Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Leonard Subi akifungua Mkutano wa mafunzo wa nchi 21 ambazo
zina maambukizi ya Ugonjwa wa Trakoma (Vikope) uliofanyika katika jiji
la Arusha.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt. Timothy Wonanji akiongea na Wadau
kutoka nchi mbali mbali wa magonjwa ya Trakoma(Vikope) katika kikao
kilichofanyika jijini Arusha huku lengo likiwa kuhimarisha mkakati wa
namna ya kugundua ugonjwa wa Trakoma na jinsi yakuweka takwimu sahihi
katika nchi hizo 21.
Mratibu wa Taifa wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele chini ya
Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazeee na watoto Dkt .
Upendo Mwingila akionga kwa kifupi juu ya hali ya ugonjwa wa Trakoma
nchini mbele ya Wadau wa ugonjwa wa Trakoma kutoka nchi 21.
Picha ya Wadau zaidi ya 100 kutoka nchi 21 ambao walihudhuria kikao
chenye lengo la kuhimarisha mkakati wa namna ya kugundua ugonjwa wa
Trakoma na jinsi yakuweka takwimu sahihi kilichofanyika jijini Arusha
Kundi namba 1 la Wataalamu likiongozwa na madaktari (Graders) wakijadili kuhusu ugonjwa wa Trakoma katika nchi zao.
Kundi namba 2 ni Wataalamu wa masuala ya Takwimu wakijadil namna ya uingizaji wa takwimu kwa usahihi.
Picha ya Pamoja ya Wadau kutoka nchi 21 wa ugonjwa ya Trakoma(Vikope)
walioshiriki katika kikao kilichofanyika jijini Arusha huku lengo likiwa
kuhimarisha mkakati wa namna ya kugundua ugonjwa wa Trakoma na jinsi
yakuweka takwimu sahihi katika nchi hizo 21.
WILAYA 58 ZAFANIKIWA KUDHIBITI UGONJWA WA TRAKOMA
Na WAMJW - ARUSHA
Mkurugenzi
wa Kinga Wizara ya Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto
Dkt. Leonard Subi amethibitisha kuwa halmashauri 58 nchini zimefanikiwa
kutibu ugonjwa wa trakoma kutokana na jitihada mbali mbali zilizofanywa na Serikali kwa ushirikiano na Wadau.
Alisema
hayo wakati akifungua Mkutano wa Uzinduzi wa Mafunzo kwa wawakilishi wa
nchi 21 ambazo zinamaambukizi ya ugonjwa wa Trakoma/ vikope huku lengo
likiwa ni kuwajengea wataalamu hao uwezo ili waweze kupambana dhidi ya
ugonjwa huu.
"Mwanzoni tulikuwa na Wilaya
takribani 75 ambazo zilikuwa na ugonjwa huu, jitihada zimeweza
kufanyika tangu 2014 hadi leo Hii Karibu Wilaya 58 zimeweza kushinda
dhidi ya ugonjwa huu, tumebakiza Wilaya 13 na kama Serikali tutaendelea
kutoa dawa na Elimu kwa umma ili waweze kujikinga dhidi ugonjwa huu ",
Alisema Dkt. Subi
Dkt
Subi aliendelea kusema kuwa sifa mojawapo ya kudhibiti ugonjwa huu ni
kupitia mafunzo yanayomjengea uwezo mtaalamu kuweza kujua namna ya kujua
ugonjwa, na kuweza kudhibiti dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huu
Kwa
upande mwingine Dkt. Subi ametoa wito kwa wananchi wote hususani
waliokatika hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa huu wa trakoma kuwa
Safi wakati wote kwa kunawa uso, kujenga vyoo na kusafisha mazingira
yanayotuzunguka mara kwa mara.
"ugonjwa huu
unatokana na uchafu, kama huogi, kama hunawi uso, unaweza sababisha
macho yako yakahathirika, ni vizuri kutumia Fursa ya maji vizuri kwa
kufanya usafi vizuri mda wote" alisema Dkt. Subi
Pia
Dkt Subi aliwahasa wananchi kutumia dawa Kwani ni salama na nzuri
ndiomaana zimeponya watu katika halmashauri 58 kufanikiwa kupambana
dhidi ya ugonjwa huu wa trakoma.
Kwa
upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt Thimothy Wonanji alisema kuwa
bado Wilaya tatu jijini Arusha zinaendelea kusumbuliwa na tatizo hili lá
trakoma, Wilaya hizo ni Longido, ngorongoro pamoja na Monduli na
kusema kuwa tatizo kubwa limeonekana kuwa ni changamoto ya upatikaaji wa
maji katika maeneo hayo.
Aliendelea
kusema kuwa Serikali katika ngazi ya Mkoa kuna uratibu wa Magonjwa
yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ambao kwa kushirikiana na wadau wamekuwa
na mradi wa kwenda kijijini na kupita nyumba kwa nyumba kuwapima wakazi
wa maeneo hayo na kuwaanzishia dawa (zitromas) kwa wanaogundulika kuwa
na ugonjwa huu.
Nae
Mratibu wa Taifa wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt Upendo
Mwingila alisema kuwa idadi ya wagonjwa wamepungua kutoka 160 Mpaka
mwaka huu wagonjwa elfu 25,000 hii inatoka na juhudi za Wizara ya Áfya
kupitia mpango wa taifa wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi
kipaumbele na Wadau mbali mbali katika kupambana dhidi ya ugonjwa huu wa
trakoma jambo lililosaidia kufanikisha kufanya upasuaji wa vikope
takribani 12,000 kwa mwaka.
0 on: "WILAYA 58 ZAFANIKIWA KUDHIBITI UGONJWA WA TRAKOMA"