Waziri wa Afya Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu Leo ametembelewa na ujumbe wa pamoja wa umoja wa Mataifa wa Mpango wa Kinga ya Saratani ya shingo ya Kizazi Duniani.
Waziri
Ummy ameushukuru ujumbe huko kwa kufika nchini na kwa kuichagua
Tanzania kuwa Moja ya nchi sita duniani zitakazo nufaika na Mpango huu
Tanzania
ni mojawapo wa nchi duniani zenye Tatizo ya saratani ya shingo ya
kizazi.katika wanawake 100,000 kuna wanawake 54 wenye tatizo hilo na
Vifo 32 katika wanawake 100,000 hiki ni kiwango kikubwa kwa nchi za
afrika mashariki(Globocan,2014)
Katika
hatua za kujikinga na hali hii Wizara ya afya inafanya kazi na wadau
mbalimbali wakiwemo Tanzania Youth Alliance (TAYOA),Medical Women
Association of Tanzania, Wanawake na Maendeleo (WAMA) ,Tanzania Network
for women living with HIV(TWN), Mbeya HIV network, T-Marc Tanzania na
vyombo vya habari vya kitaifa na kijamii katika kuhamasisha
kuishirikisha Jamii katika suala hili.
Wizara
inafanya kila jitihada kuhakikisha Mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na
kansa anapata matibabu ya kibingwa maalum ya mionzi katika Hosipiali za
Ocean Road na Bugando
0 on: "TANZANIA KUNUFAIKA NA MPANGO WA KINGA YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI"