Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Ijumaa, 23 Machi 2018

AGIZO LA WAZIRI UMMY KWA WAGANGA WAFAWIDHI

- Hakuna maoni




Nawaagiza waganga wafawidhi wote wa hospitali na vituo vya huduma kuhakikisha watoto wote wanaoanza shule za bweni wanafanyiwa uchunguzi wa TB kikamilifu kabla ya  kuanza masomo.

Ameyasema hayo mapema leo katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dodoma wakati akitoa tamko la Kifua Kikuu (TB) mbele ya Waandishi wa habari.

ALIYOYASEMA WAZIRI UMMY KATIKA SIKU YA KIFUA KIKUU (TB) DUNIANI

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (Hawapo kwenye Picha), wakati wa Maazimisho ya siku ya Kifua Kikuu Duniani, tukio limefanyika mapema leo katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dodoma.
 

Kundi la Waandishi wa Habari likifuatilia kwa ukaribu tamko la Kifua Kikuu (TB) lililokuwa lililotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dodoma mapema leo.

Na WAMJW-Dodoma.


TAMKO LA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO UMMY MWALIMU KUELEKEA  MAADHIMISHO YA SIKU YA KIFUA KIKUU DUNIANI MACHI 24 - LEO MJINI DODOMA

# Kifua Kikuu(TB) ni ugonjwa wa kuambukiza unaoongoza kwa kusababisha vifo vingi Duniani.

# Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani(WHO) inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 10.4 huugua Kifua Kikuu kila mwaka Duniani na Milioni Moja kati ya hao ni watoto wenye umri chini ya miaka 15.

# Tafiti nyingi zinaonesha kuwa karibia theluthi moja ya Watanzania tayari wamepata maambukizo ya Kifua Kikuu na wanaishi na vimelea mwilini mwao.

# Kauli mbiu ya mwaka huu inasema *" Viongozi Tuwe Mstari wa Mbele Kuongoza Mapambano ya Kutokomeza TB."*

#Nchini Tanzania kila mwaka jumla ya watu 160,000 wanakadiriwa kuwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu.

# Nitoe wito kwa viongozi wa ngazi zote kuifanya vita dhidi ya TB kuwa agenda muhimu na ya kipaumbele.

# Napenda kuwakumbusha TB inatibika na kupona kabisa, dawa zake zinatolewa bure na zinapatikana sehemu zote nchini katika vituo vya Umma na Binafsi.

# Serikali imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na tatizo la Kifua Kikuu nchini ikiwemo kuimarisha uchunguzi na ugunduzi wa Kifua Kikuu katika Vituo vya Afya.

# Serikali na wadau mbalimbali tunaendelea na utekelezaji wa kampeni za uhamasishaji na upimaji wa Wananchi katika maeneo ya migodi, makazi duni kwenye miji mikubwa, magereza na shule za bweni.

# Pia Serikali imezindua dawa mpya za TB za watoto ili kuhakikisha zinakidhi matakwa ya Shirika la Afya Duniani ( WHO), dawa hizo mpya ni za watoto za mseto ( RHZ/RH) zilizoboreshwa na  tayari zimeshawasili nchini na tumeanza kuzisambaza kwenda Mikoani na Halmashauri zote nchini.

# Nawaagiza waganga wafawidhi wote wa hospitali na vituo vya huduma kuhakikisha watoto wote wanaoanza shule za bweni wanafanyiwa uchunguzi wa TB kikamilifu kabla ya  kuanza masomo.

#Ni marufuku kwa Madaktari  kujaza fomu za uchunguzi wa Afya bila kupima wanafunzi husika. Kufanya hivyo ni kuliangamiza kwa makusudi Taifa  kwa uzembe ambao hauwezi kuvumilika.

# Serikali inatambua umuhimu wa ushirikishwaji wa jamii katika mapambano ya kutokomeza TB.

#Mpaka sasa takribani watoa huduma1530 kati ya 5000 katika ngazi ya jamii ambao wamepata mafunzo ya muda mfupi ya Kifua Kikuu wanawezeshwa ili kuibua wagonjwa wa TB na kuwafuatilia watoto wanaopata matibabu katika maeneo yao.




Jumatano, 21 Machi 2018

MAJUMUHISHO KIKAO MAWAZIRI WA ECSA

- Hakuna maoni



 Mkutano wa 65 wa Jumuiya ya Mawaziri wa Afya wa Nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini ECSA umemalizika leo jijini hapa kwa nchi wanachama kukubaliana maazimio mbali mbali yanayolenga  kutekeleza kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, saratani, magonjwa ya moyo na ya mfumo wa hewa.

Akizungumza wakati wa kufunga mkutano huo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema makubaliano hayo yamelenga kuimarisha na kuboresha sekta hiyo na afya ya wananchi kwa ujumla.

