Katibu Mkuu Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akihutubia mbele ya Wageni na Waandishi wa Habari katika uzinduzi wa
mkutano wa kujadili, kupitia na kupanga utekelezaji wa mpango kazi
katika kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele jijini Dar es
salaam.
Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele Dk. Upendo Mwingira akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (Hayupo kwenye picha)
Picha ya pamoja ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa uzinduzi wa
mkutano wa kujadili, kupitia na kupanga utekelezaji wa mpango kazi
katika kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbel.
Na WAMJW-DAR ES SALAAM
WILAYA
93 nchini yafanikiwa kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele
yakiwemo matende na mabusha ambapo wilaya hizo awali zilikua zikihitaji
kingatiba lakini kwa sasa hazihitaji kinga hizo.
Hayo yamesemwa
na Katibu mkuu Wizara ya afya Dkt. Mpoki Ulisubisya katika uzinduzi wa
mkutano wa kujadili, kupitia na kupanga utekelezaji wa mpango kazi
katika kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele jijini Dar es
salaam.
“Tumetoa dawa na tunaendelea kwa watanzania wapatao
milioni 29 kati ya milioni 50 hivyo kupiga hatua kubwa katika kudhibiti
magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele hapa nchini kwetu” alisema Dkt.
Ulisubisya.
Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa
mkutano huo uliokutanisha wadau wa afya wa nje na ndani ya nchini
unalenga kutoka na mkakati wa kupambana na magonjwa yaliyokuwa hayapewi
kipaumbele hasa maeneo ya vijijini.
Kwa upande wake
Mratibu wa Taifa wa mpango wa kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi
kipaumbele nchini Dkt. Upendo Mwingira amesema kuwa wananchi wanatakiwa
wajitokeze kwenye mazoezi ya kupata dawa za kuzuia mabusha na matende.
“Tunatakiwa
kujitokeza kila mwaka mara pindi itakapotangazwa kuwa ni kipindi cha
kupata dawa hizo na mwaka huu dawa hizo zitatolewa Septemba kwa
watanzania wote” alisema Dkt. Mwingira.
Aidha Dkt.
Mwingira amesema kuwa mbali na mafanikio yaliyopatikana katika kampeni
hiyo ya kutokomeza magonjwa hayo pia kuna changamoto za utoaji elimu na
uhamasishaji katika matumizi ya dawa hizo.
Hata hivyo amesema kwa upande wa ugonjwa wa Vikope (Trakoma) wamefanikiwa kusitisha kugawa dawa kwa wilaya 58 kati ya 71 nchini.
Mbali
na hayo Dkt. Mwingira amesema kuwa katika kuhakikisha magonjwa hayo
yanapotea nchini wamejidhatiti kuzindua kampeni ya kuwafanyia upasuaji
watu 350 Kisarawe Mkoani Pwani.
MWISHO
0 on: "WILAYA 93 NCHINI ZAFANIKIWA KUTOKOMEZA MATENDE NA MABUSHA."