Naibu Waziri Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza
jambo mbele ya baadhi ya Watumishi(hawapo kwenye picha) wa Taasisi ya Kiuma
inayomiliki chuo cha Uuguzi, Kituo cha Afya na Kanisa la Upendo wa Kristo
Kiuma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua daftari la
baadhi ya Vifaa vya Maabala wakati alipofanya ziara katika Wilaya ya Tunduru
Kituo cha Afya cha Kiuma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua
baadhi ya vifaa katika chumba cha Kompyuta wakati alipofanya ziara katika
Wilaya ya Tunduru Kituo cha Afya cha Kiuma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akipata
maelezo kutoka kwa Msimamizi wa kike(Matroni) wa Kituo cha Afya cha Kiuma Maria
Ntazama, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kiuma na Mwenyekiti wa
Kanisa la Upendo wa Kristo Kiuma Dkt. Matomola.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua
moja ya darasa katika chuo cha Uuguzi Kiuma wakati alipofanya ziara katika
Wilaya ya Tunduru Kituo cha Afya cha Kiuma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua
vitabu katika maktaba ya chuo cha Uuguzi na ukunga Kiuma wakati alipofanya
ziara katika Wilaya ya Tunduru.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (katikati)
wakiwa katika ziara yake Wilayani Tunduru, wakwanza ni Mkurugenzi wa
Mafunzo Wizara Ya Afya Dkt. Otilia Gowele na kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa
taasisi ya Kiuma ambae pia ni Mwenyekiti wa Kanisa la Upendo wa Kristo Dkt.
Matomola.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipata
maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya Kiuma ambae pia ni Mwenyekiti
wa Kanisa la Upendo wa Kristo Dkt. Matomola, wakati akikagua mabweni ya
chuo cha Uuguzi na ukunga Kiuma kilichopo Wilaya ya Tunduru.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha
uuguzi na ukunga Kiuma kilichopo Wilaya ya Tunduru wakifuatilia hotuba kutoka
kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Dkt Faustine (hayupo kwenye picha),
wakati alipofanya ziara katika taasisi hiyo ya Kiuma Wilayani Tunduru.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua kwa umakini Daftari la
opokeaji Dawa pembeni yake ni Afisa wa Kliniki Hassan Miengende.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua Kadi za dawa wakati alipofanya
ziara katika kituo cha Afya Mkasale Wilayani Tunduru.
Wanchi wa Kijiji cha Mkasale
wakifuatilia kwa makini agizo kutoka kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile juu ya usimamiaji wa rasilimali fedha
katika kituo chao cha Afya.
Na
WAMJWW, TUNDURU
Serikali ya awamu ya
tano kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imejipanga kuanzisha mfuko wa Bima ya Afya kwa watu wote nchini jambo
litalosaidia kupunguza gharama za matibabu kwa kiasi kikubwa.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipofanya ziara katika Wilaya ya
Tunduru Mkoani Ruvuma katika Taasisi ya Kiuma inayomiliki Hospitali, Chuo cha
Uuguzi na Kanisa la Upendo wa Kristo.
“Tunatambua
kwamba si kila mtu anamudu gharama hizo, kwa bahati mbaya ugonjwa unakuja
wakati hatuja jiandaa, serikali imeliona hilo, pamoja na mikakati tunayoendelea
nayo ya Bima ya Afya ya NHIF na CHF, tunatarajia kuja na utaratibu wa bima ya
afya kwa wote, suala la matibabu lisiwe la kuwaza” alisema Dkt. Faustine
Ndugulile.
Dkt.
Faustine aliendelea kusema kwamba, Serikali inaendelea kufanya vizuri barani
Afrika na Dunia kwa ujumla kwa upande wa utoaji chanjo, kwani imefikia asilimia
97 ya walengwa wote wanaohitaji chanjo
nchini jambo linalosaidia kutunza Afya za watu katika jamii.
