JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
WIZARA YA AFYA,
MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA
HOSPITALI YA RUFAA YA TAALUMA NA TIBA (MAMC) ILIYOKO MLOGANZILA
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayo
furaha kuwatangazia wananchi wote na wadau wote wa Sekta ya Afya kuwa,
Hospitali ya Rufaa ya Taaluma na Tiba (MAMC) ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili (MUHAS) iliyoko Mloganzila, jijini Dar es Salaam, imeanza
kupokea wagonjwa waliopewa rufaa kwa ajili ya matibabu ya magonjwa ya ndani (internal
medicine).
Hii
inafuatia kufunguliwa rasmi kwa Hospitali hiyo na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mnamo tarehe 25 Novemba,
2017.
Wizara
inapenda kutumia fursa hii kuwafahamisha Waganga Wakuu wa Hospitali za Rufaa za
Mikoa na Kanda kwamba maelekezo yamekwisha tolewa ya namna ya kuelekeza rufaa za
wagonjwa wao katika hospitali ya MAMC.
Aidha,
Wizara inapenda kuwataarifu Wananchi na Wadau wa Huduma za Afya kuwa, MAMC ni
Hospitali ya kisasa kabisa, na ina uwezo wa kutoa huduma za kibingwa kwa
kiwango kama kile ambacho kinatolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Vilevile,
MAMC inashirikiana na wataalamu mabingwa kutoka MNH katika kuhudumia wagonjwa.
Taarifa
hii ni muhimu kwa kuwa, kumekuwa na uvumi kutoka kwa baadhi ya wadau wanaodhani
kuwa hospitali hii ni ya mafunzo, na hivyo haiwezi kutoa matibabu sawa na MNH.
Wizara inawahakikishia wananchi na wadau wote kuwa, huduma zinazotolewa na MAMC
zinajumisha pia huduma za daraja la ubingwa wa ngazi ya juu (super specialized services) na zenye ubora
stahiki.
Wizara
inatoa wito kwa wananchi na wadau wote kupokea na kutumia huduma zinazotolewa
na MAMC.
Wizara
itaendelea kutoa taarifa za huduma mpya za MAMC kwa kadri zitakavyokuwa
zinaanzishwa ili rufaa husika zielekezwe huko.
Dkt.
Mpoki M. Ulisubisya.
KATIBU MKUU (AFYA)
14/12/2017
0 on: " HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA HOSPITALI YA RUFAA YA TAALUMA NA TIBA (MAMC) ILIYOKO MLOGANZILA"