Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 13 Desemba 2017

TAARIFA YA MWEZI NOVEMBA KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO


TAARIFA YA MWEZI NOVEMBA KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI ILIYOTOLEWA NA MHE. UMMY MWALIMU (MB); WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, TAREHE 13 DISEMBA 2017

Ndugu wanahabari,
Huu ni mwendelezo wa taarifa za kila mwezi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuhusu mwenendo wa mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu nchini ikiwa taarifa hii ni ya mwezi Novemba 2017. Aidha taarifa hii inaendelea kutoa maelekezo ya hatua zinazotakiwa kuchukuliwa katika kudhibiti ugonjwa huu nchini.

Ndugu Wanahabari,
Kwa kipindi cha kuanzia tarehe 01 hadi 30 Novemba 2017, jumla ya wagonjwa walioripotiwa walikuwa ni 462 na vifo 15. Jumla ya Mikoa 10 na Halmashauri 17 zimeripoti wagonjwa wa Kipindupindu kwa mwezi Novemba. Mikoa iliyoripoti wagonjwa wa Kipindupindu ni Dar es salaam (14 na kifo 1), Dodoma (20 bila kifo), Tanga (5 bila kifo), Ruvuma (73 na vifo 8), Morogoro (5 bila kifo), Rukwa (7 na kifo 1), Manyara (13 na kifo 1), Songwe (80 bila kifo), Mbeya (119 bila kifo), Kigoma (126 na kifo1). Halmashauri zilizoripoti wagonjwa wa Kipindupindu ni Kinondoni (8 bila kifo), Ubungo (6 na kifo1), Mpwapwa (5 bila kifo), Chamwino (12 bila kifo) na Bahi (3 bila kifo), Mkinga  5 bila kifo), Nyasa (73 na Vifo 8), Kilosa (5 bila kifo), Sumbawanga Vijijini (7 na kifo1), Kiteto (13 na kifo1), Songwe Vijijini (80 bila kifo), Mbeya Vijijini (25 bila kifo), Mbeya Mjini (26 bila kifo), Chunya (10 bila kifo), Kyela (58 bila kifo) na Kigoma vijijini (10 bila kifo), Uvinza (116 na kifo 1)



Ndugu Wanahabari,
Takwimu zinatuonesha bado maambukizi mapya ni tishio kwani kuna ongezeko la idadi ya Mikoa na Halmashauri zinazotoa taarifa za wagonjwa ikilinganishwa na mwezi uliopita japokuwa idadi ya wagonjwa imepungua. Mwezi wa Oktoba tulikuwa na jumla ya wagonjwa 570 ikilinganishwa na mwezi huu ambapo tuna jumla ya wagonjwa 462. Jumla ya Mikoa 6 na Halmashauri 11 ziliripoti wagonjwa wa Kipindupindu mwezi uliopita ukilinganisha na jumla ya Mikoa 10 na Halmashauri 17 zilizoripoti wagonjwa mwezi huu.
Pia takwimu za kipindupindu nchini kwa mikoa za tangu mwaka huu uanze zinaonyesha ongezeko za ugonjwa huu, Aidha kwa kipindi cha Januari hadi Novemba, 2017, jumla ya mikoa 17 ilitoa taarifa za wagonjwa wa Kipindupindu, ikiwa na jumla wa wagonjwa 3,839 na vifo 71 (Kama jedwali linalofuata linavyoenesha). Mikoa saba (7) haikuripoti kuwepo kwa ugonjwa huu, mikoa hii ni pamoja na Mwanza, Shinyanga, Arusha, Lindi, Kagera, Simiyu, Kilimanjaro na Mtwara.
Na.
Mkoa
Januari hadi Septemba, 2017
Octoba,2017
Novemba,2017
Jumla(Januari hadi Novemba,2017)
Wagonjwa
Vifo
Wagonjwa
Vifo
Wagonjwa
Vifo
Wagonjwa
Vifo
1
Mbeya
591
7
0
4
119
3
710
14
2
Morogoro
308
11
7
0
5
0
320
11
3
Dar es Salaam
306
4
0
0
14
1
320
5
4
Iringa
274
8
58
1
0
0
332
9
5
Dodoma
216
3
14
1
20
0
250
4
6
Kigoma
188
3
0
0
126
1
314
4
7
Katavi
133
1
0
0
0
0
133
1
8
Tanga
117
2
6
1
5
0
128
3
9
Mara
110
0
0
0
0
0
110
0
10
Pwani
83
1
0
0
0
0
83
1
11
Manyara
0
0
0
0
13
1
13
1
12
Songwe
82
0
376
4
80
0
538
4
13
Singida
58
0
0
0
73
8
131
8
14
Rukwa
46
1
0
0
7
1
53
2
15
Ruvuma
0
0
0
0
0
0
0
0
16
Njombe
10
0
0
0
0
0
10
0
17
Tabora
7
1
0
0
0
0
7
1
Jumla
2816
45
461
11
462
15
3739
71


