Bi. Ipyana
Mwamwala Muuguzi Mkunga wa Kituo cha Afya Mtego wa Simba akimpima uzito mtoto
Niran Daudi (7) pembeni ni mama wa mtoto huyo, Bi. Joyce Mwantobe. Picha na
Englibert Kayombo
Bi. Elinivoniia Mchomvu Muunguzi Mkunga akisoma kitabu cha afya ya mtoto kabla ya kutoa chanjo katika Zahanati ya Fulwe, Wilaya ya Morogoro VIjijini. Picha na Englibert Kayombo
Bi. Elinivoniia Mchomvu Muunguzi Mkunga akisoma kitabu cha afya ya mtoto kabla ya kutoa chanjo katika Zahanati ya Fulwe, Wilaya ya Morogoro VIjijini. Picha na Englibert Kayombo
Ofisa Afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Lugata akitoa elimu kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Corona.kwa wananchi waliofika katika Kituo cha Afya Mtego wa Simba Wilaya ya Morogoro Vijijini kupata huduma za afya
Ofisa Miradi kutoka Mpango wa Taifa wa Chanjo, unaosimamiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Furaha Kyesi (kushoto) akimzungumza jambo na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mtego wa Simba, Luambano Ally
Wananchi wakiingia katika Kituo cha Afya Mtego wa Simba kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa kukabiliana na Ugonjwa wa Corona kwa kunawa mikono kwa maji yanayoririka na sabuni na kukaa umbali wa zaidi ya mita moja kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine
Mwandishi
Maalum - Morogoro
Huduma ya chanjo za mkoba hasa
katika maeneo ya pembezoni (vijijini) zinapaswa kuendelea kutolewa kwa watoto
chini ya miaka mitano ili kuhakikisha wote wanafikiwa kwa wakati unaopaswa,
licha ya kuwapo kwa janga la Corona.
Pamoja
na kundi hilo, kundi jingine linalopaswa kufikiwa na kupatiwa chanjo ya ni
wasichana wenye umri wa miaka 14 ambao wanapaswa kupatiwa ile ya HPV inayokinga
dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo vinavyosabisha ugonjwa wa saratani ya
kizazi.
Rai
hiyo imetolewa jana na Ofisa Miradi kutoka Mpango wa Taifa wa Chanjo wa Wizara
hiyo, Dk. Furaha Kyesi alipozungumza na uongozi wa Kituo cha Afya Mtego wa
Simba, kilichopo Wilaya ya Morogoro Vijijini, mkoani Morogoro wakati wa ziara
ya ukaguzi wa huduma za chanjo zinazotolewa kwenye vituo vya afya kipindi hiki
cha mapambano dhidi ya janga la Corona.
Timu
ya ufuatiliaji huduma za chanjo kutoka Mpango wa Taifa wa Chanjo (IVD) wa
Wizara hiyo, maofisa chanjo wa Mkoa wa Morogoro na wa Wilaya hiyo kwa
kushirikiana na Shirika la Engeder Health kupitia Merck Sharp & Dohme B.V
(MSD), wapo mkoani humo kukagua namna huduma za chanjo zinavyoendelea kutolewa
katika kipindi hiki cha janga la Corona.
“Kundi
hili la wasichana lazima tuhakikishe tunalifikia, kwa sababu hawa awali
msisitizo ulikuwa kuwapa chanjo kwa kuwafikia shuleni, lakini sasa shule
zimefungwa kutokana na janga la Corona, lakini tunahitaji kuwafikia.
“Watoto
chini ya miaka mitano nao lazima tuwafikie ili kwamba wakati tunapambana na
Corona tuhakikishe pia tunaendelea kuwapa chanjo dhidi ya magonjwa mengine kama
vile surua, polio, kuharisha na mengineyo, ili tusije tukapata mlipuko wa
magonjwa,” amesema.
Kyesi
ameshauri kwamba watoa huduma za afya waendelee kuzingatia mwongozo wa
kujikinga na kufikia maeneo ya pembezoni hasa huko vijijini kuwapa huduma.
Awali
akizungumza, Muuguzi Mkunga wa Kituo hicho, Ipyana Mwamwala alisema kila mwezi
hupokea watoto wapatao saba na kuwapa chanjo mbalimbali kulingana na umri wao.
Amesema
kituo hicho kimezungukwa na vijiji vinne ambavyo ni Sangasanga, New Land, Mkono
wa Mara, Mkambarani na Mtego wa Simba (chenyewe).
“Wakina
mama bado wana mwamko wa kuleta watoto kituoni lakini tunahitaji kwenda
outreach kwa ajili ya kuwafikia pia wale ambao hawaji kituoni, vijiji vipo
mbali na hapa,” amesema.
Ameongeza
“Tupo tayari kwenda, tunatambua, tumetangaziwa kuna ugonjwa wa COVID -19 nchini
ambao unatokana na maambukizi ya virusi vya Corona, hata hapa kituoni
tumechukua hatua na hata tukienda kule tutazingatia kanuni zote za kujikinga
sisi wenyewe na wale tunaokwenda kuwahudumia wasipate maambukizi.
Mganga
Mfawidhi wa Kituo hicho, Luambano Ally amesema kutokana na taarifa hiyo ya
tahadhari iliyotolewa na Wizara ya Afya, walilazimika kuchukua hatua za
kuimarisha kujikinga ikiwamo kuweka ndoo za maji katika maeneo ya kuingia ndani
ya kituo hicho.
“Kwenye
milango yote ya kuingia ndani ya kituo kuna ndoo ya maji safi tiririka na
sabuni lazima mtu anawe ndipo aingie huku ndani, lakini kama amejisahau kunawa
pale au anahitaji tena kunawa akiwa humu ndani, kuna ndoo nyingine tumeweka
ataweza kunawa pia.
“Hapa
kituoni tumewapa taarifa kwamba kila anayekuja kupata huduma lazima avae
barakoa, utaona hilo wanakijiji wanalitii na wamekuwa na mwamko, wanakuja
wakiwa wamevaa, wananawa mikono, wanapata huduma na kurudi zao nyumbani,”
amesema Ally.
MWISHO
0 on: "WAHIMIZWA KUJIPANGA, KUENDELEA KUTOA HUDUMA ZA MKOBA ZA CHANJO"