Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani
Nchini SACP Fortunatus Musilimu aliyesimama akiongea na wadau mbalimbali wa
usalama barabarani hawapo pichani wakati
wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo
mjini Dodoma.
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani
(WHO) Bi. Mary Kessy akiongea na wadau mbalimbali wa usalama barabarani hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili
hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.
ASP Deus Sokoni wa kwanza kulia akiongea
na wadau mbalimbali wa usalama barabarani
hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani
nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa
Huduma za Sheria Wizara ya Mambo ya Ndani
Bi. Marlin Komba anayefuata ni
Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu.
Katibu Mkuu wa Shirikishi wa vyama vya
Walemu nchini Bw. Felicina Mkude aliyesimama akiongea na baadhi ya wadau
mbalimbali wa usalama barabarani hawapo
pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini
kilichofanyika leo mjini Dodoma.
Baadhi
ya wadau mbalimbali wa usalama barabarani wakimsikiliza kwa makini Kamanda wa Kikosi
Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu hayupo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama
barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.
Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani
Nchini SACP Fortunatus Musilimu katikati ya waliokaa akiwa kwenye picha ya pamoja
na wadau mbalimbali wa usalama barabarani
wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini
kilichofanyika leo mjini Dodoma.
Na.WAMJW-Dodoma
Madereva
nchini wamepongezwa kwa kuanza kubadilika na kutii sheria bila
shuruti katika kukabiliana na ajali za barabarani na hivyo kupungua kwa
ajali pamoja na vifo vitokanavyo na ajali kwa uendeshaji unaofuata
taratibu na sheria za barabarani.
Hayo yamesemwa na
Kamanda wa Kikosi cha Barabarani Tanzania Fortunatus Musilimu -Kamishana
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP) wakati akifungua mkutano wa siku
mbili wa kupokea maoni ya sheria kuhusu ajali za barabarani
unaojumlisha mashirika yasiyo ya Kiserikali.
Kamanda
Musilimu alisema tatizo la ajali barabarani bado ni kubwa kwani watu
wengi wanafariki na kujeruhiwa kutokana na ajali barabarani.
”sisi sote ni wahanga wa usalama barabarani hivyo hatuna budi wadau wote kushirikiana katika kukabiliana na suala hili na kila mmoja anayo nafasi ya kuchangia ili usalama wa barabarani uimarike na kuboreka zaidi”Alisema.
”sisi sote ni wahanga wa usalama barabarani hivyo hatuna budi wadau wote kushirikiana katika kukabiliana na suala hili na kila mmoja anayo nafasi ya kuchangia ili usalama wa barabarani uimarike na kuboreka zaidi”Alisema.
Alisema hivi sasa watu wengi
wameanza kubadilika hususani madereva wengi ambapo kuna wakati inabidi
jeshi la polisi kutumia nguvu nyingi ili kuweza kuepuka ajali zinazoweza
kuepukika na nguvu hizi zimetumika kwa nia nzuri ili watanzania kuwa
salama wanapotumia vyombo vya moto.
Akitolea mfano
kwa hali ya usalama barabarani kwa siku ya jana (juzi) nchi nzima
kulikua na ajali nne ambazo zimesababisha vifi viwili na majeruhi
nne,hivyo ni hatua nzuri na hata hivyo aliwataka
wadau hao kuhakikisha wanatoa maoni mazuri ambayo yatasaidia kupata
sheria ambayo haitamkandamiza mwananchi na ambayo itakua salama na
kupunguza ajali za barabarani nchini na kuwa na sheria inayotekelezeka
kwa kupunguza ajali kwa asilimia 50.
“Serikali
ya awamu ya tano inapenda kulinda maisha ya watanzania,serikali
inatengeneza uchumi wa kati na viwanda kwa kuboresha miundombinu
ikiwemo barabasha hivyo jukumu letu kushirikiana na serikali kuilinda
miundombinu yote inayotengenezwa”
Aidha,Kamanda
Musilimu aliwataka wananchi waondoe dhana kwamba ajali zinatokana na mapenzi ya Mungu, “Hii siyo kweli ila matatizo yote ya ajali ni sisi
wenyewe tunasababisha kutokana na mwendo kasi na kutotii sheria za
barabarani".
Alitaja takwimu za ajali barabarani kwa
Tanzania kwa mwezi Julai hadi Septemba mwaka 2016 ilikua 639,vifo 923
na majeruhi 2,469 na kwa mwaka 2017 kuanzia Julai hadi Septemba ajali
za barabarani zilikuwa 1,376,vifo 655 pamoja na majeruhi 1,469.
Naye
Mwakilishi toka shirika la Afya Dunia Mery Kessy alisema zaidi ya
asilimia 90 za ajali zinazotokea katika nchi zinazoendelea ingawa ni
asilimia 10 tu nchi hizo zinamiliki vyombo vya moto na hiyo ni kutokana
na sababu mbalimbali ikiwemo miundombinu,mazingira pamoja na tabia.
Alisema
wahanga wakubwa wanaopata ajali na vifo ni vijana kati ya miaka miaka
15 mpaka 29 kwani umri huu wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kusababisha
ajali na hivyo ajali hizo kuchukua zaidi ya asilimia 3 za pato la Taifa
kwani serikali inaingia gharama kubwa kutibu majeruhi katika sekta ya
afya.
0 on: "MADEREVA WAANZA KUTII SHERIA ZA BARABARANI BILA SHURUTI"