Ndugu Wanahabari,
Nchi yetu inaelekea katika majira ya mvua ambazo zinaweza kuongeza kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa Kipindupindu, hivyo tunahitaji kuzidisha juhudi za kuzuia ugonjwa huu, kwa kusimamia kikamilifu maelekezo na miongozo stahiki inayotolewa.  Aidha, Wizara inaendelea kuwasihi wananchi kuungana na Halmashauri, Mikoa pamoja na Wizara katika juhudi za kupambana na kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu. Jamii izingatie kanuni za usafi binafsi na usafi wa mazingira, ikiwa ni pamoja na:
1.    Kujenga na kutumia vyoo bora katika maeneo tunamoishi.
2.    Kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni kabla ya kula, baada ya kutumia choo, na baada ya kumsafisha mtoto aliyejisaidia.
3.    Mamlaka za maji zilizopo nchini zihakikishe upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi.
4.    Kunywa maji safi na salama yaliyotakaswa kwa dawa (kama vile water guard) au yaliyochemshwa na kupoa.
5.    Kuzingatia ushauri na elimu sahihi kuhusu ugonjwa wa kipindupindu, ili jamii iondokane na imani potofu kuhusu kipindupindu.
6.    Viongozi wa dini, watu mashuhuri na waganga wa tiba mbadala wasaidie kuhamasisha jamii zao kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huu.
7.    Kutoa huduma ya kwanza katika ngazi ya jamii kwa mgonjwa yeyote mwenye dalili za kipindupindu kwa kumpatia ORS.
8.    Endapo ORS itakuwa haipatikani hasa nyumbani, unaweza kutumia maji yaliyochanganywa na chumvi na sukari. Maji haya huweza kuandaliwa kwa kuchanganya maji safi yaliyochemshwa kiasi cha lita moja na vijiko viwili vya sukari na nusu kijiko ya chumvi.
9.    Kufikisha wagonjwa wa Kipindupindu mapema katika vituo vya kutolea huduma ili wawahi kupata matibabu.

Ndugu Wanahabari,
Ni dhahiri kuwa ushirikishwaji wa sekta zote kwa ngazi zote hadi katika jamii ni muhimu sana katika kukabiliana na ugonjwa wa Kipindupindu. Wizara inasisitiza kuwa wadau wote wapewe nafasi katika mapambano haya kupitia vikao mbalimbali ili kujadili udhibiti wa ugonjwa wa Kipindupindu kwenye halmashauri na mikoa. Viongozi wa dini, watu mashuhuri na waganga wa tiba mbadala pia wasaidie kuhamasisha jamii zao kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huu.

