Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya Viongozi na Wananchi wa Wilaya ya Chamwino wakati alipotembelea kujionea Usafi wa mazingira na matumizi ya Choo katika Wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mh. Vumilia Nyamonga akiongea na wananchi wake (hawapo kwenye picha) juu ya Usafi wa mazingira na matumizi ya choo, katika ziara ya Waziri wa Afya katika Wilaya hiyo mjini Dodoma, kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na kulia kwake ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. James Charles.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. James Charles akijibu
hoja ya mwananchi wa Kijiji cha Humekwa mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha) kuhusu upatikanaji wa kadi za matibabu ya
wazee wilayani hapo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mh. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Elizabeth Arthur wakati alipotembelea
kujionea Usafi wa mazingira na matumizi ya Choo katika Wilaya hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mh. Ummy Mwalimu akiongea na mkazi wa Kijiji cha Humekwa Wilaya ya Chamwino Bi
Cesilliah Isaya aliyefanikiwa kujenga choo chenye ubora kwa gharama ndogo ya
shiringi 55,000 tu.
Kikundi cha ngoma kutoka Kijiji cha Humekwa kikitoa Burudani
mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy
Mwalimu wakati alipofanya ziara ya kujionea Usafi wa mazingira na matumizi ya
Choo katika Wilaya hiyo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Wakazi wa Kijiji cha Humekwa
waliojumuika katika kuunga mkono ziara ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha) ili kujionea
Usafi wa mazingira na matumizi ya Choo katika Wilaya hiyo ya Chamwino Mkoani
Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mh. Ummy Mwalimu akifuatilia kwa ukaribu ratiba katika kituo kidogo cha Afya Kijiji cha
Humekwa wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mh. Ummy Mwalimu akikagua moja ya choo wakati alipofanya ziara katika Kijiji cha
Humekwa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma ili kuhamasisha usafi wa mazingira na
choo.
Mwanakijiji wa Kijiji cha Humekwa Bi Evaline Gidore akisoma
risala mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha) wakati alipofanya ziara ya
kujionea Usafi wa mazingira na matumizi ya Choo katika kijiji hicho mapema leo.
Diwani wa kata ya Aneti Mh. Peter Chidawali akitoa
mapendekezo mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mh. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha) kuhusu maboresho katika huduma za
Afya kijijini hapo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mh. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. James Charles wakati wa ziara ya kujionea Usafi wa mazingira na matumizi ya Choo
katika Wilaya hiyo, wa katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mh. Vumilia Nyamonga.
Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiongoza ziara katika kijiji cha Humekwa Wilaya ya Chamwino mapema leo Mkoani Dodoma.
NA WAMJW-DODOMA
SERIKALI
kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imedhamiria kuhakikisha kuwa kila Kituo cha Afya au Zahanati yoyote
inaongozwa na kusimamiwa na mganga na sio mhudumu wa afya au nesi kama
inavyofanyika kwenye baadhi ya vituo vya afya .
Hayo
yamesemwa na Waziri wa afya ,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto
Mheshimiwa Ummy Mwalimu wakati wa ukaguzi wa usafi wa mazingira leo
Mkoani Dodoma Wilaya ya Chamwino kata ya aneti Kijiji cha humekwa
kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya kitaifa ya usafi wa
mazingira iliyobeba ujumbe wa nipo tayari ambapo Makamuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa
mgeni rasmi.
"Hatua ya
kuimarisha upatikanaji wa dawa, upatikanaji wa vifaa na vifaa tiba
hususani vya dharura na upasuaji sanjari na kuweka mazingira safi ya
upatikanaji wa maji na vyoo safi na salama ili kupunguza magonjwa na
vifo vitokanavyo na kutokuwepo kwa huduma bora za maji na afya kwa
wakati ndiyo lengo letu" alisema Waziri Ummy.
Aidha
Waziri Ummy amesema kuwa kabla ya Serikali ya Mhe. Rais John Pombe
Magufuli haijaingia madarakani bajeti ya dawa ya wilaya ya chamwino
ilikuwa milioni 113 lakini mwaka jana bajeti ya dawa ilikuwa milioni
436 ambapo katika mwaka wa pili wametengewa milioni 505 hali inayoonesha
jitihada za dhati za serikali ya awamu ya tano kuboresha hali ya afya
ya wananchi hususani waliokuwa Vijijini.
Mbali
na hayo Waziri Ummy amewataka wananchi wa kijiji cha Humekwa kukata
kadi ya matibabu za CHF kwani zinarahisha upatikanaji wa huduma za afya
kwa urahisi na kupunguza gharama .
Aidha
Waziri Ummy amesema kuwa wananchi ambao wana ugonjwa kifua kikuu hawana
budi kuwahi hospitali na vituo vya kutolea huduma za afya kwa ajili ya
kupata dawa ili kuokoa maisha yao kwani dawa hizo hazilipiwi gharama
yoyote.
Kwa upande wake
Diwani wa Kata ya Aneti Peter Chidawali ameiomba Serikali kuwasaidia
Wananchi wa Humekwa katika hatua iliyofikiwa kwenye ujenzi wa jengo la
upasuaji ambalo wananchi wanajitolea michango yao kujenga ili likamilike
kwa matumizi yaliyokusudiwa.
Kwa
upande wake Msomarisala wa Kijiji cha Homekwe Evaline Gidore
amebainisha kuwa kampeni ya usafi wa mazingira na ujenzi wa vyoo bora
imeasaidia kupunguza idadi ya wagonjwa walioathiriwa na magonjwa
yatokanayo na uchafuzi wa mazingira .
"Kampeni
hii imechangia kuepuka magonjwa hatari kama vile kuhara damu, typhoid
na minyoo kutoka wagonjwa138 mwezi disemba 2015 hadi kufikia wagonjwa
26 Novemba Mwaka huu kwa vile tumejitahidi kuzingatia usafi wa mazingira
na matumizi ya vyoo bora"Alisema Bi Eveline.
0 on: " WAZIRI UMMY ATAKA UTARATIBU WA UONGOZI KWENYE VITUO VYA AFYA UFATWE"