MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wa kwanza kulia akisalimiana na mtoto
Mussa Hussein alipofanya ziara katika hospitali ya CCBRT kwa matibabu ya miguu ambao wamewekewa vyuma, kushoto mwenye kiremba ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na katikati ni Mkurugenzi MKuu wa Hospitali ya CCBRT
Bw. Erwin Telemans wakati wa ziara yake katika hospitali hiyo leo jijini Dar es
salaam.
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wa kwanza kulia akisalimiana na mtoto na Abdul Hamadi (10)
alipofanya
ziara katika hospitali ya CCBRT kwa matibabu ya miguu ambao wamewekewa
vyuma, kushoto mwenye kiremba ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na katikati ni Mkurugenzi MKuu wa Hospitali ya
CCBRT
Bw. Erwin Telemans wakati wa ziara yake katika hospitali hiyo leo jijini
Dar es
salaam.
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akipata maelezo kutoka kwa
Mkurugenzi MKuu wa Hospitali ya CCBRT Bw. Erwin Telemans wa kwanza kulia kuhusu kiungo cha mguu bandia wakati wa
ziara ya Makamu wa Rais katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam, kulia
ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kulia akimjulia hali mtoto Luqman Mulid
(4) kushoto aliyelazwa katika hospitali ya CCCBRT akipata matibabu ya mguu
wakati wa ziara yake katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam.
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akipata maelezo kutoka kwa
Mkurugenzi MKuu wa Hospitali ya CCBRT Bw. Erwin Telemans wa kwanza kulia wakati wa ziara ya Makamu wa Rais katika
hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam, wa pili kushoto kutoka kwa Makamu wa
Rais ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na baadhi ya wadau wa
afya,madaktari,wauguzi na wagonjwa
hawapo pichani wakati wa ziara ya
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan katika Hospitali ya CCBRT jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Ali
Hapi akiongea na baadhi ya wadau wa afya,madaktari,wauguzi na wagonjwa hawapo pichani wakati wa ziara ya MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Hospitali ya CCBRT jijini Dar es
salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi akitoa neno mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe.Samia Suluhu
Hassan wakati alipofanya ziara katika hospitali ya CCBRT kwa matibabu ya miguu ambao wamewekewa
vyuma.
Na.WAMJW-DSM
Huduma za afya ya Mama na Mtoto kwa Mkoa wa Dar es Salaam imefikia asilimia 80 ukilinganisha na miaka ya nyuma iliyopita
Hayo
yamesemwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe.Samia Suluhu
Hassan katika ziara yake kwenye hospitali ya CCRBT leo jijiji Dar es
Salaam.
"licha ya Dar es
Salaam kufikia asilimia hii ni ya huduma za mama na mtoto bado
tunahitaji mafunzo ya kiutendaji na kitaalam kwa watoa huduma za afya
ili kupiga hatua zaidi nchi nzima"Alisema Mhe.Samia.
Hata
hivyo alisema kutokana na takwimu hizo Wizara ya afya inatakiwa kufanya
kazi na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ili kupata takwimunzinazofanana
kwenye utoaji wa huduma za afya nchi nzima.
Aidha,Makamu
wa Rais ameipongeza hospitali ya CCBRT kwa huduma nzuri wanazozitoa
hususan za wagonjwa wa Fistula kwa wanawake kwa miaka 25 nchini hivyo
kuwafanya wanawake wengi kurudisha heshima na utu wao
"Hakuna
jambo kubwa Duniani kama kumrudishia mtu utu na heshima kwa wanawake
waliokuwa wanatenga na hata pengine kukimbiwa,kweli kazi mnayoifanya ni
kazi ya Mungu" .
Kwa
upande wake Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
Mhe.Ummy Mwalimu amesema wanatambua kazi kubwa inayofanywa na wadau
wakiwemo CCRBT kwa mchango mkubwa wa kutoa huduma za afya nchini ikiwemo
huduma za afya ya Mama na Mtoto kwa kuwajengea uwezo watumishi wa afya
nchini pamoja na kujenga vyumba vya upasuaji kwenye vituo vya afya.
"tunaposema
fistula inatibika,lakini fistula inaepukika na kuzuilika pale
tutakapoboresha huduma za uzazi ikiwemo huduma za dharura,nina imani
wanawake wengi watajitokeza katika matibabu haya"alisema
Waziri
Ummy amesema wakati serikali ya awamu ya tano inaingia madarakani
kulikua na vituo vya afya vya serikali 117 sawa na asilimia 20 ambavyo
vilikua vinatoa huduma ya upasuaji wa dharura nchi ilikua na vituo vya
kutoa huduma ya upasuaji wa uzazi wa dharura na hadi kufikia mwezi
desemba mwaka huu kutakua na vituo vipatavyo 350 sawa na asilimia 50 vya
huduma hiyo vinavyomilikiwa na serikali.
0 on: "HUDUMA ZA AFYA YA MAMA NA MTOTO DAR ES SALAAM YAFIKIA ASILIMIA 80"