Ndugu Wanahabari,
Changamoto moja wapo katika kudhibiti ugonjwa wa Kipindupindu ni upatikanaji wa maji safi na salama. Wizara inaendelea kusisitiza yafuatayo yasimamiwe kwenye Halmashauri na Mikoa yote nchini.
  1. Kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yote mijini na vijijini hasa wakati wa mlipuko wa Kipindupindu. Hii ni pamoja na:
o   Mamlaka za maji katika ngazi zote ziweke mkazo wa kuwepo kwa vyanzo mbadala vya maji.
o   Utakasaji wa maji ya bomba kwa njia ya kutumia klorini ufanyike kama miongozo inavyotaka na ufuatiliaji wa ubora wa maji ufanyike kulingana na miongozo.
  1. Utoaji wa taarifa sahihi na kwa wakati, za ugonjwa wa Kipindupindu kwa kufuata miongozo iliyopo.
  2. Kuongeza uwajibikaji wa viongozi na watendaji (Leadership and accountability): Usimamizi wa utekelezaji wa miongozo katika kuzuia na kudhibiti ugonjwa huu ni muhimu kwa viongozi na wanaowasimawa. Hii ni pamoja na;
o   Usimamizi wa utekelezaji wa sheria ndogondodo za usafi wa mazingira ili kuimarisha matumizi ya vyoo.
o   Usafi wa mazingira pamoja na udhibiti wa biashara za chakula na pombe za kienyeji katika mitaa.
o   Kuzingatia agizo la Mheshimiwa Rais la kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.
  1. Kuihusisha jamii katika ngazi za chini kabisa (serikali ya kijiji/mtaa) kuongoza mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kipindupindu katika maeneo yao kwa kusimamiana wenyewe katiaka makundi madogo madogo yenye kaya 10 hadi 20 kufanikisha utekelezaji wa maelekezo yote yaliyotolewa na wataalamu wa afya. Maelekezo hayo ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa kaya ambazo hazitibu maji ya kunywa, hazijajenga na hazitumii choo, wanajamii wanaochafua vyanzo vya maji na kaya au wanajamii ambao bado wanaendesha kwa siri biashara za vinywaji au chakuka zilizosimamishwa.

Ndugu Wanahabari,
Hivi karibuni Makamu wa Raisi alizindua awamu ya pili ya kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira yenye kaulimbiu, “Usichukulie Poa Nyumba ni Choo”. Napenda kuchukua nafasi hii kuhimiza ujenzi wa vyoo bora kwa kila kaya ili kuweka safi mazingira yetu hasa ikizingatiwa kuwa ni asilimia 40 tu ya kaya hapa nchini zina vyoo bora.
Aidha, Wizara yangu imekuwa karibu na Mikoa na Halmashauri katika kudhibiti ugonjwa huu kwa kufanya yafuatayo:
o   Kutuma timu za wataalamu kwenda kwenye maeneo yaliyoathirika kushirikiana na Mikoa na Halmashauri katika kudhibiti ugonjwa huu
o   Kupima vipimo vya maabara na kubaini aina ya vimelea vinavyosababisha ugonjwa pamoja na kupima usikivu wa dawa inayofaa kutibu wagonjwa katika mlipuko huu
o   Kupeleka Vifaa tiba na dawa katika Mikoa na Halmashauri zilizoathirika kupitia kanda ya bohari ya Dawa (MSD)
o   Kusambaza dawa ya kutibu maji majumbani katika Mikoa na Halmashauri zilizoathirika

HITIMISHO
Ninatambua kuwa zimekuwepo jitihada mbalimbali, na ninawashukuru na kuwapongeza wote wanaoendelea kupambana na ugonjwa huu. Aidha, ninaendelea kuwashukuru wataalam wa sekta husika, mashirika ya kimataifa, watumishi, mikoa, halmashauri pamoja na waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla kwa kuendelea kushirikiana katika suala zima la kudhibiti ugonjwa wa Kipindupindu.



Asanteni sana

Jumanne, 12 Desemba 2017

MADEREVA WAANZA KUTII SHERIA ZA BARABARANI BILA SHURUTI

- Hakuna maoni
Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu aliyesimama akiongea na wadau mbalimbali wa usalama barabarani  hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.

Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Bi. Mary Kessy akiongea na wadau mbalimbali wa usalama barabarani  hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.

ASP Deus Sokoni wa kwanza kulia akiongea na wadau mbalimbali wa usalama barabarani  hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Wizara ya Mambo ya Ndani  Bi. Marlin Komba  anayefuata ni Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu.

Katibu Mkuu wa Shirikishi wa vyama vya Walemu nchini Bw. Felicina Mkude aliyesimama akiongea na baadhi ya wadau mbalimbali wa usalama barabarani  hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.

