Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wa Tatu
kulia akizindua majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi yaliyojengwa kupitia
ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Maralia
(Global Fund) uliofanyika leo jijini Dodoma, wa pili kulia ni Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Kassim Majaliwa wa nne kulia akikata
utepe kuzindua majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi yaliyojengwa kupitia
ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Maralia
(Global Fund) uliofanyika leo jijini Dodoma na wanne kutoka kushoto ni Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kulia akipokea cheti cha umalizaji wa ujenzi wa
majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi kutoka kwa Waziri wa Afya,Maendeleo
ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa majengo
hayo uliofanyika leo jijini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa mwenye suti ya bluu akikagua baadhi ya sehemu za
majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi baada ya kuzindua majengo hayo
yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua
Kikuu na Maralia (Global Fund) yaliyozinduliwa leo jijini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kulia akipata ufafanuzi wa kina kutoka kwa Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa
uzinduzi wa majengo majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi yaliyojengwa
kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na
Maralia (Global Fund) uliofanyika leo jijini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na
wanafunzi wa Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi wakati wa uzinduzi wa majengo ya
Taasisi hiyo yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na
Ukimwi, Kifua Kikuu na Maralia (Global Fund) uliofanyika leo jijini Dodoma, wa
tatu kutoka kushoto ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu.
Baadhi ya viongozi na wananchi wa Mvumi wilayani Chamwino waliojitokeza
kumsikiliza na kushuhudia uzinduzi wa Majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi
yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua
Kikuu na Maralia (Global Fund) uliofanya na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo jijini Dodoma.
NA
WAMJW-DODOMA
SERIKALI itaendelea kutoa kipaumbele
kwenye sekta ya afya hususan swala la
kuajiri wataalam wa kada mbalimbali za afya nchini kwa kuzingatia maeneo yenye
uhaba mkubwa wa watumishi hasa maeneo ya vijijini.
Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa kuzindua majengo
ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa
Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Maralia (Global Fund) uliofanyika
leo jijini Dodoma.
Mhe. Majaliwa aliendelea kusema kuwa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuchukua hatua
mbalimbali katika kutekeleza Malengo Endelevu ya Milenia hususan lengo nambari
tatu linalohusu kuboresha afya za watu pamoja na ustawi wao.
“Miongoni mwa hatua hizo ni
kuhakikisha tunashirikiana na wadau wote ili kuongeza idada ya wataalam wa afya
nchini kwa kuvijengea uwezo wa kimiundombinu vyuo vya elimu ya afya nchini ili
viweze kuongeza udahili na kuzalisha wataalam bora wa afya” alisema Mhe.
Majaliwa.
Aidha, Mhe. Majaliwa aliwataka
wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali za kuongeza idadi ya watumishi wa afya
nchini watakaotekeleza majukumu yao kwa uadilifu na weredi mkubwa kwani Taifa
bora linajengwa na wananchi wenye afya bora na afya bora kwa wananchi
itapatikana iwapo watahudumiwa ipasavyo.
Mbali na hayo Mhe. Majaliwa alisema
kuwa nchi bado inakabiliwa na changamoto
ya magonjwa ya Kifua kikuu na Malaria ,hata hivyo Serikali kwa kushirikiana
na wadau wa sekta ya afya nchini imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za
ugunduzi wa magonjwa hayo kwa kutumia vipimo vya vina saba (gene -expert).
“Tumefanikiwa kusambaza mashine za
“gene expert” 191 kwenye Hospitali zote za Rufaa za Kanda ,Mikoa,Wilaya na
baadhi ya vituo vikubwa vya afya ili kuwezeza kupata majibu ya vipimo vya
utambuzi wa kifua kikuu ndani ya masaa mawili badala ya kipimo cha hadumini
kinachotoa majibu baada ya masaa 24” alisema Mhe. Majaliwa
Aidha , Mhe. Majaliwa amewataka wananchi
kujikinga na maambukizi ya Malaria kwa kuzuia mazalia ya mbu kupitia usafi wa
mazingira wanayoishi na kutumia vyandarua kwa usahihi ili kuunga mkono juhudi
za Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Kwa uapnde Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto mhe. Ummy Mwalimu ametoa shukrani zake kwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kutoa kipaumbele
kikubwa katika masuala ya afya za Watanzania.
“Serikali kupitia Wizara yangu
itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye sekta ya afya yenye
lengo la kuboresha huduma za afya na
vyuo vya kutolea mafunzo ya kada za afya ili kuimarisha afya za
wananchi” alisema waziri Ummy.
Naye Mkurugenzi wa Tume ya Kikristo ya
Huduma za jamii Bw. Peter Maduki amesema kuwa mradi wa ukarabati ,upanuzi na
ujenzi wa majengo mapya pamoja na vifaa tiba na tahama ulioanza April 2015 katika chuo hicho umegharimu shilingi Bilioni
5.2 ikiwa na malengo ya kuongeza uzalishaji wa wataalam wa afya nchini.
0 on: "SERIKALI ITAENDELEA KUTOA KIPAUMBELE KWA WATAALAM WA AFYA"