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa  wamekubaliana pia kuongeza uwajibikaji kwenye afya ya mama na mtoto ili kuepusha vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na uzazi.

“Tumekubaliana kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza tumegundua katika nchi hizo magonjwa
yanayoongoza ni pamoja na kisukari, saratani, magonjwa ya moyo na ya mfumo wa hewa" alisema Waziri Ummy.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa Suala lingine walilokubaliana ni kutilia mkazo suala la heshima kwa wajawazito kwa sababu mawaziri wameshauri pia Tanzania kukitambua Chuo cha Upasuaji cha Afrika Mashariki, Kati na Kusini.  

Waziri Ummy ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, amesema wamkubaliana wamekubaliana pia kuimarisha ushirikiano na ulinzi katika maeneo ya mipaka.

DALILI ZA DENGUE HIZI HAPA, MHE. UMMY MWALIMU

- Hakuna maoni



WAZIRI wa Afya, Maendeleo yaJamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu a mewashauri wananchi kwenda vituo vya tiba haraka mara baada ya kugundua kuwa wana dalili za ugonjwa wa dengue.

Hayo ameyasema wakati alipotoa tamko juuya kuingia kwa ugonjwa wa dengue hapa nchini mara baada ya kufunga Mkutano  wa 65 wa Jumuiya ya Mawaziriwa Afya wa Nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini ECSA leo jijini Dar essalaam.

“Kuna dalili za Ugonjwa Dengue zikiwemo homa ya ghafla, kuumwa kichwa hususan sehemu za macho, maumivu ya viungo  na uchovu. Dalili hizi huanza kujitokeza kati ya siku 3 hadi 14 tangu mtu alipoambukizwa virusi vya homa ya Dengue hivyo Wizara inashauri kuwa wananchi wasiwe na hofu, bali mara tu  anapoona dalili za ugonjwa waende katika vituovya tiba" alisema Waziri Ummy.

WAZIRI UMMY AWASHAURI WANANCHI KWENDA VITUO VYA TIBA HARAKA PINDI WANAPOGUNDUA DALILI ZA UGONJWA WA DENGUE.

- Hakuna maoni

NA WAMJW-DAR ES SALAAM


WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewashauri wananchi kwenda vituo vya tiba haraka mara baada ya kugundua kuwa wana dalili za ugonjwa wa dengue.

Hayo ameyasema wakati alipotoa tamko juu ya kuingia kwa ugonjwa wa dengue hapa nchini mara baada ya kufunga Mkutano wa 65 wa Jumuiya ya Mawaziri wa Afya wa Nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini ECSA leo jijini Dar es salaam.

“Kuna dalili za Ugonjwa Dengue zikiwemo homa ya ghafla, kuumwa kichwa hususan sehemu za macho, maumivu ya viungo na uchovu. Dalili hizi huanza kujitokeza kati ya siku 3 hadi 14 tangu mtu alipoambukizwa virusi vya homa ya Dengue hivyo Wizara inashauri kuwa wananchi wasiwe na hofu, bali mara tu wanapoona dalili za ugonjwa waende katika vituo vya tiba alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Wakati mwingine dalili za ugonjwa huu zinaweza kufanana sana na dalili za malaria hivyo basi wananchi wanaaswa kuwa, wakipata homa wahakikishe kuwa wanapima ili kugundua kama wana vimelea vya malaria au Dengue, au sababu nyingine, ili hatua stahiki zichukuliwe.

Waziri Ummy amesema kuwa ili kujikinga na ugonjwa huo ni lazima Kuangamiza mazalio ya mbu kwa kufukia madimbwi ya maji yaliyotuama au nyunyuzia dawa ya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi hayo pamoja na Kujikinga na kuumwa na mbu kwa  kuvaa nguo ndefu muda wote hasa nyakati za mchana.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Wizara itaendelea Kuimarisha ufuatiliaji wa magonjwa nchi nzima kwa kutumia mfumo uliopo wa ukusanyaji wa taarifa (IDSR), ambapo tunaendelea kupata taarifa za kila siku juu ya mwenendo wa ugonjwa huu na Kutoa elimu kwa jamii kupitia vyombo vya habari.

 Mbali na hayo Waziri Ummy amesisitiza kuwa  hakuna vikwazo vyovyote vilivyowekwa kwa ajili ya wasafiri wanaoingia na wanaotoka nchini na  Wizara itaendelea kushirikiana na wadau na sekta mbalimbali katika kufuatilia na kudhibiti ugonjwa huo.

Homa ya Dengue ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoenezwa na mbu wa aina ya Aedes ambao ni weusi wenye madoa madoa meupe yenye kung’aa.








