Dkt.Ndugulile akiongea na watumishi wa kituo cha afya Kibakwe nje ya kituo hicho
Dkt.Faustine Ndugulile Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akikagua fomu ya orodha ya dawa iliyofanywa na kituo hicho kwa mnunuzi wa nje na ile ya MSD kwenye stoo ya dawa ya kituo cha afya cha kibakwe.
Picha ya pamoja ya Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto pamoja na watumishi wa kituo cha afya Kibakwe wilayani Mpwapwa.
Na WAMJW-DODOMA
NAIBU
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile amemuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Said Mawjji
kuandaa maoteo ya mahitaji ya dawa mapema na kupeleka Bohari kuu ya
Dawa (MSD) kwa ajili ya upatikanaji huo na sio kununua dawa kiholela.
Hayo
ameyasema wakati wa ziara yake kwa ajili ya kuangalia miundo mbinu
pamoja na upatikanaji wa dawa na huduma za afya zitolewazo katika wilaya
ya Mpwapwa mkoani Dodoma aliyoifanya jana.
“Katika
milioni 57 ya kununua dawa laki saba tu ndo imeenda MSD zilizobaki
zimeenda kwa mshitiri mwingine ambapo ni uagizaji dawa kiholela kwani
mmeshindwa kufuata taratibu za uagizaji dawa wakati dawa hizo
zinapatikana MSD” alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha
Dkt. Ndugulile alimuagiza Dkt. Mawjji kuhakikisha upanikaji wa dawa zote
muhimu zinapatikana kwa asilimia 80 katika vituo vya afya wilayani hapo
kama ilivyofikiwa na MSD katika kusambaza dawa hapa nchini ili
kuondokana na tatizo la uhaba wa dawa ambapo ni kipaumbele cha Serikali
kwa uapande wa sekta ya afya nchini.
Dkt. Ndugulile
alimuagiza DMO wa Mpwapwa mpaka kufikia Desemba 13 mwaka huu awe tayari
amewasilisha nyaraka za uagizaji dawa zote kuanzia Julai 2017mpaka
Septemba mwaka huu ili kujiridhisha na utaratibu wao wa uagizaji dawa.
Mbali
na hayo Dkt. Ndugulile amemuagiza DMO huyo kujitahidi kuongeaa baadhi
ya watumishi katika kituo cha afya cha Kibakwe kilichopo katika tarafa
ya Kibakwe Wilayani Mpwapwa kwani wanahitajika watumishi akiwemo mtaalam
wa maabara na mfamasia wa kituo ili kuleta ufanisi katika huduma za
afya kituoni hapo.
Aidha Dkt. Ndugulile ameumbia
uongozi wakituo cha afya Kibakwe na pamoja na wanakijiji kuwa Serikali
imetenga milioni 500 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa jengo la
upasuaji wa dharura kwa akina mama wajawazito,nyumba za watumishi pamoja
na ununuzi wa vifaa tiba ili kuokoa maisha ya akina mama wanapopata
uzazi tata wakati wa kujifungua
Katika kituo hicho
cha afya Kibakwe Naibu Waziri huyo alikutana na changamoto ya tofauti ya
dawa kwenye fomu za kuagiza dawa MSD na zile za kununua dawa hizo kwa
mshitiri wa nje hali iliyomlazimu Dkt.Ndugulile kuanza kuhakikia fomu
moja kwa dawa moja hadi nyingine na kugundua ubadilishaji wa aina za
dawa zilizoagizwa MSD na baadae kwa mnunuzi wa nje.
Hata
hivyo Dkt.Ndugulile aliwakanya watumishi wa stoo ya dawa ya kituo hicho
kuacha kufanya mchezo huo wa kubadilisha mahitaji ya dawa pale
wanapokosa MSD na kiruhusiwa kununua nje kwani Serikali ya awamu ya tano
imejipanga na kuhakikisha upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya
kote nchi ni zaidi ya asilimia 80 na hivyo kuwataka wakazi wa Kibakwe
kusimamia kwa makini matumizi ya dawa kituoni hapo.
0 on: "DKT. NDUGULILE AMPA MAAGIZO DMO MPWAPWA."