Baadhi  ya wadau mbalimbali wa usalama barabarani  wakimsikiliza kwa makini Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu hayupo pichani  wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.



Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu katikati ya waliokaa akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa usalama barabarani  wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.



Na.WAMJW-Dodoma     
Madereva nchini wamepongezwa   kwa kuanza kubadilika na kutii sheria bila shuruti katika kukabiliana na ajali za barabarani na hivyo kupungua kwa ajali pamoja na vifo vitokanavyo na ajali kwa uendeshaji unaofuata taratibu na sheria za barabarani.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kikosi cha Barabarani Tanzania  Fortunatus Musilimu -Kamishana Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP) wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa kupokea maoni ya sheria kuhusu ajali za barabarani  unaojumlisha mashirika yasiyo ya Kiserikali.
Kamanda Musilimu alisema tatizo la ajali barabarani bado ni kubwa kwani watu wengi wanafariki na kujeruhiwa kutokana na ajali barabarani.
”sisi sote  ni wahanga wa usalama barabarani hivyo hatuna budi  wadau wote kushirikiana katika kukabiliana na suala hili  na kila mmoja anayo nafasi ya kuchangia ili usalama wa barabarani uimarike  na kuboreka zaidi”Alisema.
Alisema hivi sasa watu wengi wameanza kubadilika hususani madereva wengi ambapo kuna wakati inabidi jeshi la polisi kutumia nguvu nyingi ili kuweza kuepuka ajali zinazoweza kuepukika na nguvu hizi zimetumika kwa nia nzuri ili watanzania kuwa salama wanapotumia vyombo vya moto.
Akitolea mfano kwa hali ya usalama barabarani kwa siku ya jana (juzi) nchi nzima kulikua na ajali nne ambazo zimesababisha vifi viwili na majeruhi nne,hivyo ni hatua nzuri na hata hivyo aliwataka wadau hao kuhakikisha wanatoa maoni mazuri ambayo yatasaidia kupata sheria ambayo haitamkandamiza mwananchi na ambayo itakua salama na kupunguza ajali za barabarani nchini na kuwa na sheria inayotekelezeka kwa kupunguza ajali kwa asilimia 50.

“Serikali ya awamu ya tano inapenda kulinda maisha ya watanzania,serikali inatengeneza uchumi wa kati  na viwanda kwa kuboresha miundombinu ikiwemo barabasha hivyo jukumu letu kushirikiana na serikali kuilinda  miundombinu yote inayotengenezwa”
Aidha,Kamanda Musilimu aliwataka wananchi waondoe dhana kwamba ajali zinatokana na mapenzi ya Mungu, “Hii siyo kweli ila matatizo yote ya ajali ni sisi wenyewe tunasababisha kutokana na mwendo kasi na kutotii sheria za barabarani".
Alitaja takwimu za ajali barabarani kwa Tanzania kwa mwezi Julai hadi Septemba mwaka 2016 ilikua 639,vifo 923 na majeruhi 2,469 na kwa mwaka 2017 kuanzia Julai hadi Septemba ajali za barabarani zilikuwa 1,376,vifo 655 pamoja na majeruhi 1,469.
Naye  Mwakilishi toka shirika la Afya Dunia  Mery Kessy alisema zaidi ya asilimia 90 za ajali zinazotokea katika nchi zinazoendelea ingawa ni asilimia 10 tu nchi hizo  zinamiliki vyombo vya moto na hiyo ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo miundombinu,mazingira pamoja na tabia.
Alisema wahanga wakubwa wanaopata ajali na vifo ni  vijana kati ya miaka miaka 15 mpaka 29 kwani umri huu wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kusababisha ajali na hivyo ajali hizo kuchukua zaidi ya asilimia 3 za pato la Taifa kwani serikali inaingia gharama kubwa kutibu majeruhi katika sekta ya afya.


Jumatatu, 11 Desemba 2017

MH. UMMY(MB) AWEKA HISTORIA KATIKA ZIARA YA ZAHANATI YA MHANDU KATA YA CHELA WILAYANI MSALALA.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akimsalimia  mgonjwa aliyekuwa anasubiri huduma katika Zahanati ya Segese wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa  malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.

