Ijumaa, 31 Januari 2020
WAFAMASIA WATAKIWA KUFUATA MISINGI YA KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI
Ijumaa, Januari 31, 2020
-
Maoni 1
Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula akimkabidhi mmoja wa wahitimu wa kada ya Famasi cheti cha taaluma pamoja na usajili katika warsha iliyofanyika jijini Dodoma. |
Na Emmanuel Malegi- Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula amewasihi
wahitimu wa kada ya famasi kutoka vyuo mbalimbali nchini na nje ya nchi
kuheshimu na kufuata misingi na miongozo ya taaluma hiyo ili kuweza kutoa
huduma bora kwa wananchi.
Dkt. Chaula amesema hayo mapema leo wakati alipohudhuria
warsha fupi ya kuwatunuku vyeti vya kuhitimu na usajiri wahitimu zaidi ya 100
waliohitimu shahada ya Famasi katika vyuo mbalimbali nchini.
“Ninaomba mkawe wanyenyekevu mkiwa maeneo yenu ya kazi,
kuzingatia kanuni na misingi ya taaluma ni jambo muhimu la kufuata kwa kila
mmoja wetu, nidhamu mahala pa kazi huleta umakini katika kazi yako, jamii
inawategemea ili muweze kutoa huduma nzuri kwa wananchi”. Amesema Dkt. Chaula.
Dkt. Chaula ameendelea kusisitiza kuwa taaluma hiyo ni
muhimu sana nchini kwani wagonjwa wanategemea kupata dawa sahihi ambazo zitatolewa
na wafamasia hao ili ziwasaidie kupona maradhi yanayowasumbua.
Aidha, Dkt. Chaula amewataka Wahitimu hao kushirikiana kwa
karibu na madaktari pamoja na wahudumu wengine wa afya wakiwemo manesi ili
waweze kusaidia katika kutoa huduma bora za afya na kusaidia wananchi kupata
nafuu na kupona kabisa maradhi yanayowasumbua.
Kwa upande wake Msajili wa Baraza la Famasi nchini Bi.
Elizabeth Shekalaghe amewataka wahitimu hao kwenda kuisaidia jamii na kuziba
baadhi ya mapengo ya taaluma hiyo ambayo ina watumishi wachache na uhitaji ni
kubwa nchini ambapo hivi sasa Tanzania ina wafamasia takribani 1200
waliosajiliwa na Baraza hilo nchi nzima.
Jumatano, 29 Januari 2020
TANZANIA HAINA MGONJWA WA CORONA
Jumatano, Januari 29, 2020
-
Hakuna maoni
Na. WAMJW-Dodoma
Mpaka sasa Tanzania haina Mgonjwa wala muhisiwa wa ugonjwa unaosababishwa na kirusi cha Coromna (Hona kali ya mafua) hata hivyo kutokana na mwingiliano mkubwa uliopo hasa kibiashara na kijamii kati ya Tanzania na nchi za bara la Asia ikiwemo nchi ya China nchi inakuwa katika hatari pia ya ugonjwa huo.
Haya yamesemwa leo na Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akitoa tarifa kwa umma kuhusu mwenendo wa ugponjwa huo jijini hapa.
“Ugonjwa huu unasababiswa na kirusi jamii ya Corona na ni kipya “Novel (New) Corona virus 2019” (2019-nCOV) ambacho ni tofauti na virusi vingine vya jamii hiyo ambavyo viliwahi kusababisha milipuko ya ugonjwa uliojulikana kama ‘SARS-CoV’ mwaka 2003 na MERS-CoV Corona Virus mwaka 2013”.Amesema Waziri Ummy.
Aidha, waziri Ummy amesema ugonjwa huo huambukizwa kwa njia ya hewa kwa kuingiwa na majimaji yenye virusi kutoka mtu mmoja kwa njia ya kukohoa au kupiga chafya au kwa kugusa majimaji au makamasi kutoka kwa mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na dalili za ugonjwa huo na dalili huanza kuonekana kati ya siku moja hadi kumi na nne tangu kupata maambukizo.
Hata hivyo ametaja dalili za ugonjwa huu ni pamoja na Homa, mafua, kuumwa kichwa, mwili kuchoka, kikohozi, kubanwa mbavu, maumivu ya misuli, vidonda vya koo, mapafu kuathirika, kupumua kwa shida na hata kifo.
“Ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba ya moja kwa moja, hivyo kama yalivyo magonjwa mengine yanayosababishwa na virusi, matibabu hufanyika kwa kuzingatia dalili zilizopo na ufuatiliaji wa karibu” Amesisitiza Waziri Ummy.
Wakati huo huo waziri huyo amewashauri wananchi kuchukua hatua ili kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo kuzingatia kanuni za afya na usafi ikiwa ni pamoja na kukaa mbali na mtu mwenye dalili za mafua mwenye historia ya kusafiri katika nchi zilizokumbwa na mlipuko na kufunika mdomo na pua wakati wa kukohoa kwa kitambaa safi au nguo uliyovaa sehemu za mikono
“Kutokana na mwenendo na kasi ya kusambaa kwa ugonjwa huo kipindi hiki cha mlipuko, Wizara inashauri kusubiri na kuepuka safari zisizo za lazima kwenda kwenye maeneo yaliyoathirika na inapolazimu kusafiri basi wapate maelezo ya kitaalamu kabla ya kuondoka nchini pamoja na kuepuka kugusana na mgonjwa mwenye dalili za magonjwa ya njia ya hewa”.
Vile vile wananchi wanatakiwa kutoa taarifa ya uwepo wa mtu mwenye dalili zinazohiswa kuwa za ugonjwa huu kwenye kituo cha huduma za afya kilicho karibu nawe au piga simu namba 0800110124 au 0800110125 bila malipo.
-Mwisho_
Jumapili, 26 Januari 2020
KINU CHA KUFUA OKSIJENI KCMC KUWA MSAADA KWA WENYE MATATIZO YA UZAZI
Jumapili, Januari 26, 2020
-
Hakuna maoni
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) Dkt. Sarah Urasa akizungumza katika Mkutano wa Maafisa Habari wa Wizara ya Afya na Taasisi zake katika kampeni ya "TumeboreshaAfya".
Bibi Catherine Mushi akiendesha kinu cha kuzalisha hewa safi (Oxygen plant) katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC.
Mtaalam wa kutengeneza baskeli za magurudumu matatu(wheelchair) Bw. Samson Shirima akiwa katika kiwanda cha kuzalisha bidhaa hizo katika hospitali ya rufaa ya KCMC.
Madaktari pamoja na wauguzi wakiwahudumia watoto njiti katika wodi maalum ya watoto hao KCMC.
Mtaalam kutoka Idara ya ngozi Bw. Maghembe Juma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kilimanjaro KCMC akitengeneza dawa na mafuta maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi katika Hospitali hiyo.
Grace Manyika akiweka alama za ukomo wa matumizi ya mafuta maalum kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) katika kiwanda hicho kilichopo hospitali ya KCMC, Kilimanjaro.
Mtambo wa kinu cha kisasa cha kuzalisha hewa safi (oxygen plant)wenye uwezo wa kuzalisha mitungi 400 kwa siku ambao upo katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya kaskazini KCMC.
KCMC
KINU CHA KUFUA OKSIJENI KCMC KUWA MSAADA KWA WENYE MATATIZO YA UZAZI
Na Mwandishi wetu, KILIMANJARO.
IMEELEZWA kuwa uwepo wa kinu kipya na cha kisasa chenye uwezo wa kufua hewa ikiwemo hewa safi ya Oxygen na ile ya Naitrojeni kitakuwa msaada kwa wenye tatizo la uzazi nchini.
Akizungumzia hospitalini hapo ikiwa ni utekelezaji wa kampeni ya Tumeboresha sekta ya Afya yenye lengo la kuonyesha mafanikio makubwa yaliyopatikana katika uwamu ya tano ndani ya Wizara ya afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Kaimu Mkurugenzi wa KCMC Dkt. Sarah Urasa alisema:
"Uhifadhi wa mbegu za kiume na kike upo mbioni kuanza hapo baadae. Hatua hiyo kwani tayari tumeanzisha klininiki maalumu kwa ajili ya watu wenye matatizo ya uzazi ambayo tunaonana na wagonjwa kwa wiki mara moja ambapo huwahudumia watu 10 mpaka 12." Alisema.
