Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 13 Desemba 2017

TAARIFA YA MWEZI NOVEMBA KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO


TAARIFA YA MWEZI NOVEMBA KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI ILIYOTOLEWA NA MHE. UMMY MWALIMU (MB); WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, TAREHE 13 DISEMBA 2017

Ndugu wanahabari,
Huu ni mwendelezo wa taarifa za kila mwezi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuhusu mwenendo wa mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu nchini ikiwa taarifa hii ni ya mwezi Novemba 2017. Aidha taarifa hii inaendelea kutoa maelekezo ya hatua zinazotakiwa kuchukuliwa katika kudhibiti ugonjwa huu nchini.

Ndugu Wanahabari,
Kwa kipindi cha kuanzia tarehe 01 hadi 30 Novemba 2017, jumla ya wagonjwa walioripotiwa walikuwa ni 462 na vifo 15. Jumla ya Mikoa 10 na Halmashauri 17 zimeripoti wagonjwa wa Kipindupindu kwa mwezi Novemba. Mikoa iliyoripoti wagonjwa wa Kipindupindu ni Dar es salaam (14 na kifo 1), Dodoma (20 bila kifo), Tanga (5 bila kifo), Ruvuma (73 na vifo 8), Morogoro (5 bila kifo), Rukwa (7 na kifo 1), Manyara (13 na kifo 1), Songwe (80 bila kifo), Mbeya (119 bila kifo), Kigoma (126 na kifo1). Halmashauri zilizoripoti wagonjwa wa Kipindupindu ni Kinondoni (8 bila kifo), Ubungo (6 na kifo1), Mpwapwa (5 bila kifo), Chamwino (12 bila kifo) na Bahi (3 bila kifo), Mkinga  5 bila kifo), Nyasa (73 na Vifo 8), Kilosa (5 bila kifo), Sumbawanga Vijijini (7 na kifo1), Kiteto (13 na kifo1), Songwe Vijijini (80 bila kifo), Mbeya Vijijini (25 bila kifo), Mbeya Mjini (26 bila kifo), Chunya (10 bila kifo), Kyela (58 bila kifo) na Kigoma vijijini (10 bila kifo), Uvinza (116 na kifo 1)



Ndugu Wanahabari,
Takwimu zinatuonesha bado maambukizi mapya ni tishio kwani kuna ongezeko la idadi ya Mikoa na Halmashauri zinazotoa taarifa za wagonjwa ikilinganishwa na mwezi uliopita japokuwa idadi ya wagonjwa imepungua. Mwezi wa Oktoba tulikuwa na jumla ya wagonjwa 570 ikilinganishwa na mwezi huu ambapo tuna jumla ya wagonjwa 462. Jumla ya Mikoa 6 na Halmashauri 11 ziliripoti wagonjwa wa Kipindupindu mwezi uliopita ukilinganisha na jumla ya Mikoa 10 na Halmashauri 17 zilizoripoti wagonjwa mwezi huu.
Pia takwimu za kipindupindu nchini kwa mikoa za tangu mwaka huu uanze zinaonyesha ongezeko za ugonjwa huu, Aidha kwa kipindi cha Januari hadi Novemba, 2017, jumla ya mikoa 17 ilitoa taarifa za wagonjwa wa Kipindupindu, ikiwa na jumla wa wagonjwa 3,839 na vifo 71 (Kama jedwali linalofuata linavyoenesha). Mikoa saba (7) haikuripoti kuwepo kwa ugonjwa huu, mikoa hii ni pamoja na Mwanza, Shinyanga, Arusha, Lindi, Kagera, Simiyu, Kilimanjaro na Mtwara.
Na.
Mkoa
Januari hadi Septemba, 2017
Octoba,2017
Novemba,2017
Jumla(Januari hadi Novemba,2017)
Wagonjwa
Vifo
Wagonjwa
Vifo
Wagonjwa
Vifo
Wagonjwa
Vifo
1
Mbeya
591
7
0
4
119
3
710
14
2
Morogoro
308
11
7
0
5
0
320
11
3
Dar es Salaam
306
4
0
0
14
1
320
5
4
Iringa
274
8
58
1
0
0
332
9
5
Dodoma
216
3
14
1
20
0
250
4
6
Kigoma
188
3
0
0
126
1
314
4
7
Katavi
133
1
0
0
0
0
133
1
8
Tanga
117
2
6
1
5
0
128
3
9
Mara
110
0
0
0
0
0
110
0
10
Pwani
83
1
0
0
0
0
83
1
11
Manyara
0
0
0
0
13
1
13
1
12
Songwe
82
0
376
4
80
0
538
4
13
Singida
58
0
0
0
73
8
131
8
14
Rukwa
46
1
0
0
7
1
53
2
15
Ruvuma
0
0
0
0
0
0
0
0
16
Njombe
10
0
0
0
0
0
10
0
17
Tabora
7
1
0
0
0
0
7
1
Jumla
2816
45
461
11
462
15
3739
71


