Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi akisema jambo kwa watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando (hawapo pichani)
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi (wa upande wa kulia) akipokea zawadi za kwaheri kutoka kwa watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa - Bugando alipokuw akifanya kazi awali kabla ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kuwa Mganga Mkuu wa Serikali.
Mganga
Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi (wa upande wa kushoto) akipokea zawadi
za kwaheri kutoka kwa watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa -
Bugando alipokuw akifanya kazi awali kabla ya kuteuliwa na Rais wa
Jamhuri ya Muugano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kuwa Mganga
Mkuu wa Serikali.
Na WAMJW – Mwanza
Vituo vya kutolea huduma za afya nchini
vyatakiwa kufanya uchunguzi juu ya kifo chochote kitakachotokana na ugonjwa wa
corona ili kubaini kama mgonjwa alihudumiwa ipasavyo kabla ya kifo kutokea.
Agizo hilo limetolewa na Mganga Mkuu
wa Serikali Prof. Abel Makubi akiwa Jijini Mwanza mara baada ya kuagana na
uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa – Bugando alipokuwa akifanya
kazi awali kama Mkurugenzi Mtendaji kabla ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mganga Mkuu wa
Serikali.
“Kwakweli tusingependa kuona mgonjwa anafariki kwa
sababu zisizo na msingi, naagiza hospitali zote zenye kamati ya uchunguzi (Clinical
Audit) kufanya uchunguzi wa vifo vinavyohusiana au kutokana na corona ili kuona
kama kulikuwa na tatizo lolote katika kumpokea mgonjwa au katika kumhudumia” alisema
Prof. Makubi
Prof. Makubi amewataka wananchi
kuelewa kuwa sio kila kifo kinachotokea hivi sasa kinasababishwa na ugonjwa wa
corona kwa kuwa yapo magonjwa mengine pia ambayo yanatushamblia binadamu.
“Siyo kweli kwamba mgonjwa akiwa na
presha, kisukari, figo au kansa akifariki iwe imesababishwa na corona,
tuendelee kuwahudumia wananchi, kuepusha vifo vinavyoweza kuwa na uhusiano wa
corona”. Alisema Prof. Makubi.
Aidha Prof. Makubi ametoa rai kwa
vituo vya afya kuwapokea wagonjwa wote na kuwapatia matibabu bila kuwabagua
kuwa na dalili za corona.
“Serikali inapenda kuona wagonjwa wa
corona wanapokelewa nakupata matibabu, tuendelee kuwapokea na kuwahudumia huku
tukichukua tahadhari ya maambukizi”. Alisema Prof. Makubi.
“Watumishi wa afya wasiwe na ubaguzi
wa kuchagua wagonjwa wa kuwahudumia au mpaka apimwe kipimo cha covid-19 ndio
ahudumiwe, tuwapokee wote lakini wakati huo tukichukua tahadhari zote za
kujikinga na ugonjwa”. Alisisitiza Prof.
Makubi.
Katika hatua nyingine Prof. Makubi
amesema kuwa Serikali inaendelae kusambaza vifaa kinga kwa ajili ya kuwawezesha
watoa huduma kujikinga na ugonjwa huo wakati wakitoa huduma.
“Serikali imeanza kugawa vifaa kinga
kama vile PPE, masks pia sanitizer kwa ajili ya vituo vyote vya afya Tanzania,
kwahiyo pasIwepo kisingizio chochote cha kushindwa kumhudumia mgonjwa wa corona
kwa sababu ya vifaa kinga”.
Mwisho
0 on: "VIFO VYA CORONA KUCHUNGUZWA"