Waziri wa Afy,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya wakazi
wa Kijiji Nyamwage cha wakati alipotembelea Kituo cha Afya cha Ikwiriri na
Zahanati ya Nyamwage katika ziara yake ya kuangalia utekelezaji unaofanyika
kupitia mpango wa malipo kwa ufanisi unaotekelezwa katika mikoa nane nchini.
Waziri wa
Afy,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi moja yam
zee kadi ya Afya ya matibabu bure kwa wazee wakati alipotembelea Kituo cha Afya
cha Ikwiriri na Zahanati ya Nyamwage katika ziara yake mapema jana.
Waziri wa
Afy,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongozana na Tabibu
mfawidhi wa Zahanati ya Nyamwage Agness Salvatory Kilapilo wakati wa ziara yake
ya kuangalia utekelezaji unaofanyika kupitia mpango wa malipo kwa ufanisi
unaotekelezwa katika mikoa nane nchini.
Waziri wa
Afy,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na baadhi
ya viongozi wa Kijiji cha Nyamwage (hawapo kwenye picha) wakati alipotembelea duka
la dawa katika Zahanati ya Nyamwage.
Waziri wa
Afy,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akifuatilia
matangazo katika mbao ya matangazo katika Zahanati ya Nyamwage wakati alipotembelea
Kituo cha Afya cha Ikwiriri na Zahanati ya Nyamwage katika ziara yake mapema
jana, pembeni yake ni Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Mhe. Juma Njwayo.
Waziri wa
Afy,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimpa maelekezo Tabibu
mfawidhi wa Zahanati ya Nyamwage Agness Salvatory Kilapilo wakati akikagua
Usafi wa Choo nkatika Zahanati hiyo.
Waziri wa
Afy,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisalimiwa na mtendaji kata wa kata ya Umwe baada ya akipokelewa
na Mkuu wa Wilaya Mhe. Juma Njwayo wakati wa ziara yake alipotembelea Kituo cha
Afya cha Ikwiriri na Zahanati ya Nyamwage.
Waziri wa
Afy,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu aliyebeba mtoto huku
akiwa ametabasamu akiwa na mama wa mtoto huyo Bi. Mwamvua wakati alipotembelea
wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya cha Ikwiriri, aliesimama ni Msimamizi wa Wodi ya Wazazi Gidion Stevene.
Waziri wa
Afy,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisikiliza jambo
kwa umakini kutoka kwa Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Mohammed Mchengerwa wakati
akijiandaa kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyamwage .
Picha ya
pamoja nikiongozwa na Waziri wa Afy,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
Ummy Mwalimu na Wazee wa Kijiji cha Nyamwage wakiwa wameshika kadi za matibabu
ya bure kwa wazee.
Na.WAMJW-Rufiji
Utekelezaji
wa mpango wa malipo kwa ufanisi(RBF) Wilayani Rufiji umeleta mabadiliko
makubwa katika Vituo vya afya na Zahanati kwa uboreshaji wa miundombinu
pamoja na upatikanaji wa dawa muhimu
Hayo
yamesemwa jana na Waziri wa Afy,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu wakati alipotembelea Kituo cha Afya cha Ikwiriri na
Zahanati ya Nyamwage katika ziara yake ya kuangalia utekelezaji
unaofanyika kupitia mpango wa malipo kwa ufanisi unaotekelezwa katika
mikoa nane nchini
Waziri
Ummy alisema mabadiliko hayo katika sekta ya afya yamefanyika katika
maeneo ya utoaji huduma,Uongozi na Utawala,Rasiliamaliwatu,Mifumo ya
usimamizibwa utoaji taarifa za afya,madawa na teknilojia ya afya ambapo
mfumo huo umesaidia maboresho, uwajibikaji,ufanisi na usawa kwani dhana
hiyo inamfanya mtoa huduma kulipwa kulingana na matokeo ya kazi yake
ambayo amehakikiwa na hivyo kucanya vituo hivyo kuweza kuongeza hali ya
upatikanaji wa dawa na kuboresha miundombinu ya vituo hivyo
"Tumeanza
mpango huu katika mikoa 8,tumefanya tathimini kwenye vituo vya afya na
zahanati zote za Mkoa wa Pwani ikiwemo Wilaya ya Rufiji,tukagundua vituo
vya afya na zahanati hazikuwa na viwango vya ubora unaogakiwa tukaona
tuwapatie shilingi milioni 10 kila kituo vilivyokidhi kwa ajili ya
kuboresha miundombinu"alisema Waziri ummy.
Hata
hivvyo aliipongeza kamati ya afya ya kijiji cha Nyamwage kwa kutumia
ipasavyo shilingi milioni 10 kwa kuongeza urefu wa paa na kupaua,kuweka
malumaru na kuongeza matundu ya choo pamoja na tundu moja la choo kwa
ajili ya walemavu"nikupongeze mganga mfawidhi kwa kuboresha zahanati hii
kwakweli unapaswa kupongezwa kwani umefanya vizuri ila badilika lugha
chafu kwa wananchi haitakiwi,nakupa mwezi mmoja ila kwa upande huu
mwingine umenifurahisa,mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni"
Aidha
,alitoa wito kwa wanawake kuhudhuria kliniki pale wanapohisi kuwa
wajawazito na hasa mahudhurio yote manne ili kuweza kujua hali zao
kiafya na kuweza kupata matibabu pale wanapogundulika na matatizo na
kujifungua salama"hatutaki kuona mwanamke mjamzito anafariki wakati wa
kujifungua,ndiyo maana serikali ya awamu ya tano imeboresha huduma za
afya na tumeanza ujenzi wa vyumba vya upasuaji wa dharura kwa mwanamke
atakayepata uzazi pingamizi,kujifungua salama ni haki ya kila mwanamke
mjamzito
Akisoma taarifa
ya Wilaya,Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Mhe.Juma Njwayo alisema mpango wa
malipo kwa ufanisi umeongeza idadi ya akina mama wanaojifungulia kwenye
zahanati na kutoka 3,382 mwaka 2016 hadi kufikia 4,086 mwaka 2017 na
wanawake wanaohudhuria mahudhurio manne kliniki wamefikia 3,955 mwaka
2017 kutoka 1,906 mwaka 2016.
"Hali
ya upatikanaji dawa muhimu hivi sasa ni asilimia 91 na dawa zingine ni
zaidi ya asilimia 50 na hii inachangiwa na mpango huu"alisema Mhe.
Njwayo.
Malipo kwa
ufanisi (RBF) wilayani Rufiji ulianza kutekelezwa mwaka 2016 kwa
kupatiwa shilingi milikni 240 kutoka wizara ya afya na kila kituo cha
afya ama zahanati kilipatiwa shilingi milioni 10 kwa ajili ya kuboresha
miundombinu na inatekelezwa kwenye vituo kumi na mbili ambavyo vilikidhi
vigezo vya mpango huo.
0 on: "MPANGO WA MALIPO KWA UFANISIWALETA MABADILIKO SEKTA YA AFYA RUFIJI."