Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu kushoto akimsalimia mgonjwa aliyekuwa anasubiri huduma katika
Zahanati ya Segese wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala
wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa malipo wa
ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.
Baadhi ya Wanakijiji wa Kijiji cha Segese wakimsikiliza kwa makini
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu hayupo pichani wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya
Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa
malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya
msingi.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akikagua choo cha Zahanati ya Mhandu wakati wa ziara yake katika
Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa
mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya
ngazi ya msingi , aliyevaa suti nyeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama Bw.
Fadhil Mkuru.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu katikati akisisitiza jambo kuhusu upatikanaji wa dawa katika
Zahanati ya Mhandu wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala
wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa malipo wa
ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akifurahia jambo na baadhi ya wazee wa kijiji cha Segese wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu kushoto akimkabidhi kitambulisho cha matibabu bila ya malipo
mmoja wa wazee wa kijiji cha Segese Bibi. Shija Petro (60) kulia wakati
wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili
kuangalia utekelezaji wa mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya
kutolea huduma za afya ngazi ya msingi, Bibi huyo aliwawakilisha wazee
413 waliopata vitambulisho hivyo katika Halmashauri ya Msalala ambapo
lengo ni kuwafikia wazee742 kufikia Machi 2018.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu katikati akiangalia friji la kuhifadhia chanjo kwa ajili ya
watoto katika Zahanati ya Segese wakati wa ziara yake katika
Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa
mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya
ngazi ya msingi.
Na WAMJW-MSALALA
Waziri wa Afya,Maendeleo
ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto aweka historia kwa kutembelea Zahanati
ya Mhandu kata ya Chela Wilayani Msalala ambapo tangu Uhuru wa Tanzania
kijiji hicho hakijawahi kutembekewa na Kiongozi wa Kitaifa.
Waziri
Ummy Mwalimu yupo ziara ya kikazi Wilayani Msalala kujionea Utekelezaji
wa Mpango wa Malipo kwa Ufanisi(RBF) ambapo ulianza Januari 2016 kwa
Mkoa wa Shinyanga
RBFni Mpango wa malipo wa
ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi ambapo
vituo vinapewa maeneo ya utekelezaji na kupimwa kuona kama wamekidhi na
kufikiwa malengo hivyo kituo huhakikiwa na hatimaye kutolewa fedha
kulingana na matokeo ya idadi za huduma zilizotolewa na ubora kulingana
na miongozo ya utoaji wa huduma za Afya.
Fedha zinazopatikana zinafanya maboresho ya vituo ikiwemo miundombinu ya kituo,madawa na vifaa tiba
Waziri
Ummy Mwalimu ameipongeza halmashauri ya wilaya hiyo kwa kufanya vizuri
katika kutekeleza Mpango huo hata hivyo aliwataka watendaji kufanya
uhakiki na kujiridhisha kwamba huduma za Afya zitolewazo zinakidhi
viwango kulingana na miongozo ya Afya ndipo malipo yatolewe
Alisema
Mpango huo unahakikisha huduma ya Afya ya msingi zinatolewa bila
vikwazo,"nimekuja kufuatilia utekelezaji kwakweli nimefurahi kwani
mnatekeleza na mmeboresha huduma zenu"
Aidha,alisema
kabla ya utekelezaji wa Mpango huo kuanza mwaka 2015 hali ya
miundombinu ilikua mibovu,hakukuwa na dawa,hivyo kupitia Mpango huo
Serikali hupeleka fedha ambazo zinasaidia kuimarisha mifumo ya vituo vya
Afya,kuongeza huduma za huduma,kuchochea jamii kutumia vituo vya Afya
hususan wanawake wajawazito pamoja na kutoa motisha kwa wahudumu na
watumishi wa Afya katika vituo vya kutolea huduma.
"Mpango
huu tunataka wanawake wajawazito waje vituoni ndani ya miezi mitatu ya
mwanzo na serikali tunaleta shilingi 8290,na mjamzito akihudhuria
kliniki angalau Mara NNE wakati wa ujauzito tunaleta shilingi 6210
kwenye zahanati" alisema Waziri Ummy
Alitaja
kiasi cha shilingi 20,700 serikali inatoa kwa mjamzito akienda
kujifungua kwenye Zahanati hivyo alitoa ari kwa wanawake wajawazito
wilayani Msalala kuacha kwenda kujifungua kwa wakunga wa jadi kwani
Serikali ya awamu ya tano imeboresha huduma za Afya nchini ikiwemo hali
ya upatikanaji wa dawa ambapo Msalala kwa mwaka wa fedha 2017/2018
wametengewa shilingi milioni 417 tofauti na ile ya mwaka 2015/2016 ya
shilingi milioni 108.
0 on: "MH. UMMY(MB) AWEKA HISTORIA KATIKA ZIARA YA ZAHANATI YA MHANDU KATA YA CHELA WILAYANI MSALALA. "