Mafundi wakiwa katika hatua ya mwisho ya kumalizia
jengo la Mochwari lilipo katika Kituo cha Afya Mundemu Wilayani Bahi Mkoa Dodoma
.
|
NA WAMJW-DODOMA
WAZIRI wa Afya,maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameweka jiwe la msingi katika Kituo cha Afya Mdemu
kilichopo Wilayani Bahi Jijini Dodoma baada ya kuridhishwa na ujenzi huo.
Akizungumza wakati wa kuweka jiwe hilo la msingi
Waziri Ummy alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe
Magufuli imefanya kipaumbele maboresho mbalimbali hususan katika sekta ya afya
nchini.
“Nilipofika hapa mwaka 2016 niliona wanawake wajawazito
wanalala kwa kubanana na wengine wanafariki kwa uzazi pingamizi hivyo nikaona
tuanze kujenga vyumba vya upasuaji wa dharura nchini ikiwemo wodi ya wanawake wajawazito ili kuokoa Maisha
ya mwanamke na mtoto anapojifungua ” alisisitiza Waziri Ummy.
Aidha, Waziri Ummy alisema kuwa mpaka sasa wilaya ya
Bahi imefikia asilimia 98 ya wanawake wajawazito kujifungulia katika vituo vya
afya amabapo Kitaifa inaonesha katika kila wanawake 100 wanawake 51 ndo hijifungilia kwenye vituo vya afya.
Vilevile Waziri Ummy amesema kuwa Juhudi za Serikali
katika kuokoa vifo vya wakina mama wajawazito Kijijini Mundemu atawapatia gari ya kubebea
wagonjwa kwa ajili ya rufaa kutoka kituo kituoni hapo kwenda Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Bahi Bi. Benadertha Januari amesema kuwa wamefanikiwa kupunguza vifo
vitokanavyo na uzazi kutoka vifo 4 mwaka 2015 mpaka vifo 3 mwaka 2017 na vifo
vya watoto chini ya miaka 5 kutoka 50 mwaka 2015 mpaka kufikia vifo 12 2017.
Aidha Bi. Januari amesema kuwa wamefanikiwa
kukusanya chupa za damu salama 1640 kati ya chupa 2216 ya malengo waliojiwekea
ambayo ni sawa na asilimia 74 kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Juni mwaka
huu.
Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Kata ya Mundemu Bw.
Reuben Ntiruka amesema kuwa Kituo cha afya Cha Mundemu kinapokea rufaa ya
kutoka Zahanati 21 za vijiji vitatu ambayo idadi ya walengwa wake ni wananchi
9103.
Mbali na hayo Bw. Ntiruka ameiomba Serikali
kuijengea Kituo hicho Uzio ,nyumba za watumishi, kuongeza idadi ya
watumishi pamoja gari ya kubebea
wagonjwa kwani ndio changamoto kubwa zinazoikumba Kituo hicho cha afya.
0 on: "UMMY MWALIMU AWEKA JIWE LA MSINGI KITUO CHA AFYA MUNDEMU"