Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye kilemba cha bluu) akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila jijini Dar es Salaam. Pembeni kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Huduma za Hospitali, Prof. Said Aboud.
NA WAMJW-MLOGANZILA
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya muungano
wa Tanzania Bi. Samia Suluhu Hassan amehaidi kuiongezea fedha za dawa hospitali Mloganzila Sh.
milioni 600 mpaka kufikia Sh. milioni 900 ili kukabiliana na changamoto ya
upungufu wa dawa hospitalini hapo.
Hayo ameyasema wakati alipofanya
ziara yake ya kuangalia hali ya utoaji huduma katika Hospitali ya Mloganzila
iliyopo nje kidogo ya jiji la Dar es salaam leo alipoambatana na Waziri wa
Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
“Tatizo hata fedha mliyopewa awali
mkichukua dawa MSD hamrudishi tena fedha kule, hakikisheni hizi fedha
tunazowaongeza mlipe bili MSD ili iweze kuleta dawa nyingi zaidi angalau nusu
ya fedha muirejeshe tena huko,” alisema.Mhe. Samia.
Aidha Mhe. Samia ameiagiza pia
hospitali hiyo kufungua duka la dawa ili kuweza kuweka aina ya dawa ambazo
wamekuwa wakizikosa Bohari ya Dawa.
Mbali na hayo Mhe. Samia alikagua na kushangazwa na Wakala wa
Ujenzi Tanzania (TBA kwa kitendo cha kusuasua ujenzi wa mabweni katika
Hospitali ya Taaluma na Tiba Mloganzila.
Kwa upande wake Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliwataka wananchi kuchangia huduma za
matibabu kupitia bima za afya ili waweze kupata matibabu ya kibingwa ngazi za
juu bila vikwazo vya kifedha
“ Mloganzila ni miongoni mwa
Hospitali saba zinazomilikiwa na serikali zinazotoa matibabu ya kibingwa
ngazi ya juu na uwepo wake umeleta unafuu katika kuongeza wigo wa huduma na
mafunzo kwa wataalamu wa afya” alisema Mhe. Ummy.
Naye, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo
huduma za hospitali, Profesa Said Abood, alisema wamekuwa wakipata asilimia 24
pekee ya dawa wanazozihitaji kutoka MSD na dawa zingine wamekuwa wakizinunua
kupitia wakala mbalimbali.
|
0 on: "MAKAMU WA RAIS AHAIDI MILIONI 600 KUPAMBANA NA CHANGAMOTO ZA DAWA MLOGANZILA."