TANZANIA imepata pongezi kutoka kwa Kituo cha
Kimataifa cha kufuatilia , kutathimini , kutoa taarifa na kuchukua hatua (CDC)
kwa kufanya vizuri katika utekelezaji huo hasa katika magonjwa ya mlipuko.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa kikao cha kuangalia hali ya
utendaji katika sekta ya Afya nchini.
"Wenzetu wa CDC kutoka Marekani wanatusaidia kujenga uwezo wa
kufuatilia , kutoa taarifa na kuchukua hatua juu ya magonjwa ya mlipuko kama
vile Ebora na Kipindupindu na wameridhika kwa utendaji wetu hapa nchini"
alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Tanzania imeimarika
katika kufanya uchunguzi , kutathimini ,
kutoa taarifa na kuchukua hatua juu ya magonjwa mbalimbali.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa magonjwa hayana mipaka hivyo ni lazima
kuwa waangalifu na kuchukua hatua mda
wote kwa kujenga mifumo imara ya ufuatiliaji.
Kwa upande wake
Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Bi. Inmi Petterson amesema kuwa
wamefurahishwa na kazi ya wataalamu wa afya waliowekwa hapa nchini katika
kupambana na magonjwa na kuahidi kuongeza nguvu kubwa ikiwemo vitendea kazi.
Aidha Balozi Inmi amesesema kuwa Serikali ya
Tanzania inatakiwa kushirikiana na wananchi wa Tanzania katika kupata taarifa
sahihi za magonjwa na kujenga nchi yenye wananchi wenye afya bora.
0 on: "TANZANIA YAPONGEZWA NA CDC UFUATILIAJI, UTOAJI TAARIFA ZA MAGONJWA KIMATAIFA"