|
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa kikao na wawakilishi wa Mfuko wa Pamoja
wa Dunia wa kushughulikia magonjwa ya TB,Maralia na Ukimwi(GLOBAL FUND) hawapo pichani kilichofanyika katika Ofisi
ndogo ya Wizara jijini Dar es salaam.
|
|
Mkurugenzi wa Mfuko wa Pamoja wa Dunia wa
kushughulikia magonjwa ya TB,Maralia na Ukimwi (GLOBAL FUND) hapa nchini Dkt. Sai Kumar kulia akimueleza
jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu wakati wa kikao cha kujadili mambo mbalimbali ya afya kilichofanyika
katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es salaam.
|
|
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu kulia akizungumza na
Naibu Waziri wake Dkt. Faustine Ndugulile kushoto wakati wa kikao na wawakilishi
wa Mfuko wa Pamoja wa Dunia wa kushughulikia magonjwa ya TB,Maralia na Ukimwi (GLOBAL
FUND) hawapo pichani kilichofanyika
katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es salaam.
|
|
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu katikati akizungumza wakati wa kikao na wawakilishi wa Mfuko
wa Pamoja wa Dunia wa kushughulikia magonjwa ya TB,Maralia na Ukimwi (GLOBAL
FUND) kilichofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es salaam. Kulia
ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile.
|
Na WAMJW-DSM
Mfuko wa pamoja wa Dunia wa kupambana
na magonjwa ya UKIMWI,Malaria na Kifua Kikuu (GLOBAL FUND) umeridhishwa
kwa kiasi kikubwa na Jinsi Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya
katika kupambana na magonjwa hayo.
Pamoja
na hayo Wawakilishi wa Mfuko huo hapa Nchini wamesema kuwa kutokana na
mwenendo mzuri wa Tanzania katika kutumia vizuri Mfuko huo sasa wanaweza
kuanzisha kitu kingine kizuri kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya na
kupeleka mapendekezo na kukubaliwa.
Malengo ya kikao hiko kati ya Global Fund na Wizara ya Afya ilikuwa ni kujadili ,kupanga na kuboresha Sekta ya Afya nchini.
0 on: "GLOBAL FUND YARIDHISHWA NA UTENDAJI WA WIZARA YA AFYA NCHINI."