumia watoa huduma hao
kama kiungo kati ya jamii na vituo vya kutolea huduma za afya.
0 on: "MARUFUKU KUAJIRI WATOA HUDUMA NGAZI YA JAMII NJE YA ENEO HUSIKA."