Waziri wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee
na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akikagua shughuli za ujenzi wa jengo la
wodi ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou toure wakati
alipotembelea kukagua shughuli za ujenzi wa jengo hilo jijini Mwanza.
Waziri wa afya,Maendeleo ya
jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akipata maelezo kutoka
kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kushoto wakati
alipotembelea kukagua shughuli za ujenzi wa jengo la Mamlaka hiyo jijini
Mwanza. Kulia ni Mkurugenzi wa Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya afya
Dkt. Mohammed Mohammed.
Waziri wa afya,Maendeleo ya
jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akipata maelezo juu ya
sukari zinazopimwa ubora wake kutoka kwa
Mkuu wa Maabara wa TFDA Kanda ya Ziwa
Bw. Salum Kindoli wakati alipotembelea kukagua shughuli za ujenzi wa jengo la
Mamlaka hiyo jijini Mwanza.
Waziri wa afya,Maendeleo ya
jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akipata baadhi ya maelezo kutoka kwa
Mkurugenzi wa Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya afya Dkt. Mohammed
Mohammed kushoto wakati alipotembelea kukagua shughuli za ujenzi wa jengo la
Mamlaka hiyo jijini Mwanza.
Baadhi ya mafundi wakiendelea na
shughuli za ujenzi wa wa jengo la wodi
ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou toure
jijini Mwanza.
SERIKALI
KUFUTA TOZO YA USAJILI,KUHUWISHA NA KUSHIKILIA USAJILI KWA WAWEKEZAJI WA NDANI.
NA
WAMJW-MWANZA
SERIKALI kupitia wizara ya
afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imefuta tozo ya usajili ,
kuhuwisha pamoja na kushikilia usajili wa bidhaa zao kwa wawekezaji wa ndani
kupitia Mamlaka ya chakula na Dawa TFDA .
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati
alipotembelea kuangalia ujenzi wa jengo la TFDA ambalo linajengwsa Jijini
Mwanza ili kusogeza huduma kwa wananchi wa mkoa huo.
“Ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt.
John Pombe Magufuli za kukuza nchi kupitia uchumi wa viwanda hivyo TFDA msiwe
kikwazo kwa wawekezaji hao hivyo kuanzia leo nafuta tozo za kusajili
bidhaa,kuhuwisha bidhaa na tozo ya kushikilia usajili wa bidhaa”, alisema
Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa kuendana
na juhudi hizo pia Serikali imefuta tozo
ya udhibiti ya thamani ya 0.25 za
dawa,vifaa na vifaa tiba zinazoingizwa kwenye hospitali za Umma kutoka kwa
wafadhili.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa
TFDA ina wajibu wa kusimamia Tanzania isiwe jalala la bidhaa zisizo na ubora
kwa watanzania hivyo wanatakiwa kuweka afya ya wananchi mbele kuliko manufaa
binafsi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
TFDA Bi. Agness Kijo amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo ukikamilika utasaidia
kuhudumia huduma za kimaabara kwa bidhaa zinazoingia nchini kwani itakuwa sio
lazima tena kwenda kupima bidhaa hizo jijini Dar es salaam.
“Maabara hizi zikikamilika zitasaidia
kufanya vipimo na udhibiti wa bidhaa katika mipaka mingi ya kanda ya ziwa
ikiwemo Silali,Lusumo na Mtukula ili kuweka usalama wa bidhaa zinazoingia na
kutoka nje ya nchi kwa usalama wa wananchi.
Sambamba na hilo Waziri Ummy alipata
nafasi ya kutembelea kukagua ujenzi wa jengo la wodi ya mama na mtoto katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou toure na kuhakikisha ujenzi
unakamilisha ili kuokoa vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na uzazi.
“Kama watu wa mwanza wanaridhishwa na
huduma zinazotolewa katika hospitali hii basi ni lazima huduma za afya
ziboreshwe ikiwemo afya ya mama na mtoto hivyo ninaleta mashine ya CT Scan kwa
ajili ya kuboresha matibabu hapa” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy aliwataka watendaji wa
Hospitali kutoa taarifa za utendaji kwa
Waziri wa Afya na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo pamoja na kusimamiwa na Wakuu wa
Mikoa yao ili kuimarisha huduma za afya nchini.
0 on: "SERIKALI KUFUTA TOZO YA USAJILI,KUHUWISHA NA KUSHIKILIA USAJILI KWA WAWEKEZAJI WA NDANI."