Mbali na kazi hiyo kinu hicho kinauwezo wa kufua hewa ya Oksijeni ambayo kwa kiwango kikubwa hutumika kuwasaidia watu wenye matatizo ya kupumua ambapo kwa siku mitungi 400 hufuliwa katika kinu hicho.
Dkt. Sarah Urasa aliongeza kuwa: "Hii ni hospitali ya kwanza kuwa na kinu ya kufua hewa ya oksijeni na Nitrogen hapa nchini.
Hewa ya Oksijeni pia inatumika kwa wale wagonjwa wanaopewa dawa za usingizi kwaajili ya upasuaji, hewa ya nitrogen inatumika kuhifadhi sampuli kutoka kwa wagonjwa,tiba kwa magonjwa ya ngozi vile vile hutumika kukata matokeo kwenye ngozi au kwenye viungo vya uzazi" alisema.
Huduma hiyo ambayo imeanza mwaka huu Dkt. Sarah alisema ununuzi wa mitungi ya gesi ya oksijeni pekee ulikuwa ukiwagharimu takribani milioni tatu kwa wiki huku gharama za usafirishaji ikiwa haijajumuishwa hatua ambayo imeokoa gaharama za uendeshaji hospitalini hapo.
Dkt.Sarah alieleza kuwa kwa kadiri uzalishaji unavyoongezeka katika kinu hicho wataanza kutumia mfumo wa kuunganisha gesi moja kwa moja hadi katika kitanda cha mgonjwa.
"Tumeona uharibifu mkubwa unaotokana namitungi hii ya gesi sakafu yetu imekuwa ikiharibika kutokana na uzito wa mitungi yenyewe kwahiyo mfumo tutakapkuja kuutumia utakuwa bora zaidi tofauti na sasa "alisema.
Mafanikio mengine aliyoyataja Dk.Sarah alisema katika utawala wa Rais Dk.John Magufuli wamefanikiwa kuanza kutengeneza maji tiba 'dripu' kwaajili ya kuwasaidia wagonjwa ndani na nje ya hospitali.
"Hii inetusaidia kwa kiwango kikubwa hata hospitali zingine zimekuwa zikifika hapa kwaajili ua kujifunza namna ya kutengeneza maji tiba "alisema.
Pia alisema KCMC ndio kituo pekee inayotambulika kimaitafa kutoa mafunzo ya magonjwa ya ngozi na zinaa kwa nchi zote za Afrika Mashariki.
"Kituo hiki ndio kinachozalisha mafuta ya ngozi kwaajili ya watu wenye ualbino na tayari tumeingia makubaliano na Bohari kuu ya Dawa MSD kwaajili ya kusambaza dawa na tayari tumefikia mikoa 25 kwa kutumia mfumo wetu wa usambazaji na sasa MSD watatuongezea nguvu ili kusambazwa nchi mzima "alisema
Kwa upabde wake, Mhandisi KCMC Dustan Kanza alisema mgonjwa mmoja hutumia mtungi mmoja lengo kuepukana na maambukizi.
Alisema katika kinu hicho kwa saa 24 inauwezo wa kuzalisha mitungi 400 na mpaka sasa tayari zaidi ya mitungi 600 imezalishwa tangu kuanza kufanya kazi kwa kinu hicho januari mwaka huu.
Mwisho.

Ijumaa, 24 Januari 2020
HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA YATAKIWA KUJIUNGA NA TIBA MTANDAO
Ijumaa, Januari 24, 2020
-
Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akionyesha mashine ya kufanyia uchunguzi wa matiti ijulikanayo kwa jina la Mamograhy katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa kwenye kwenye chumba cha kipimo cha CT-Scan kwenye hospitali hiyo
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa kwenye wodi ya wagonjwa walioupandikiza
Na. Catherine Sungura-Dodoma
Hospitali ya Benjamin Mkapa imetakiwa kujiunga na tiba mtandao ili kuweza kutoa tiba kwa wagonjwa kwa haraka na kwa ufanisi ili kuwapunguzia wagonjwa muda wa kusubiri majibu hususani ya mionzi .
Rai hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati alipoitembelea hospitali hiyo kujionea hali ya utoaji huduma.