“Tumefkia
hatua kubwa sana ya walengwa wote wanaohitaji kupata chanjo, jambo linaloifanya
Tanzania kuwa moja kati ya nchi chache sana zilizofikia malengo hayo” alisema
Dkt. Faustine
Aidha
Serikali imetoa fedha kwa Vituo vya Afya 172 kwa lengo la kujenga thieta, Chumba
cha Kujifungulia, Wodi ya Wazazi, nyumba ya Watumishi na Maabara, Huku Wilaya
ya Tunduru ikifanikiwa kupata fedha hizo kwa vituo viwili, kikiwepo kituo cha
Afya cha Mkasale.
Kwa
upande mwingine Dkt. Faustine
ameupongeza uongozi wa Taasisi ya Kiuma kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya
ikiwemo kutoa huduma za afya kwa wananchi, kutoa ajira, jambo linalotokana na
uwekezaji mkubwa uliofanywa na Taasisi hiyo hivyo kuipunguzia mzigo Serikali
katika Nyanja hizo.
Nae
Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Uuguzi ambae pia ni Mwenyekiti wa Kanisa la Kanisa
Upendo wa Kristo Kiuma Dkt. Matomola ameiomba Serikali kupitia Naibu Waziri wa
Afya Dkt. Faustine Ndugulile itambue huduma inayotolewa chuoni hapo na
kuwaongezea Watumishi, pia Serikali iwasaidie kuchangia mahitaji madogo madogo
kama vitabu, maabara na vifaa.
Katika
ziara hiyo Dkt. Ndugulile alifanikiwa kutembelea Kituo cha Afya Mkasale katika Wilaya
hiyo ya Tunduru na kujiridhisha na hali ya upatikanaji wa dawa huku akiwasisitiza
wananchi wasiuziwe dawa zote muhimu kwani hali ya upatikanaji wa Dawa ni nzuri
maeneo yote na sasa ni wastani wa asilimia 80.
Aidha
Dkt. Ndugulile amewahakikishia wanakijiji wa Mkasale kuwa kituo chao cha Afya
kipo katika Vituo 172 vilivyopata mgao wa fedha za ujenzi wa maabara, chumba
cha kujifungulia, Wodi ya wazazi, thieta, na kuwataka kusimamia vizuri fedha
hizo ili kuweza kuboresha Zaidi huduma katika kituo hicho.
Nae Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Chiza
Marando wakati akiwasilisha taarifa ya Wilaya alisema kuwa Halmashauri ya
Wilaya ya Tunduru ina jumla ya vituo vya kutolea huduma za Afya 65 zikiwemo Hospitali
3 Vittuo vya Afya 5 na Zahanati 57 kati ya hizo 52 ni za serikali, 3 ni za
mashirika ya dini na 2 zinamilikiwa na watu binafsi.
Mhe. Chiza Marando
aliongeza kuwa Halmashauri ya Tunduru inakabiriwa na uhaba mkubwa wa watumishi
wa kada ya Afya hali inayopelekea changamoto kubwa katika utoaji wa huduma kwa
wananchi katika halmashauri hiyo.
“Tunduru ina jumla ya
watumishi 339 wa Serikali sawa na asilimia 26.3 kati yawatumishi 1286
wanaohitajika na kufanya upungufu wa watumishi 974 sawa na asilimia 73.6, huku
upungufu mkubwa ukiwa katika kada ya
madaktari, waganga, maafisa Afya na wauguzi.” Alisema Mhe. Chiza Marando
Kwa upande mwingine
Mhe. Marando aliongeza kwa kusema hali ya utoaji huduma imeongezeka ikiwemo
Huduma ya Chanjo kutoka 94 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 95 mwaka 2016 na
kwa mwaka 2017 kiwango kimefikia asilimia 92.
Aidha Mhe. Chiza
Marando alisema kuwa Wilaya hiyo inatoa huduma kwa makundi maalumu kwa
kuzingatia Sera ya Wizara ya Afya kwa kutoa vitambulisho vya matibabu ya Wazee
kwa baadhi ya kata zilizofanyiwa utambuzi, tayari vitambulisho 1234 vimetolewa
kwa Wazee.
0 on: " SERIKALI YATARAJIA KUANZISHA BIMA YA AFYA KWA WATU WOTE"