Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia
Suluhu Hassan akisisitiza jambo mbele ya wadau na wakazi wa Chang’ombe Mkoa wa
Dodoma katika Uzinduzi wa kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba ni Choo
iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Chang’ombe.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mh. Ummy Mwalimu akimkabidhi zawadi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa
Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa
usafi wa mazingira na vyoo bora kutoka halmashauri mbali mbali nchini Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia
Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakipiga makofi ishara ya kupongeza uzuri na usafi wa
moja ya mfano wa choo bora.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan wapili kutoka kushoto wakiwa mbele
ya choo bora, tukio lililifanyika katika viwanja vya shule ya msingi Chang’ombe
Mkoani Dodoma. Wakwanza ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mh. Ummy Mwalimu, watatu ni Elizabeth Arthur na wa mwisho ni Waziri wa
TAMISEMI Suleiman Jaffo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan wapili kutoka kushoto akiwapungia mkono wakazi wa Chang'ombe na wadau wa masuala ya mazingira na usafi wa vyoo. akwanza ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mh. Ummy Mwalimu, watatu ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Mahenge.
Timu ya viongozi wa serikali ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakiwa tayari kumpokea mgeni rasmi Makamu wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.
Mratibu wa Kampeni ya kitaifa ya Usafi na Mazingira kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Anyitike Mwakitalima akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akimuelekeza jambo Waziri wa TAMISEMI Suleiman Jaffo wakiwa katika banda la maonesho la Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mpango wa Simavi Thea Bongertman, wa kwanza ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu.
Kikundi cha Burudani kutoka eneo la Chang’ombe Mkoani Dodoma, kikionesha manjonjo mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wa Serikali.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha akipokea zawadi ya Usafi bora ya gari kutoka kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiwa na Naibu wa Wizara hiyo Mh. Faustine Ndugulile wakimkabidhi zawadi ya Usafi bora Mwakilishi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bi Eveline Kibenya.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiwa na Naibu wa Wizara hiyo Mh. Faustine Ndugulile na Elizabeth Arthur katika bango la kampeni ya “Usichukulie Poa Nyumba ni Choo”
Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiwa na Naibu wa Wizara hiyo Mh. Faustine Ndugulile wakiwa pamoja na Washindi Usafi na vyoo bora kutoka Halmashauri mbali mbali nchini.
NA
WAMJW-DODOMA.
WATANZANIA wanapaswa kuzingatia mambo ya msingi hususani matumizi ya vyoo bora ili kuepuka magonjwa ya kuambukiza na mlipuko kwa ajili ya kujenga
Tanzania ya Viwanda pasipokuwa na adui mkubwa wa maradhi nchini.
Hayo
yamesemwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa
awamu ya pili ya kampeni ya taifa ya mazingira uliyofanyika mkoani leo Mkoani
Dodoma.
“Watanzania
tunapaswa kuzingatia mambo ya msingi ikiwemo kutumia vyoo bora ,kunawa mikono
kwa maji safi yanayotiririka na sabuni pamoja na kuchemsha maji ya kunywa ili
kuepuka magonjwa mlipuko nchini” alisema Mhe. Samia.
Aidha
Mhe. Samia amesema kuwa watanzania tunatakiwa kuwa kipaumbele kwenye usafi wa
mazingira kwa tumepoteza kiasi cha shilingi bilioni 440 kutokana na hali duni
ya usafi wa hasa ukosefu wa huduma ya vyoo bora.
Kwa
mujibu wa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu
Hassan amesema kuwa takwimu zinaonyesha watu wapatao elfu thelathini
huugua magonjwa ya kuhara kila mwaka na baadhi yao hupoteza maisha hivyo
tunatakiwa kuzingatia usafi wa mazingira
ili kuepuka idadi ya wastani wa watu 83 kwa siku.
“Taifa
hatuna kuwekeza nguvu na rasilimali zetu katika suala la usafi wa mazingira
ikiwemo matumizi ya maji safi na vyoo bora ili kufikia malengo yetu ya kitaifa
pampja nay ale ya kidunia” alisema Mhe. Samia Suluhu.
Mbali na
hayo Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema
kuwa endapo watoto wataendlea kuishi kwenye mazingira machafu ni hatarishi kwani kuna
uwezekano wa kuwa na watoto waliodumaa kimwili na kiakili.
Kwa
upande wake Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Me. Ummy
Mwalimu amesema kuwa Tanzania inaendelea kupambana na ugonjwa wa kipindupindu
ambao ulirejea tena mwaka 2015 baada ya kupotea takribani miaka minne.
“ Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameonesha
kusikitishwa kwake kutokana na uwepo wa kipindupindu nchini hivyo watanzania
hatuna budi kuwa wasafi wa mazingira ili kuepuka mlipuko wa ugonjwa huo”
alisema Waziri Ummy.
Aidha
Waziri Ummy amewataka watanzania kupambana na adui wa afya kwa kutunza
mazingira na kuepuka vishiria vya magonjwa mbalimbali kuliko kulalamika ukosefu wa dawa kwani kinga
ni bora kuliko tiba.
Kwa
upande Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Bw. Suleiman Jaffo amesema kuwa kupitia ofisi yake atahakikisha anasimamia na
kuwaagiza watendaji wake wa ngazi zote
kusimamia usafi wa mazingira kama
alivyoagizwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Kampeni
iliyozinduliwa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan jijini Dodoma ni ya
awamu ya pili ya usafi wa mazingira ambayo imebeba ujumbe usemao “USICHUKULIE POA
NYUMBA NI CHOO” imeenda sambamba na ugawaji wa zawadi na vyeti kwa waliofanya
vizuri kwenye usafi wa mazingira ambapo Halmashauri ya Mji wa Njombe umeibuka
kidedea na kupata zawadi ya Trekta.
0 on: "WATANZANIA WATAKIWA KUZINGATIA MATUMIZI YA VYOO BORA"