“Nawaelekeza ni vyema mkajiunga na huduma ya tiba mtandao ili muweze kutoa huduma kwa haraka na kwa ufanisi zaidi, mnatakiwa mkajifunze huduma hii kutoka hospitali ya Muhimbili au MOI". Amesema waziri Ummy.
Aidha, Waziri huyo amesema kuwa hivi sasa kwenye hospitali nyingi kuna changamoto za wataalam wa kusoma picha kwani wataalam wengi waliopo ni wale wa kupiga ”bahati nzuri sisi tunao wataalam wengi wa kupiga picha mana kwenye mionzi kuna aina mbili za wataalam wapo wa kupiga picha (radiographer) na wa kusoma picha, hivyo serikali itahakikisha inapata wataalam wengi zaidi wa kusoma ili kukidhi mahitaji.
Waziri Ummy amesema wizara ina lengo la kuziunganisha hospitali za wilaya pamoja na vituo vya afya kwenye mfumo wa hospitali za rufaa za mikoa kwa kufunga senta zitakazosaidia hospitali za wilaya na vituo vya afya vinavyofanya vipimo vya ‘utra sound’ na ‘x-ray’ na majibu yakasomwa haraka na wataalam wa Hospitali za rufaa na kutoa majibu haraka bila kumsubirisha mgonjwa kwa muda mrefu.
Alitaja hospitali zilizojiunga na tiba mtandao ni pamoja na hospitali za rufaa za mikoa ya Lindi na Morogoro , pia hospitali teule za wilaya za Nyangao,Turiani na hospitali za wilaya ya Nachingwea,kilosa na Mvomero.
Wakati huo huo Waziri Ummy ameitaka hospitali hiyo kupunguza gharama za kulipia uchunguzi wa saratani ya matiti kwa wanawake kutoka elfu sabini hadi elfu thelathini kama hospitali zingine za taifa zinavyofanya.
Hata hivyo waziri huyo ametoa wito kwa wananchi wa Dodoma na mikoa jirani kutosafiri hadi dar es salaam kupata huduma za kibingwa kwani huduma zote karibu zinapatikana hapo na hivyo ameahidi wizara wataleta madaktari bingwa wa mishipa ya fahamu pamoja na mifupa.
_Mwisho-
NIMR YATENGA MILIONI 800 TIBA YA MITISHAMBA NCHINI
Ijumaa, Januari 24, 2020
-
Hakuna maoni
Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof. Yunus Mgaya akisisitiza jambo wakati wa kikao na Maafisa Habari wa Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Waandishi wa Habari kilichofanyika katika ofisi za Taasisi hiyo Muhimbili, Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kituo cha Muhimbili Prof. Mfinanga akieleza jambo wakati wa kikao na Maafisa Habari wa Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Waandishi wa Habari kilichofanyika katika ofisi za Taasisi hiyo Muhimbili, Jijini Dar es Salaam.
Msanifu wa Maabara ya NIMR-Muhimbili Said Omary akielezea namna vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu vinavyokuzwa kwenye utafiti.
Kikao cha Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR)
Prof. Yunus Mgaya na Maafisa Habari
wa Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Waandishi wa Habari
kilichofanyika katika ofisi za Taasisi hiyo Muhimbili, Jijini Dar es
Salaam.
Maafisa Habari
wa Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Waandishi wa Habari,
NIMR YATENGA MILIONI 800 TIBA YA MITISHAMBA NCHINI
Na WAMJW - DSM
TAASISI ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imesema ipo mbioni kusimika mitambo ya kisasa itakayosaidia kuzalisha dawa za mitishamba kutoka miti dawa ili kukabiliana na magonjwa mbalimbali nchini.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa NIMR, Profesa Yunus Mgaya wakati akizungumza katika ziara ya 'Tumeboresha Sekta ya Afya' inayoendeshwa na Maafisa Habari waandamizi wa Wizara ya Afya na Taasisi zake.
Maofisa Habari hao wapo katika ziara ya Kampeni iitwayo Tumeboresha Sekta ya Afya ambayo inalenga kuonesha mafanikio yaliyopatikana katika sekta hiyo kipindi cha Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli
Alisema Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Afya imetoa fedha shilingi Milioni 800 ambazo zitasaidia kununulia mitambo na kukarabati eneo itakaposimikwa mitambo hiyo.