Ndugu Wanahabari,
Nchi yetu inaelekea katika majira ya mvua ambazo zinaweza kuongeza kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa Kipindupindu, hivyo tunahitaji kuzidisha juhudi za kuzuia ugonjwa huu, kwa kusimamia kikamilifu maelekezo na miongozo stahiki inayotolewa.  Aidha, Wizara inaendelea kuwasihi wananchi kuungana na Halmashauri, Mikoa pamoja na Wizara katika juhudi za kupambana na kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu. Jamii izingatie kanuni za usafi binafsi na usafi wa mazingira, ikiwa ni pamoja na:
1.    Kujenga na kutumia vyoo bora katika maeneo tunamoishi.
2.    Kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni kabla ya kula, baada ya kutumia choo, na baada ya kumsafisha mtoto aliyejisaidia.
3.    Mamlaka za maji zilizopo nchini zihakikishe upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi.
4.    Kunywa maji safi na salama yaliyotakaswa kwa dawa (kama vile water guard) au yaliyochemshwa na kupoa.
5.    Kuzingatia ushauri na elimu sahihi kuhusu ugonjwa wa kipindupindu, ili jamii iondokane na imani potofu kuhusu kipindupindu.
6.    Viongozi wa dini, watu mashuhuri na waganga wa tiba mbadala wasaidie kuhamasisha jamii zao kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huu.
7.    Kutoa huduma ya kwanza katika ngazi ya jamii kwa mgonjwa yeyote mwenye dalili za kipindupindu kwa kumpatia ORS.
8.    Endapo ORS itakuwa haipatikani hasa nyumbani, unaweza kutumia maji yaliyochanganywa na chumvi na sukari. Maji haya huweza kuandaliwa kwa kuchanganya maji safi yaliyochemshwa kiasi cha lita moja na vijiko viwili vya sukari na nusu kijiko ya chumvi.
9.    Kufikisha wagonjwa wa Kipindupindu mapema katika vituo vya kutolea huduma ili wawahi kupata matibabu.

Ndugu Wanahabari,
Ni dhahiri kuwa ushirikishwaji wa sekta zote kwa ngazi zote hadi katika jamii ni muhimu sana katika kukabiliana na ugonjwa wa Kipindupindu. Wizara inasisitiza kuwa wadau wote wapewe nafasi katika mapambano haya kupitia vikao mbalimbali ili kujadili udhibiti wa ugonjwa wa Kipindupindu kwenye halmashauri na mikoa. Viongozi wa dini, watu mashuhuri na waganga wa tiba mbadala pia wasaidie kuhamasisha jamii zao kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huu.

