Wadau mbali mbali wa wa masuala mbali mbali ya VVU wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi ambae ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya Dkt.
Angera Ramadhan ikiwa ni kuelekea katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya Furaha
yangu,mkoani Dodoma Juni 19 mwaka huu,inayohusisha upimaji wa VVU na
kuanza kutumia ARV.
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa,anatarajiwa kuzindua kampeni ya kitaifa ya Furaha
yangu,mkoani Dodoma Juni 19 mwaka huu,inayohusisha upimaji wa VVU na
kuanza kutumia ARV
Hayo
yamezungumzwa na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya Dkt.
Angera Ramadhan,
Kampeni hiyo imetajwa kuhamasisha mkakati wa
serikali wa upimaji wa VVU na kuanza kutumia ARV mapema kwa wale
watakaokutwa na maambukizi.
"Asilimia
45 ya wanaume wanajijua kuwa wanaishi na maambukizi ya VVU na asilimia
55 hawajijui huku wanawake waliokuwa wanajijua kuwa wanamaambukizi ni
asilimia 56 na 44 bado hawako tayari" alisema Dkt. Angera
Dkt.
Angera amesema kuwa Kuanza ARV mapema kutapunguza wingi wa VVU
mwilini na kuimarisha kinga kwa wagonjwa,hivyo kampeni hii kwa wanaume
itakuwa chachu ya kujua afya zao na wengi kuwa tayari kwa kuimarisha
afya na kupunguza hatari ya kuambukiza wenza wao.
Aidha
Dkt. Angera amesema kuwa serikali itaendelea kubuni mbinu mbadala ili
kufikia malengo ya dira ya taifa ya kutokomeza maambukizi ya Ukimwi
iliyoridhia malengo ya UNAIDS ya 90-90-90 ambayo ni kuhakikisha asilimia
90 ya watu wote wanaoishi na VVU wanatambua afya zao,wanaanza dawa na
kupunguza maambukizi mapya.
Naye
Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI TACAIDS, Dkt. Leornad
Maboko,alisema uzinduzi wa kampeni hiyo utakuwa na siku tano za kutoa
huduma za afya bila malipo,ikiwemo upimaji wa VVU na magonjwa sugu.
Aidha
Dkt. Maboko alisema kuwa lengo la kuhamasisha kwa kauli ya Furaha
yangu Pima,Jitambur ,Ishi na mwanaume njoo kwenye huduma ni kutokana na
kubaini kundi hilo kubwa halifikiwi na ili kumaliza maambukizi ni
lazima kupewa hamasa.
"Hivyo
tunatoa wito wakazi wa Dodoma,mikoa ya jirani na mikoa sita ambayo ipo
katika awamu ya kwanza ya uzinduzi ikiwemo Njombe,Iringa na Mwanza
kumuunga mkono Waziri Mkuu kwa kujitokeza kwa wingi kujua afya zao na
ikigundulika kutumia dawa mapema ili kuiamrisha afya na kupunguza nguvu
ya VVU," alisema Dkt. Maboko.
0 on: "WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUZINDUA KAMPENI YA FURAHA YANGU JUNI 19 DODOMA"