"NIMR tupo mbioni kuleta mitambo kutoka China. mitambo ambayo itatoa uwezo wa kuzalisha dawa kutoka kwenye miti dawa kwa ajili ya kuongeza uwezo wa kukabiliana dhidi ya magonjwa mbalimbali ambayo yanawagusa wananchi."
"Watalaam wetu tayari wameshaenda China kujifunza na pia wametembelea kampuni za mitambo hiyo ya kisasa na tumejiridhisha.
Mtambo mmoja unagharimu kati ya shilingi za kitanzania Milioni 500 hadi milioni 600 hivyo milioni 800 zitatosha kabisa kukamilika zoezi zima" alisema.
Pia alisema kuwa, dawa hizo zitatokana na miti dawa mbalimbali ikiwemo na kwa Waganga hapa nchini.
"Sisi tutatengeneza dawa kutokana na asili ya miti dawa.Tunachokifanya ni kutafiti. Baada ya kwenda kwa Mganga ambaye atakumiminia kwenye kikombe, Sisi tutakachokuambia ni kuwa dawa hiyo inamchanganyiko wa kiambata fulani na utaitumia kwa kiwango fulani." Alisema.
Aidha, alisema katika tiba ya mitishamba Duniani inatumika kwa wingi katika nchi mbili pekee ikiwemo China na India.
"China na India kuna Hospitali kabisa zinatibu kwa kutumia dawa za mitishamba na Nchi ya Korea pia" Alisema Profesa Mgaya.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa NIMR kituo cha Muhimbili, Profesa Sayoki Mfinanga alieleza kuwa miongoni mwa mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya tano ni pamoja na kuongezeka kwa tafiti kutoka 10 hadi 20 kwa mwaka.
"NIMR-Muhimbili tumefanikiwa kufanya tafiti mbalimbali kwenye magonjwa ya Kifua kikuu, Vimelea vya Ukimwi na Magonjwa yasiyoambukiza (Non Communicable Diseases).
"Uwezo wa kituo wa kufanya tafiti umeongezeka kutoka wastani wa tafiti kubwa 10 kwa mwaka kwenye miaka ya nyuma ya 2010 mpaka wastani wa tafiti kubwa 20 kwenye miaka ya kuanzia 2017." Alisema Profesa Mfinyanga.
Ambapo alibainisha kuwa, miongoni mwa tafiti hizo ni pamoja zile za huduma za kudhibiti Ukimwi na Kifua Kikuu.
"Tafiti hizi kupitia NIMR-Muhimbili zimechangia kuboresha au kutoa taarifa zilizoboresha huduma za kudhibiti UKIMWI na kifua kikuu.
"NIMR-Muhimbili imekamilisha utafiti uliotathimini mkakati tiba kwa kupunguza vifo kwa wagonjwa wenye maambukizi ya fangasi (Cryptococcus Neofroman) na kusababisha homa ya Uti wa mgongo (Cryptococcal meningitis) kwa wagonjwa walioathirika na Ukimwi.
Utafiti huu umehusisha wagonjwa 721 toka Tanzania, Malawi, Zambia, na Cameroon. "Alisema profesa Mfinanga.
Aidha, katika ziara hiyo pia wanahabari na maafisa hao wa Wizara ya Afya waliweza kitembelea Maabara kubwa ya NIMR -Muhimbili na kujionea jinsi inavyofanya kazi huku wakishuhudia vifaa na mashine za kisasa kabisa zenye ubora na ufanisi wa hali ya juu.
NIMR ilianzishwa kwa sheria ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Namba 23 ya mwaka 1979. NIMR ni taasisi iliyo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto huku kazi yake kubwa ni pamoja na kufanya utafiti, inaratibu, inakuza na kusimamia tafiti za afya zinazofanyika nchini na kukuza matumizi ya matokeo ya tafiti hizo.
Ambapo pia hadi sasa ina idara ya tafiti za Tiba Asili ambayo jukumu lake ni kufanya utafiti juu ya dawa za miti-shamba, ambazo nyingine zimekuwa zinatumika miaka mingi na bibi na babu zetu.
