Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta (DSC) Dkt. Andrew Komba ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika mkutano wa ufunguzi wa Mwongozo wa Taifa wa
Huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya Afya uliofanyika Mjini
Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha usafi wa Mazingira
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Stephen Kiberiti
akimkaribisha mgeni rasmi Dkt. Andrew Komba wa pili kutoka kushoto katika
mkutano wa ufunguzi wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa
mazingira katika vituo vya Afya.
Wadau wa masuala ya Afya na Usafi wa mazingira wakifuatilia
kwa ukaribu taarifa kutoka kwa mgeni rasmi (hayupo kwenye picha) katika mkutano
wa ufunguzi wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira katika
vituo vya Afya uliofanyika mapema leo Mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mipango WATERAN Tanzania Abel Dugango akisoma
taarifa fupi kuhusu huduma za maji na usafi wa mazingira mbele ya Viongozi wa
Wizara na Wadau wa Sekta ya Afya, shughuli inayoendelea Mjini Dodoma.
Mratibu wa Kampeni ya Kitaifa ya Usafi na Mazingira kutoka
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Anyitike Mwakitalima akitoa taarifa fupi
mbele ya wadau wa Afya katika mkutano wa ufunguzi wa Mwongozo wa Taifa wa
Huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya Afya uliofanyika Dodoma.
Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta (DSC) Dkt. Andrew Komba
akikata Utepe kuashiria ufunguzi wa Mkutano wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za
maji na usafi wa mazingira katika vituo vya Afya kulia ni mmoja wa waratibu wa
kampeni ya Usafi wa Mazingira.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Bumi Mwamasage akipokea
mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira kutoka kwa Mkurugenzi
wa Uratibu wa Sekta (DSC) Dkt. Andrew Komba ambae pia alikuwa mgeni rasmi wa
mkutano huo.
Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta (DSC) Dkt. Andrew Komba
akipokea vipeperushi vilivyoandaliwa kwaajili ya kutoa elimu kutoka kwa Salome
Mtenga.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta
(DSC) Dkt. Andrew Komba akiwa na Wadau wa masuala ya Afya katika mkutano wa
ufunguzi wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira katika
vituo vya Afya uliofanyika Dodoma.
NA WAMJW-DODOMA
Serikali kupitia
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imezindua mwongozo wa huduma za maji na usafi
wa mazingira katika vituo vya tiba ikiwemo zahanati, vituo vya afya na
hospitali ikiwa ni katika kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili
ya kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira iitwayo NIPO TAYARI.
Akiongea
wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Sekta Ofisi ya Rais Tamisemi, Dkt. Andrew
Komba amesema uzinduzi wa mwongozo huo ni katika kueleka awamu ya pili ya
kampeni ya NIPO TAYARI itakayozinduliwa rasmi na Makamu wa Rais,Mhe. Samia Suluhu Hassan ifikapo Desemba 7 mjini
Dodoma.
“Mwongozo
huo utasimamia na kutekeleza shughuli zinazohusiana na mazingira na umelenga
katika kutoa maelezo stahiki namna ambavyo vituo vya afya, ikiwemo ngazi za
chini mpaka juu ili maelekezo hayo yaweze kutumika katika upangaji wa mipango
na uandaaji wa bajeti zitakazotumika,” amesema Dkt. Komba.
Aidha,Dkt.
Komba amesema kuwa watanzania tunatakiwa kuzingatia usafi wa mazingira pamoja
kutumia vyoo bora ili kuweza kudumisha afya njema kwa maendeleo ya Tanzania.
Kwa upande
wake Mratibu wa Kampeni ya Kitaifa ya
Usafi ya Mazingira, Anyitike Mwakitalima amesema kuwa kampeni hiyo inalenga
kuwahamisha wananchi kuweza kutumia vyoo bora na mpaka kufikia Juni 2021 kaya zote nchini ziwe zinatumia vyoo.
“Kutokana na
kulegalega katika baadhi ya maeneo, waligundua kwamba kisababishi
kimojawapo ilikuwa ni ukosefu wa mwongozo wa taifa ambao wadau na serikali
ingeutumia kusimamia usafi wa mazingira kwahyo kampeni hii itahakikisha mpaka
kufikia 2025 kaya zote zinatumia vyoo vilivyo bora” alisema Bw. Anyitike.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Mipango kutoka Shirika la Water Aid, Abel Duganga
amesema kutokana na kukosekana kwa mwongozo huo unaopima hali ya maji nchini
utendaji wa serikali na wadau ulikuwa ukisuasua, lakini sasa
utawezesha kuwa na vigezo vinavyofanana katika kupima na kuwa na takwimu
sahihi.
0 on: "SERIKALI YAZINDUA MWONGOZO WA HUDUMA ZA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA"