Waziri wa Afya,Maendeleo ya
jamii,Jinsia,Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akikagua vifaa vipya
vilivyowekwa kwenye chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Benjami Mkapa
wakati wa uzinduzi wa Bodi ya udhamini na chumba cha uchujaji damu Hospitalini
hapo leo jijini Dodoma.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
jamii,Jinsia,Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akikagua chumba cha
kusafishia maji ya wagonjwa wa figo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa wakati
wa uzinduzi wa Chumba cha uchujaji damu kwa wagonjwa wa figo leo jijini Dodoma,
Kulia mwenye koti jeupe ni Daktari Bingwa wa Figo Dkt. Kessy Shija.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee
na watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kulia Dkt. Alponce Chandika kuhusu kengere za kuitia wauguzi katika wodi
ya wagonjwa wa figo wanaochujwa damu kwenye Hospitali hiyo wakati wa uzinduzi
wa Bodi ya udhamini na chumba cha uchujaji damu leo jijini Dodoma.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
jamii,Jinsia,Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria kuzindua
rasmi miongozo ya Bodi ya udhamini katika Hospitali ya Benjamin Mkapa
iliyozinduliwa leo jijini Dodoma.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
jamii,Jinsia,Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria kuzindua
rasmi jengo la kuchuja damu kwa wenye matatizo ya figo katika Hospitali ya
Benjamin Mkapa jijini Dodoma leo.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
jamii,Jinsia,Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi vitendea kazi
Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Hospitali ya
Benjamin Mkapa Dkt. Deodatus Mtasiwa kushoto baada ya kuzinduliwa rasmi
kwa bodi hiyo leo jijini Dodoma.
Na WAMJW-Dodoma
Magonjwa yasiyo ya kuambukizwa kama
moyo,figo na mengineyo yanaongezeka kwa kasi duniani kote na hapa nchini
yamekua yakigharimu Serikali kiasi cha
shilingi Bilioni 36.6 kwa mwaka.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo
ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa bodi ya
wadhamini ya Hospitali ya Benjamin Mkapa leo Jijini Dodoma.
Waziri Ummy amesema hapa nchini kwa
takwimu za Julai 2013 hadi Juni 2016 magonjwa ya Moyo na Figo ndiyo yalikuwa
yakiongoza kwa idadi kubwa ya wagonjwa
kutibiwa nje ya nchi na kugharimu
Serikali kiasi hicho cha fedha.
“Kati ya wagonjwa 560 waliosafirishwa
na Serikali wagonjwa 430 walienda
kutibiwa moyo na wagonjwa 160 walienda kupandikizwa figo ”alisema Mhe.Ummy.
Aidha, Waziri Ummy alisema kuwa kwa
takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) magonjwa yasiyoambukiza yanachangia
vifo kati ya watu mia moja watu sitini
hufa kwa magonjwa hayo na kati ya wagonjwa 100 watu 47 wanaugua magonjwa yasiyoambukiza
Waziri Ummy aliongeza kuwa kwa
kuanzishwa hospitali ya Benjamin Mkapa kutaokoa kiasi kikubwa cha fedha na
kuipunguzia Serikali mzigo mkubwa wa
gharama na badala yake fedha hizo zitatumika kuimarisha miundombinu ya hospitali
za hapa nchini.
Hata hivyo aliitaka bodi hiyo ya
wadhamini kuongeza kasi ya utekelezaji
wa mikakati ya kuboresha huduma za afya ili kuvutia wagonjwa wengi zaidi
kutibiwa hospitalini hapo na kupunguza rufaa za wagonjwa wanaopelekwa nje ya
nchi kwa matibabu.
“Nawaomba mkachape kazi bila kuchoka ili hospitali hii ikawe na tija
katika kuwahudumia watanzania na hata ndugu zetu wa nchi jirani hasa za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika huduma za
matibabu ya Kibingwa”,Alisisitiza Waziri Ummy.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali hiyo Dkt. Alponce Chandika alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa
hospitali hiyo ni kutoa huduma za afya maalum za Kibingwa ikiwemo uchunguzi wa
magonjwa ya Moyo,Figo,Macho,Damu, Saratani pamoja na kutoa huduma za upasuaji kwa kutumia matundu madogo(endoscope).
“Mbali na huduma hizo hospitali yetu
inatumika kwa ajili ya kufundisha wataalamu wa kada za afya,kufanya tafiti na
huduma za kliniki tembezi” alisema Dkt.Chandika.
Dkt.Chandika alisema kuwa wanatarajia
mwezi Agosti kufanya tena upandikizaji
wa figo kwa wagonjwa watatu pia wanatarajia kufanya upasuaji wa matundu
madogo kuanzia mwezi Julai mwaka huu
Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo
Dkt.Deodatus Mtasiwa alisema kuwa Serikali na wananchi wanatarajia huduma nzuri
katika hospitali hiyo hivyo hawanabudi kushirikiana na hospitali mbalimbali
zinazotoa huduma za Kibingwa ili kutoa huduma stahili hapa nchini.
Sambamba na uzinduzi wa bodi hiyo
yenye wajumbe sita Waziri Ummy alizindua
kitengo cha kuchuja damu katika hospitali ya Benjamin Mkapa.
0 on: "MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA YAONGEZEKA"