Mkurugenzi wa taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt Julius Mwaiselage
akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu juu ya ufanisi wa
mashine mpya na yakisasa ya mionzi iliyopo katika taasisi hiyo.
Mtaalamu wa masuala ya mionzi kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Hemed Myanza akitoa majibu ya moja ya swali lililoulizwa na Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu pindi alipofanya ziara katika taasisi hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akimsililiza ndugu wa moja kati ya wagonjwa waliofika
Hospitalini hapo kupata huduma za matibabu ya Saratani.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akisikiliza malalamiko ya mama aliekuwa akisubiri matibabu ya
ugonjwa wa kansa katika taasisi hiyo ya Ocean Road. Wa katikati ni
Mkurugenzi wa taasisi hiyo Dkt. Julius Mwaiselage.
Mashine ya Kisasa ya Linear Accelerator iliyounganishwa na CT simulator zote mbili zikiwa na gharama ya shilingi Bilion9.5 iliyojumuishwa na mafunzo ya Wataalamu na matengenezo kinga ya miaka miwili.
WAZIRI UMMY ATEMBELEA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD
NA KUWATAKA WAKAMILISHE HARAKA UFUNGAJI WA MASHINE MPYA ZA MIONZI ILI
KUHAKIKISHA HUDUMA BORA ZAIDI KWA WAGONJWA WA SARATANI NCHINI
Na WAMJW-Dar Es Salaam.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu
(Mb), amefanya ziara ya kikazi katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road
ili kukagua utoaji wa huduma za Matibabu katika Hospitali hiyo.
Katika
ziara hiyo, Mhe. Waziri alifahamishwa kwamba mashine zote za tiba ya
mionzi ya nje inafanya kazi vizuri na huduma zinaendelea kutolewa kwa
wagonjwa.
Pia wakati wa
ziara hiyo, Mhe.Ummy alitumia fursa hiyo kuzungumza na wagonjwa
mbalimbali waliokuwa wakipata huduma za tiba ya mionzi hospitalini
hapo, huku baadhi ya wagonjwa walitoa malalamiko kwa Waziri kuwa,
wamekuwa wakitumia muda mrefu kusubiri kupata huduma hususani huduma za
mionzi ya nje.
Kufuatia
hali hiyo, mhe. Ummy alitoa maelekezo kwa uongozi wa Hospitali
kuhakikisha wanaweka utaratibu mzuri ambao utapunguza muda kwa wagonjwa
kusubiri huduma za mionzi ikiwemo kuwepo na ratiba ambayo kila mgonjwa
atajua anafika saa ngapi kupata tiba hiyo.
Vile
vile, mhe. Ummy alitembelea kitengo cha utoaji wa huduma za mionzi ya
ndani ambapo alijionea changamoto ya kutokufanya kazi kwa mashine hizo
za utoaji wa mionzi ya ndani kutokana na kukosekana kwa vifaa vya
'transfer tubes' na 'gyn applicators'.
Kufuatia
hali hiyo mhe.Ummy alitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Ocean Road, Dkt.Julius Mwaiselage kuhakikisha kuwa mashine hizo
zinafanya ndani ya siku 2 kwa kuazima hivyo vifaa hivyo kutoka Hospitali
ya Bugando ili kurudisha huduma hizo kwa wagonjwa ambao wengi ni
wanawake wenye tatizo la Saratani ya Mlango wa Kizazi.
"Naelekeza kuwa fanyeni utaratibu wa kupata kifaa kilichoharibika mapema iwezekanavyo" alisema mhe.Ummy.
Naye
Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road , Dkt.Julius Mwaiselage
alimhakikishia mhe.Waziri kuwa atajitahidi ili vifaa vilivyoharibika
vinapatikana ndani ya siku mbili kutoka Hospitali Bugando na pia
wameagiza vifaa hvyo kutoka kiwandani nje ya nchi kwa gharama ya Euro
43,200.00
0 on: "WAZIRI UMMY ATEMBELEA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD NA KUWATAKA WAKAMILISHE HARAKA UFUNGAJI WA MASHINE MPYA ZA MIONZI ILI KUHAKIKISHA HUDUMA BORA ZAIDI KWA WAGONJWA WA SARATANI NCHINI"