Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi na Ukunga kutoka Wizara ya Afya Gustav
Moyo akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya maadili kwa wauguzi wakuu wa
Mikoa na hospitali za Kitaifa na za Rufaa za kanda unaoendelea chuo cha
Uuguzi Mirembe Mkoani Dodoma
Wauguzi wakuu toka mikoa mbalimbali wakifuatilia mada zinazowasilishwa
kwenye mafunzo hapo.mafunzo hayo yana lenga kuwakumbusha uadilifu na
maadili ya uuguzi wakati wa utoaji huduma za afya nchini.
Baadhi ya wauguzi wa mikoa wakijadili kwenye makundi mikakati ya nini
kifanyike katika kutekeleza majukumu yao ili kuondokana na malalamiko ya
taaluma yao kutoka kwa wananchi.
Wauguzi wakuu wakiendelea na kazi kwenye makundi.
Mkurugenzi wa Uuguzi na Ukunga Gustav Moyo akiongea na wauguzi wakuu wa mikoa kwenye mafunzo hayo.
Na WAMJW-Dodoma
Wauguzi
wakuu wa Mikoa na hospitali za Taifa na Rufaa za Kanda wametakiwa
kusimamia maadili ili kupunguza malalamiko toka kwa wananchi.
Hayo
yamesemwa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Mpoki Ulisubisya wakati wa mafunzo juu
ya maadili kwa wauguzi wakuu yanayoendelea mjini hapa kwenye chuo cha
uuguzi na ukunga Mirembe
Dkt.Mpoki
alisema hivi sasa kumekua na malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya
huduma wanazozitoa hivyo kupitia mafunzo hayo wanapaswa kusimamia
ipasavyo maarifa na mikakati watakayojiwekea ili kuleta mabadiliko
makubwa na kuondoka malalamiko hayo.
"Jamii
na Serikali inawategemea sana katika usimamizi wa huduma bora
nchini,naamini kwamba ninyi mna nguvu,nia na maarifa katika kuboresha
maadili ya wauguzi wote nchini,hivyo ni muhimu mkasimamie"alisema
Dkt.Mpoki
Aidha, alisema
wizara yake inatambua umuhimu wa kuboresha maadili hususani kwa
wauguzi,hivyo kuwapatia mafunzo kama ni muhimu kwa taaluma yao.
"Kumekuwepo
na malalamiko na ongezeko kubwa la vitendo visivyo vya kiadilifu kwa
watumishi wa afya ikiwa ni pamoja na kauli mbovu kwa wagonjwa,naamini
kwa mafunzo haya changamoto zote mtazijadili na kusaidia kuondokana na
malalamiko toka kwa wananchi"
Naye
Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi na Ukunga wizara ya afya Gustav Moyo
alisema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa namna gani ya
kuboresha uadilifu na maadili ya sehemu zao za kazi wauguzi nchini
Aidha,ametoa
wito kwa wauguzi wote nchi kuzingatia Iadilifu,utu,upendo na maadili
yao ya kwa kuipatia thamani stahiki taaluma yao kwani wauguzi ndio
wanaokuwepo muda wote mahali pa kazi.
"Serikali ya
awamu ya tano inasisitiza suala la uadilifu hivyo wananchi wanahimizwa
kuwabaini na kuwasema ili kuwabaini baadhi ya wanaokiuka maadaili au
kufanya vitendo visivyozingatia maadili ili tuwachukulie hatua ama
kurekebisha na tuweze kutoa huduma yenye viwango na inayokubalika na
salama kwa wananchi".
0 on: " WAUGUZI NI CHACHU YA HUDUMA BORA NCHINI"