PICHA ZINAZOONYESHA TUKIO LA UTIAJI SAINI MAKUBALIANO YA UJENZI WA MADARASA 6 KATIKA SHULE YA MSINGI MWAKIDILA MKOANI TANGA KATI YA UBALOZI WA JAPAN NA TAASISI YA MAENDELEO YA WANAWAKE TANGA ( TAWODE).
NA WAMJW-DAR ES SALAAM.
Serikali ya Japan kupitia ubalozi wa Japan nchini Tanzania
imetoa kiasi cha shilingi miliioni 188 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 6 ya
shule ya msingi Mwakidila kata ya Tangasisi iliyopo Jijini Tanga
Fedha hizo zimetolewa leo jijini hapa kupitia Shirika la Maendeleo ya Wanawake wa Mkoa wa
Tanga (TAWODE) chini ya Mwenyekiti wake Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu .
Ubalozi wa Japan nchini imetoa fedha hizo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha miundombinu ya elimu ya Msingi na Sekondari
katika jiji la Tanga.
Akiongea wakati wa hafla ya kutia saini mkataba wa ujenzi
wa madarasa hayo Balozi wa Japan Nchini Tanzania Mhe. Masaharu Yoshida alisema Serikali ya japan imetoa fedha
hizo ili kusaidia maendeleo ya elimu kwa
Jiji la Tanza ili kutatua tatizo la
mrundikano wa wanafunzi madarsani
Aidha, Balozi Yoshida
ameitaka TAWODE kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kikamilifu na kukamilisha ujenzi huo wa madarasa kwa
wakati.
Akiongea wakati wa kutiana saini mkataba huo Mwenyekiti wa
TAWODE, Waziri Ummy Mwalimu ameushukuru Ubalozi wa Japan nchini kwa kukubali
ombi la kufadhili ujenzi wa madarasa ya
shule hiyo ya Msingi Mwakidila ambayo
ina wanafunzi zaidi ya 1,400 kulinganisha na madarasa yaliyopo.
“Sisi kama sehemu ya wanajamii wa Jiji la Tanga tuliona
tuna wajibu wa kuunga mkono Serikali kwa kutafuta vyanzo vingine vya fedha ili
kuwezesha elimu ya Msingi na ile ya sekondari hususan changamoto ya madarasa
itatuliwe hivyo fedha hizi ni za jamii ya Wana Tanga hivyo TAWODE tutahakikisha
zinatumika ipasavyo”.Alisema Waziri Ummy.
Hata hivyo alisema hivi sasa kumekuwa na changamoto ya
madarasa kwenye halmashauri mbalimbali nchini kutokana na ongezeko la wanafunzi kutokana na
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt.John Magufuli ya kutoa elimu
bure .
Kwa upande wake Meya wa Jiji la Tanga Mhe.Selebosi Mhina
ameushukuru Ubalozi wa japan pamoja na kumpongeza Mhe.Ummy mwalimu kwa kuwa
bega kwa bega katika kusukuma mbele
maendeleo ya wananchi wa Tanga katika sekta ya Elimu na Afya.
0 on: "UBALOZI WA JAPAN YAMUUNGA MKONO MHE. UMMY KUJENGA MADARASA MKOANI TANGA"