Naibu Waziri Wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile aliyevaa shati la vyumbavyumba akikagua na kutoa
maelekezo juu ya upatikanaji wa dawa katika baadhi ya vituo vya afya
katika Wilaya ya Meru wakati wa ziara yake mkoani Arusha.
Naibu Waziri Wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile katikati akipata maelezo kutoka kwa mmoja ya
mtumishi wa Chuo Cha Maendeleo ya Jamii cha Tengeru (TICD) wakati
alipotembelea chuo hiko katika ziara yake mkoani arusha.
Baadhi ya Watumishi wa Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Tengeru TICD
wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri Wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia
,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani wakati
alipotembelea chuo hiko katika ziara yake mkoani Arusha.
Naibu Waziri Wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile katikati akionyeshwa mpaka wa Chuo Cha Maendeleo ya
Jamii Tengeru TICD wakati alipotembelea chuo hiko katika ziara yake
mkoani Arusha.
Naibu Waziri Wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile aliyevaa shati la vyumbavyumba akiwajulia hali baadhi
ya wagonjwa katika vituo vya afya katika Wilaya ya Meru wakati wa
ziara yake mkoani Arusha.
Naibu Waziri Wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile wa pili kulia akisikiliza maelezo kutoka kwa Mganga
Mkuu wa Wilaya ya Meru Dkt. Cosmas Kilasara wa kwanza kulia kwenye moja
ya jengo la Hospitali ya Wilaya ya Meru mkoani Arusha.
Naibu Waziri Wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile kulia akiongea na baadhi ya wanakijiji wa kata ya
Mbuguni wilayani Meru wakati wa ziara yake mkoani Arusha.
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Tengeru TICD wakitoa
chngamoto na maswali kwa Naibu Waziri Wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia
,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani wakati
alipotembelea chuo hiko katika ziara yake mkoani Arusha.
Na WAMJW- ARUSHA.
NAIBU Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile
amutaka uongozi wa Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Tengeru kuunda Bodi ya
chuo haraka iwezekenavyo ili kuleta maendeleo ya kitaaluma chuoni hapo.
Hayo
ameyasema wakati alipotembelea Chuo hiko leo katika ziara yake ya siku
mbili mkoani Arusha kwa ajili ya kuangalia hali ya upatikanaji wa huduma
za afya .
"Uongozi wa
chuo unatakiwa kuhakikisha unakuwa na bodi ya chuo pamoja na kuwa na
Mkuu wa chuo alithibitishwa kwani mpaka sasa hakuna mkuu wa chuo hiyo ni
hatari"alisema Dkt. Ndugulile
Aidha
Dkt. Ndugulile amesema kuwa uongozi wa chuo hiko hauna budi kuhakikisha
unamaliza tatizo la mipaka na kupata hati miliki ya kiwanja hiko kwani
inaweza kusababisha upokwaji wa kiwanja hiko.
Katika
ziara hiyo Dkt. Ndugulile alifanikiwa kutembelea Hospitali ya Wilaya ya
Meru na kujiridhisha na hali ya upatikanaji wa dawa na kuwasisitiza
wananchi wasiuziwe dawa zote muhimu.
Aidha
Dkt. Ndugulile ametembelea Kituo cha Afya Mbuguni na kuwapongeza
kutokana na kupeana elimu juu ya uzazi wa mpango kwa wanakijiji wote wa
kata hiyo na kufanya kupata huduma za afya kwa urahisi na kwa ufasaha.
"Ila
nataka niwaambie wanakijiji hata kama dawa zipo kwa asilimia 100 na
sisi ni lazima tujikinge na magonjwa yasioambukiza kwani yamekuwa tishio
kwa watanzania"alisema Dkt. Ndugulile
Aidha
Dkt. Ndugulile amepongeza viongozi wa Hospitali ya Meru na Kituo cha
afya Mbuguni Wilayani Meru kwa kupiga hatua katika kutokomeza vifo vya
mama na watoto.
0 on: "DKT.NDUGULILE AWATAKA TICD KUUNDA BODI MARA MOJA."