Baadhi ya Wanakijiji wa Kijiji cha Segese wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa  malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikagua choo cha Zahanati ya Mhandu wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa  malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi , aliyevaa suti nyeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama Bw. Fadhil Mkuru.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akisisitiza jambo kuhusu upatikanaji wa dawa katika  Zahanati ya Mhandu wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa  malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.

 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akifurahia jambo na baadhi ya  wazee wa kijiji cha Segese wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa  malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akimkabidhi kitambulisho cha matibabu bila ya malipo mmoja wa wazee wa kijiji cha Segese Bibi. Shija Petro (60) kulia  wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa  malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi, Bibi huyo aliwawakilisha wazee 413 waliopata vitambulisho hivyo katika Halmashauri ya Msalala ambapo lengo  ni kuwafikia wazee742 kufikia Machi 2018.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati  akiangalia  friji la kuhifadhia chanjo kwa  ajili ya watoto  katika Zahanati ya Segese wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa  malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akipata maelekezo juu ya upatikanaji wa dawa kutoka kwa mtoa huduma kushoto  katika Zahanati ya Segese wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa  malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.



Na WAMJW-MSALALA

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto aweka historia kwa kutembelea Zahanati ya Mhandu kata  ya Chela Wilayani Msalala ambapo tangu Uhuru wa Tanzania kijiji hicho hakijawahi kutembekewa na Kiongozi wa Kitaifa.

Waziri Ummy Mwalimu yupo ziara ya kikazi Wilayani Msalala kujionea Utekelezaji wa  Mpango wa Malipo kwa Ufanisi(RBF) ambapo ulianza Januari 2016 kwa Mkoa wa  Shinyanga

RBFni Mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi ambapo vituo vinapewa maeneo ya utekelezaji na kupimwa kuona kama wamekidhi na kufikiwa malengo hivyo kituo huhakikiwa na hatimaye kutolewa fedha kulingana na matokeo ya idadi za huduma zilizotolewa na ubora kulingana na miongozo ya utoaji wa huduma za Afya.

Fedha zinazopatikana zinafanya maboresho ya vituo ikiwemo miundombinu ya kituo,madawa na vifaa tiba

Waziri Ummy Mwalimu ameipongeza halmashauri ya wilaya hiyo kwa kufanya vizuri katika kutekeleza Mpango huo hata hivyo aliwataka watendaji kufanya uhakiki na kujiridhisha kwamba huduma za Afya zitolewazo zinakidhi viwango kulingana na miongozo ya Afya ndipo malipo yatolewe

Alisema Mpango huo unahakikisha huduma ya Afya ya msingi zinatolewa bila vikwazo,"nimekuja kufuatilia utekelezaji kwakweli nimefurahi kwani mnatekeleza na mmeboresha huduma zenu"

Aidha,alisema kabla ya utekelezaji wa Mpango huo kuanza mwaka 2015 hali ya miundombinu ilikua mibovu,hakukuwa na dawa,hivyo kupitia Mpango huo Serikali hupeleka fedha ambazo zinasaidia kuimarisha mifumo ya vituo vya Afya,kuongeza huduma za huduma,kuchochea jamii kutumia vituo vya Afya hususan wanawake wajawazito pamoja na kutoa motisha kwa wahudumu na watumishi wa Afya katika vituo vya kutolea huduma.

"Mpango huu tunataka wanawake wajawazito waje vituoni ndani ya miezi mitatu ya mwanzo na serikali tunaleta shilingi 8290,na mjamzito akihudhuria kliniki angalau Mara NNE wakati wa ujauzito tunaleta shilingi 6210 kwenye zahanati" alisema Waziri Ummy

Alitaja kiasi cha shilingi 20,700 serikali inatoa kwa mjamzito akienda kujifungua kwenye Zahanati hivyo alitoa ari kwa wanawake wajawazito wilayani Msalala kuacha kwenda kujifungua kwa wakunga wa jadi kwani Serikali ya awamu ya tano imeboresha huduma za Afya nchini ikiwemo hali ya  upatikanaji wa dawa ambapo Msalala kwa mwaka wa fedha 2017/2018 wametengewa shilingi milioni 417 tofauti na ile ya mwaka 2015/2016 ya shilingi milioni 108.