Ndugu Wanahabari,
Changamoto moja wapo katika kudhibiti ugonjwa wa Kipindupindu ni upatikanaji wa maji safi na salama. Wizara inaendelea kusisitiza yafuatayo yasimamiwe kwenye Halmashauri na Mikoa yote nchini.
  1. Kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yote mijini na vijijini hasa wakati wa mlipuko wa Kipindupindu. Hii ni pamoja na:
o   Mamlaka za maji katika ngazi zote ziweke mkazo wa kuwepo kwa vyanzo mbadala vya maji.
o   Utakasaji wa maji ya bomba kwa njia ya kutumia klorini ufanyike kama miongozo inavyotaka na ufuatiliaji wa ubora wa maji ufanyike kulingana na miongozo.
  1. Utoaji wa taarifa sahihi na kwa wakati, za ugonjwa wa Kipindupindu kwa kufuata miongozo iliyopo.
  2. Kuongeza uwajibikaji wa viongozi na watendaji (Leadership and accountability): Usimamizi wa utekelezaji wa miongozo katika kuzuia na kudhibiti ugonjwa huu ni muhimu kwa viongozi na wanaowasimawa. Hii ni pamoja na;
o   Usimamizi wa utekelezaji wa sheria ndogondodo za usafi wa mazingira ili kuimarisha matumizi ya vyoo.
o   Usafi wa mazingira pamoja na udhibiti wa biashara za chakula na pombe za kienyeji katika mitaa.
o   Kuzingatia agizo la Mheshimiwa Rais la kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.
  1. Kuihusisha jamii katika ngazi za chini kabisa (serikali ya kijiji/mtaa) kuongoza mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kipindupindu katika maeneo yao kwa kusimamiana wenyewe katiaka makundi madogo madogo yenye kaya 10 hadi 20 kufanikisha utekelezaji wa maelekezo yote yaliyotolewa na wataalamu wa afya. Maelekezo hayo ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa kaya ambazo hazitibu maji ya kunywa, hazijajenga na hazitumii choo, wanajamii wanaochafua vyanzo vya maji na kaya au wanajamii ambao bado wanaendesha kwa siri biashara za vinywaji au chakuka zilizosimamishwa.

Ndugu Wanahabari,
Hivi karibuni Makamu wa Raisi alizindua awamu ya pili ya kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira yenye kaulimbiu, “Usichukulie Poa Nyumba ni Choo”. Napenda kuchukua nafasi hii kuhimiza ujenzi wa vyoo bora kwa kila kaya ili kuweka safi mazingira yetu hasa ikizingatiwa kuwa ni asilimia 40 tu ya kaya hapa nchini zina vyoo bora.
Aidha, Wizara yangu imekuwa karibu na Mikoa na Halmashauri katika kudhibiti ugonjwa huu kwa kufanya yafuatayo:
o   Kutuma timu za wataalamu kwenda kwenye maeneo yaliyoathirika kushirikiana na Mikoa na Halmashauri katika kudhibiti ugonjwa huu
o   Kupima vipimo vya maabara na kubaini aina ya vimelea vinavyosababisha ugonjwa pamoja na kupima usikivu wa dawa inayofaa kutibu wagonjwa katika mlipuko huu
o   Kupeleka Vifaa tiba na dawa katika Mikoa na Halmashauri zilizoathirika kupitia kanda ya bohari ya Dawa (MSD)
o   Kusambaza dawa ya kutibu maji majumbani katika Mikoa na Halmashauri zilizoathirika

HITIMISHO
Ninatambua kuwa zimekuwepo jitihada mbalimbali, na ninawashukuru na kuwapongeza wote wanaoendelea kupambana na ugonjwa huu. Aidha, ninaendelea kuwashukuru wataalam wa sekta husika, mashirika ya kimataifa, watumishi, mikoa, halmashauri pamoja na waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla kwa kuendelea kushirikiana katika suala zima la kudhibiti ugonjwa wa Kipindupindu.



Asanteni sana

0 on: "TAARIFA YA MWEZI NOVEMBA KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI"