Na
Mwandishi Maalum – Pwani
20/05/2020
Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Mpango wa
Taifa wa Chanjo imejipanga kuwafikia walengwa wote waliostahili kupata chanjo
na kuhakikisha kiwango kinabaki vilevile kama ilivyotarajiwa.
Hayo
yamesemwa leo na Ofisa Mradi kutoka Mpango huo Lotalis Gadau wakati wa
usimamizi elekezi wa kukagua utoaji huduma za chanjo katika Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na Engender Health kupitia
Merck Sharp& Dohme B.V (MSD).
Gadau
alisema kuwa katika kipindi hiki cha nchi kukabiliana na Ugonjwa wa Corona,
Wizara imejipanga kuhakikisha watoa huduma wa afya wanaendelea kutoa huduma za
chanjo kwa watoto wadogo pamoja na wasichana ambao walikua wapate chanjo ya
kujikinga na saratani ya mlango wa kizazi(HPV).
“Kama
Wizara tumejipanga vizuri kwa kuhakikisha chanjo zote zinakuwepo kwa wakati
kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na kuhakikisha watoto wote waliokuwa
wanatarajia kupata chanjo wanapata,na watoa huduma wanachukua tahadhari zote za
kujikinga na ugonjwa huu”,
Alisema
walikuwa wakisikia wananchi wana wasiwasi kufika kwenye vituo vya kutolea
huduma,“tumepita kwenye vituo vya afya kwenye mkoa huu na tumeona hali ni zuri
kwani wazazi na mabinti wengi wanakuja kwenye vituo na tumewasisitiza kila
mmoja anayeenda awe balozi anaporudi nyumbani kuhakikisha wataambiana ili kila
anayestahili kupata chanjo anaenda kwenye kituo cha afya chochote cha jirani
aweze kupata chanjo”.
Vile
vile alisema kuhusu mabinti ambao walikua wapate chanjo ya kuzuia saratani ya malango wa kizazi tofauti na awali ambapo walikua wakifuatwa
mashuleni ila kutokana na janga la
Corona inasisitizwa wafike kwenye vituo
cha kutolea huduma za afya vya karibu
waweze kupata chanjo hiyo.
Upande wa watoto wadogo, Bi. Gadau amesema
hivi sasa umewekwa utaratibu kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka miwili
ambao wanastahili kupatiwa chanjo wao wanatakiwa kupata chanjo kama ilivyo
kawaida”Kwa kipindi hiki watoto ambao wamekamilisha ratiba ya chanjo na
wanafika kituoni kwa ajili ya uzito tu wao wanatakiwa waende kila baada ya
miezi mitatu hii ni kuepuka misongamano na tunasisitiza elimu ya afya ambayo
ilikua ikitolewa kwa muda mrefu au kusubiriana kwa sasa itatolewa kwa muda mfupi usiopungua dakika
tano lakini endapo mtoto atapata homa au tatizo lolote anatakiwa kupekekwa
kwenye kituo cha afya kwa ajili ya matitabu.
Naye
Mratibu Huduma za Chanjo kwa Mkoa wa Pwani Abbas Hincha amesema kuwa asilimia
90 ya walengwa wa chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi kwa mabinti wenye umri
wa miaka 14 ambao hapo awali walikuwa wakipatiwa wakiwa shuleni ila kutokana na
janga hili wanashirikia na walimu wa shule zao kwani walikua wameandikishwa
hivyo wanawapatia namba za simu na kuwapigia wazazi na walezi ili kuwapeleka
kupatiwa chanjo hiyo.
Alisema
katika mkoa wake wamepanga mikakati mbalimbali ikiwemo ya kuwashirikisha watoa huduma ngazi ya jamii kuwatafuta
mabinti hao kwenye maeneo yao na kuwakumbusha kwenda kupata chanjo.
Alisema
muamko kwa chanjo kwa upande wa watoto wadogo unaendelea vizuri na kuna muitikio
mzuri hivyo wanaendela kutoa elimu jinsi ya kujikinga na Corona na kwenye vituo
ambavyo havina nafasi kubwa wanatoa huduma hizo nje ya kituo ili kuzingatia
umbali wa mita moja kati ya mtu na mtu
0 on: "SERIKALI INAHAKIKISHA WALENGWA WOTE WA CHANJO WANAFIKIWA KATIKA KIPINDI CHA CORONA"