DKT. NDUGULILE AMPA MAAGIZO DMO MPWAPWA.

Naibu Waziri akimuuliza maswali mmoja kati ya wauguzi anayehusika na stoo hiyo ya dawa kwenye kituo cha afya kibakwe.

Dkt.Ndugulie akiongea na baadhi ya wakazi wa Kibakwe waliofika kituoni hapo kuwajulia hali wagonjwa wao.Dkt.Ndugulile aliwasisitiza wakazi hao kusimamia matumizi ya fedha na dawa kwani kituo hicho kimetengewa shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha upasuaji wa dharura,nyumba za watumishi pamoja na ununuzi wa vifaa tiba kituoni hapo.

 Dkt.Ndugulile akiongea na watumishi wa kituo cha afya Kibakwe nje ya kituo hicho

Dkt.Faustine Ndugulile Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akikagua fomu ya orodha ya dawa iliyofanywa na kituo hicho kwa mnunuzi wa nje na ile ya MSD kwenye stoo ya dawa ya kituo cha afya cha kibakwe.


Picha ya pamoja ya Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto pamoja na watumishi wa kituo cha afya Kibakwe wilayani Mpwapwa.



Na WAMJW-DODOMA
NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amemuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa  Dkt. Said Mawjji kuandaa maoteo ya mahitaji ya dawa mapema na kupeleka Bohari kuu ya Dawa (MSD) kwa ajili ya upatikanaji huo na sio kununua dawa kiholela.
Hayo ameyasema wakati wa ziara yake kwa ajili ya kuangalia miundo mbinu pamoja na upatikanaji wa dawa na huduma za afya zitolewazo katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma aliyoifanya jana.
“Katika milioni 57 ya kununua dawa laki saba tu ndo imeenda MSD zilizobaki zimeenda kwa mshitiri mwingine ambapo ni uagizaji dawa kiholela kwani mmeshindwa kufuata taratibu za uagizaji dawa wakati dawa hizo zinapatikana MSD” alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha Dkt. Ndugulile alimuagiza Dkt. Mawjji kuhakikisha upanikaji wa dawa zote muhimu zinapatikana kwa asilimia 80 katika vituo vya afya wilayani hapo kama ilivyofikiwa na MSD katika kusambaza dawa hapa nchini ili kuondokana na tatizo la uhaba wa dawa ambapo ni kipaumbele cha Serikali kwa uapande wa sekta ya afya nchini.
Dkt. Ndugulile alimuagiza DMO wa Mpwapwa mpaka kufikia Desemba 13 mwaka huu awe tayari amewasilisha nyaraka za uagizaji dawa zote kuanzia Julai 2017mpaka Septemba mwaka huu ili kujiridhisha na utaratibu wao wa uagizaji dawa.
Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amemuagiza DMO huyo kujitahidi kuongeaa baadhi ya watumishi katika kituo cha afya cha Kibakwe kilichopo katika tarafa ya Kibakwe Wilayani Mpwapwa kwani wanahitajika watumishi akiwemo mtaalam wa maabara na mfamasia wa kituo ili kuleta ufanisi katika huduma za afya kituoni hapo.
Aidha Dkt. Ndugulile ameumbia uongozi wakituo cha afya Kibakwe na pamoja na wanakijiji kuwa Serikali imetenga milioni 500 kwa ajili ya ujenzi na  ukarabati wa jengo la upasuaji wa dharura kwa akina mama wajawazito,nyumba za watumishi pamoja na ununuzi wa  vifaa tiba ili kuokoa maisha ya akina mama wanapopata uzazi tata wakati wa kujifungua
Katika kituo hicho cha afya Kibakwe Naibu Waziri huyo alikutana na changamoto ya tofauti ya dawa kwenye fomu za kuagiza dawa MSD na zile za kununua dawa hizo kwa mshitiri wa nje hali iliyomlazimu Dkt.Ndugulile kuanza kuhakikia fomu moja kwa dawa moja hadi nyingine na kugundua ubadilishaji wa aina za dawa zilizoagizwa MSD na baadae kwa mnunuzi wa nje.
Hata hivyo Dkt.Ndugulile aliwakanya watumishi wa stoo ya dawa ya kituo hicho kuacha kufanya mchezo huo wa kubadilisha mahitaji ya dawa pale wanapokosa MSD na kiruhusiwa kununua nje kwani Serikali ya awamu ya tano imejipanga na kuhakikisha upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya kote nchi ni zaidi ya asilimia 80 na hivyo kuwataka wakazi wa Kibakwe kusimamia kwa makini matumizi ya dawa kituoni hapo.

