Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel akisisitiza jambo wakati akiongea na Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (hawapo kwenye picha).
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel akiteta jambo na Mkurugenzi wa tiba Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe, wakati alipofanya ziara ya kuongea na Watumishi wa Sekta ya Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Mkurugenzi wa tiba Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe akiteta jambo na Mkururugenzi msaidizi anaesimamia hospitali za Rufaa Dkt. Caroline, wakati alipofanya
ziara ya kuongea na Watumishi wa Sekta ya Afya katika Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Baadhi ya Watumishi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakifuatilia neno kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel pindi alipofanya ziara katika Hospitali hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel akimjulia hali mtoto aliefika na mzazi wake kupata matibabu katika wodi ya watoto, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel akiwa na baadhi ya Watumishi kutoka Wizara ya Afya, katika chumba cha Watoto njiti, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel akimjulia hali mama aliyempeleka mtoto kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel akiwa na viongozi kutoka Wizara ya Afya na Watumishi wa Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma pindi alipofanya ziara ya kuongea na Watumishi hao.
Jengo la Idara ya magonjwa ya wanawake na uzazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
HONGERENI WATUMISHI WOTE WA AFYA KWA
JINSI MLIVYO PAMBANA KATIKA JANGA LA CORONA.
Na WAMJW- DOM
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel amewashukuru Watumishi wote
wa Sekta ya Afya nchini kwa namna walivyojitoa katika mapambano dhidi ya
maambukizi ya virusi vya Corona.
Dkt. Mollel ameyasema hayo leo,
wakati alipofanya ziara ya kuongea na Watumishi wa Sekta ya Afya katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na Hospitali ya Rufaa ya kanda ya kati ya
Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.
"Jinsi ambavyo nyie mmepambana
dhidi ya virusi vya Corona na bado mkamuunga mkono Mhe. Rais na ushauri
alioutoa yeye na Wataalamu wengine wa Wizara kupitia
Waziri wa Afya,
nyie mmekuwa mashujaa na jeshi la uzalendo wa hali ya juu, nawashukuru sana"
alisema Dkt. Mollel.
Dkt. Mollel aliendelea kwa kukemea
tabia za wanasiasa wachache kupotosha Watanzania na Dunia kwa ujumla juu
ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa Corona kwa Watumishi wa Sekta ya Afya nchini
jambo ambalo sio kweli.
"Kuna wanasiasa wanapiga kelele kuhusu
Corona kuliko sisi, nawaomba watu tuache kupiga siasa, sisi
watumishi wa afya ndio watu wakwanza kukutana na wagonjwa wa Corona laikini leo
watumishi mpo 504 je niambieni kuna yoyote amelazwa, watumishi walijibu hapana,
kama kweli kuna
Watumishi wanakufa basi nyie mngekuwa wa kwanza kuugua na kupoteza
maisha"
alisema.
Aidha, Dkt Mollel alitoa wito kwa
Watumishi wa Sekta ya Afya nchini kufanya kazi kwa bidii katika kuwahudumia
wananchi ili kutoa huduma bora, huku akiweka wazi kuwa kazi ya kuwahudumia
wananchi ni ya wito na ya uzalendo.
Pia, Mhe
Mollel alielezea kuwa Rais alikuwa na maono ya kusitisha matibabu ya nje ya
nchi kwa kuboresha huduma za kibingwa nchi na hii imejizihirisha baada ya dunia
kupata janga la corona nchi yetu imeendelea kutoa huduma za kibingwa pasipo
kutegemea matibabu ya nje kwa wananchi ambao walikuwa na sifa za kutibiwa nje .
Nae Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Ibenzi Ernest ameweka wazi kuwa Hospitali hiyo
imeendelea kutoa huduma za Afya bila kutetereka na kutoa elimu kwa umma licha
ya kupitia katika kipindi cha mlipuko wa virusi vya Corona ulioikumba nchi.
"Tumeendelea kutoa huduma bora
kwa wananchi bila kutetereka hata katika wakati huu wa janga la mlipuko wa
maambukizi ya virusi vya Corona ulioikumba nchi, Watumishi wetu wamesimama
imara huku wakiendelea kutoa elimu ya kujikinga dhidi ya Corona "alisema.
0 on: "HONGERENI WATUMISHI WOTE WA AFYA KWA JINSI MLIVYO PAMBANA KATIKA JANGA LA CORONA. "