MAWAZIRI WA AFYA WA JUMUIYA YA ECSA WAKUBALIANA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA

- Hakuna maoni

Matukio ya Mkutano wa 65 wa Mawaziri wenye dhamana ya Sekta ya Afya katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Mashariki, kati na kusini mwa Afrika (Eastern, Central and Southern Africa Health Community, ECSA-HC), yanayoendelea jijini Dar es salaam, yakiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, kikao hicho kilifunguliwa juzi machi 19 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitembelea Mabanda ya LAB EQUIP LMTD na Banda la Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi TFDA baada ya mapumziko mafupi ya Mkutano wa 65 wa Mawaziri wenye dhamana ya Sekta ya Afya katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Mashariki, kati na kusini mwa Afrika (Eastern, Central and Southern Africa Health Community, ECSA-HC).




Kikao cha ndani cha Mawaziri wenye dhamana ya Sekta ya Afya katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Mashariki, kati na kusini mwa Afrika (Eastern, Central and Southern Africa Health Community, ECSA-HC), huku wakikubaliana kuimarisha utawala na kuweka mikakati ya pamoja ya kudhibiti na kupambana na magonjwayanayolipuka baina ya nchi hizo, pia kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukiza kama vile magonjwa ya Saratani, ambayo yanasababishwa na aina ya vyakula vyenye mafuta kupita kiasi, matumizi ya vilevi na matumizi ya sigara.
Pia kuongeza uwajibikaji ili kuimarisha Sekta ya Afya hasa katika Afya ya mama na mtoto.




Viongozi wa Serikali kutoka Wizara ya Afya wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto- Idara kuu ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya (Watatu kutoka Kushoto) wakwanza ni Mkurugenzi wa Ubora wa Huduma za Afya Dkt. Mohamed Mohamed, wa pili ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhamed Bakari Kambi na wa mwisho ni Dkt. Kwasi. wakiwa katika hafla ya chakula cha usiku baada ya Mkutano wa 65 wa Mawaziri wenye dhamana ya Sekta ya Afya katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Mashariki, kati na kusini mwa Afrika (Eastern, Central and Southern Africa Health Community, ECSA-HC) uliofanyika katika Hotel ya Kilimanjaro jijini Dar es salaam.

NA WAMJW-DAR ES SALAAM


Mkutano wa 65 wa Jumuiya ya Mawaziri wa Afya wa Nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini ECSA umemalizika leo jijini hapa kwa nchi wanachama kukubaliana maazimio mbali mbali yanayolenga  kutekeleza  kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, saratani, magonjwa ya moyo na ya mfumo wa hewa.

Akizungumza wakati wa kufunga mkutano huo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema makubaliano hayo yamelenga kuimarisha na kuboresha sekta hiyo na afya ya wananchi kwa ujumla.

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa  wamekubaliana pia kuongeza uwajibikaji kwenye afya ya mama na mtoto ili kuepusha vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na uzazi.

“Tumekubaliana kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza tumegundua katika nchi hizo magonjwa yanayoongoza ni pamoja na kisukari, saratani, magonjwa ya moyo na ya mfumo wa hewa" alisema Waziri Ummy.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa Suala lingine walilokubaliana ni kutilia mkazo suala la heshima kwa wajawazito kwa sababu mawaziri wameshauri pia Tanzania kukitambua Chuo cha Upasuaji cha Afrika Mashariki, Kati na Kusini.  

Waziri Ummy ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, amesema wamkubaliana wamekubaliana pia kuimarisha ushirikiano na ulinzi katika maeneo ya mipaka.

“Kwa sababu nchi zina mipaka lakini magonjwa hayana mipaka tukiimarisha itasaidia kuondoa na kudhibiti uwezekano wa magonjwa hasa ya mlipuko kuenea ikiwemo Zika, Ebola, Dengue, Chikungunya na mengineyo,” alisema Waziri Ummy.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Ummy  amesema pia wamekubaliana kuimarisha masuala ya utawala kwamba kila mmoja ana wajibu kwa nafasi yake kwani sekta ya afya ni mtambuka.

“Tumeona kuna umuhimu mkubwa wa kushirikisha sekta zingine ikiwamo kilimo, maji, elimu, utumishi, mazingira zinahusika kwa ukaribu na masuala ya Afya” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa azimio la saba walilokubaliana katika mkutano huo ni kuweka mkakati wa pamoja kukabiliana na magonjwa akitolea mfano nchi ya Uganda ambao wamepata ugonjwa wa Marbugy unaofanana dalili na ugonjwa wa Ebola.


Mkutano huo wa kujadili masuala mbalimbali ya afya yalijumuisha nchi 9 kutoka  Nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini ECSA umefanyika nchini Tanzania kwa siku tatu.