Jumamosi, 9 Desemba 2017

DKT. NDUGULILE AFANYA ZIARA KATIKA CHUO CHA AFYA NA MAZINGIRA WILAYANI MPWAPWA.

Naibu Waziri  wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile wa kwanza kulia akimjulia hali mgonjwa aliyelazwa katika kituo cha afya cha kibakwe wakati wa ziara yake katika Kijiji hiko  wilani Mpwapwa mkoani Dodoma.


Naibu Waziri  wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile katikati aliyevaa shati la bluu akiongea na baadhi ya wananchi na watumishi wa afya wa kituo cha afya cha Kibakwe kuhusu changamoto na maendeleo ya sekta ya afya katika Kijiji hicho wakati wa ziara yake wilani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Naibu Waziri  wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua dawa zilizopo kwenye stoo ya dawa ya Kituo cha afya cha  Kibakwe  wakati wa ziara yake katika Kijiji hiko  wilani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Naibu Waziri  wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile wa kwanza kulia akiwajulia hali wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma wakati wa ziara  yake leo wilayani humo.

Naibu Waziri  wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile wa pili kushoto akiongea na baadhi ya watumishi wa Chuo Cha Afya na Mazingira Mpwapwa alipotembelea chuo hiko wakati wa ziara yake wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma, wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Chuo hiko Bw. Rogasian Tarimo.

Naibu Waziri  wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile mbele aliyevaa shati la bluu akisikiliza changamoto kutoka kwa  badhi ya wanafunzi wa mwaka wa pili fani ya udaktari katika Chuo Cha Afya na Mazingira Mpwapwa alipotembelea chuo hiko wakati wa ziara yake wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri  wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa ziara yake katika Chuo Cha Afya na Mazingira  wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

HOSPITALI YA SARATANI YA OCEAN ROAD YATOA HUDUMA YA UCHUNGUZI WA SARATANI KWA WATU WENYE ALBINO

 





Hospitali ya Saratani ya Ocean Road imefanikisha kutoa huduma za uchunguzi wa Saratani kwa watu wenye albino.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa huduma za jamii hospitali ya Saratani ya Ocean Road Dkt. Cyrpian katika ziara yake Mkoani Simiyu.

Dkt. Cyrpian alibainisha kuwa Uchunguzi huo umefanywa kwa kushirikiana na Taasisi ya Albino nchini huku likijumuisha kuwafundisha wataalamu wa Afya na kuanzisha Kliniki za kutoa huduma  hizi.

“tumefanyia uchunguzi albino 16 Kati ya hao 2 wana saratani, watu 12 wenye dalili za awali za saratani tumewatibu papo hapo kwa tiba baridi huku wawili wakiwa vizuri” alisema Dkt. Dkt. Cyrpian.

Dkt. Cyrpian alibainisha kuwa zoezi hili limeanza tangu Desemba 3 mpaka Desemba 9 Wilayani Misungwi liliwalenga wanafunzi 65 kutoka shule ya msingi Misungwi Mitindo huku wanafunzi 50 wakipewa mafuta ya albino yakujikinga na jua. Wanafunzi 2 walikuwa na dalili za aratani ya ngozi na walitibiwa kwa tiba baridi (cryotherapy) na 13 walikuwa hawana shida.

Dkt. Cyrpian alikiri kuwafundisha madaktari katika hospitali ya wilaya  ya Misungwi, hospital ya shinyanga na Simiyu.