Hospitali ya
Saratani ya Ocean Road imefanikisha kutoa huduma za
uchunguzi wa Saratani kwa watu wenye albino.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa huduma za jamii hospitali ya
Saratani ya Ocean Road Dkt. Cyrpian katika
ziara yake Mkoani Simiyu.
Dkt. Cyrpian alibainisha kuwa Uchunguzi huo umefanywa kwa kushirikiana na
Taasisi ya Albino nchini huku likijumuisha kuwafundisha wataalamu wa Afya na
kuanzisha Kliniki za kutoa huduma hizi.
“tumefanyia uchunguzi albino 16 Kati ya hao 2 wana saratani,
watu 12 wenye dalili za awali za saratani tumewatibu papo hapo kwa tiba
baridi huku wawili wakiwa vizuri” alisema Dkt. Dkt. Cyrpian.
Dkt. Cyrpian alibainisha kuwa zoezi hili limeanza tangu Desemba 3 mpaka
Desemba 9 Wilayani Misungwi liliwalenga wanafunzi 65 kutoka shule ya msingi
Misungwi Mitindo huku wanafunzi 50 wakipewa mafuta ya albino yakujikinga na
jua. Wanafunzi 2 walikuwa na dalili za aratani ya ngozi na walitibiwa kwa tiba
baridi (cryotherapy) na 13 walikuwa hawana shida.
Dkt. Cyrpian alikiri kuwafundisha madaktari katika hospitali ya wilaya ya Misungwi, hospital ya shinyanga na Simiyu.
0 on: "HOSPITALI YA SARATANI YA OCEAN ROAD YATOA HUDUMA YA UCHUNGUZI WA SARATANI KWA WATU WENYE ALBINO"