Mwisho

Jumanne, 21 Januari 2020
"HUDUMA ZA AFYA KWENYE HOSPITALI ZA RUFAA ZA MIKOA ZIMEIMARIKA" - DKT.CHAULA
Jumanne, Januari 21, 2020
-
Hakuna maoni
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula akifafanua jambo wakati wa kakao cha Kamati ya Bunge Huduma na Maendeleo ya Jamii
Na. WAMJW-Dodoma
Wizara ya afya,Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto –Idara kuu Afya imeendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za kibingwa kwenye mazingira karibu na wananchi kwenye hospitali zake za rufaa za mikoa hapa nchini
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Zainabu Chaula wakati akijibu maswali kutoka kwa wajumbe wa kamati ya ya kudumu ya Bunge na huduma na maendeleo ya jamii jijini hapa.
“Katika kipindi cha Julai hadi Novemba 2019 hospitali za rufaa za mikoa 18 zilitoa huduma za mkoba katika fani za kibingwa na hii ni katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya karibu na wananchi”.Alisema Dkt. Chaula
Alizitaja huduma za mkoba za kibingwa zilizotolewa ni pamoja na magonjwa ya macho,watoto ,dawa za usingizi,upasuaji wa kawaida,afya ya uzazi na magonjwa ya wanawake.
“Zipo huduma zingine ambazo wananchi walinufaika nazo ikiwemo ya upasuaji wa mishipa ya fahamu na ubongo,sikio,pua na koo,radiologia,afya ya akili,afya ya kinywa na meno pamoja na tiba ya ngozi na huduma za tiba kwa mazoezi”.
Hata hivyo alisema katika kliniki hizo jumla ya wagonjwa 13,107 walihudumiwa kati yao wagonjwa 1,762 walifanyiwa upasuaji.
Kwa upande mwingine Dkt. Chaula alisema jumla ya wagonjwa 2,194,738 walihudumiwa katika hospitali 28 za rufaa za mikoa ambapo wagonjwa wa nje (OPD) walikuwa 1,891, 713 na wagonjwa wa kulazwa (IPD) walikuwa 303,025 katika kipindi cha julai hadi desemba 2019.
-Mwisho-
Jumatatu, 20 Januari 2020
ASILIMIA 74 YA WAJAWAZITO WANAJIFUNGULIA KWENYE VITUO VYA AFYA
Jumatatu, Januari 20, 2020
-
Hakuna maoni
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa wizara kwa kipindi.cha
julai.hadi.desemba 2019 kwa kamati ya Bunge ya huduma na maendeleo ya
jamii
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii Mhe. Peter Serukamba akiongea wakati wa kikao hicho
Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Benard Konga akiwasilisha taarifa ya utendaji wa mfuko huo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula akifuatilia taarifa iliyowasilishwa na Waziri wa Wizara yake Mhe.Ummy Mwalimu
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha kamati ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii
Na.WAMJW-Dodoma
Jumla ya wajawazito 813,923 sawa na asilimia 74 wamejifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma huduma za afya nchini.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa wizara kwa kipindi cha julai hadi desemba 2019 kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii
"Katika kipindi hiki matarajio yalikua ni wajawazito 1,100,000 wangejifungua,hata hivyo takwimu zinaonesha kuwa jumla ya wajawazito 813,923 sawa na,asilimia 74 walijifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma"Amesema Ummy Mwalimu.
Kwa upande wa wajawazito waliofanya mahudhurio ya kliniki,Waziri huyo amesema kuwa jumla ya wajawazito 797,803 sawa na asilimia 73 ya walengwa walifanya mahudhurio ya kliniki manne na zaidi kama mwongozo ulivyoelekeza.
Aidha, amesema kuwa asilimia 87.4 ya wajawazito sawa na akinamama 886,810 walipatiwa dawa za kukinga Malaria na jumla ya dozi 2,844,174 sawa na asilimia 84.6 walipewa dawa ya kuzuia upungufu wa damu(FEFOL).
Hata hivyo Waziri Ummy amesema,kuwa wizara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ilihakikisha dawa muhimu za kuzuia na kutibu kifafa cha mimba na kukinga na kutibu kupoteza damu baada ya kujifungua,kutibu magonjwa na,watoto chini ya miaka mitano uliimarika kwa zaidi ya asilimia 85.
SERIKALI YAENDELEA KUIMARISHA MIKAKATI YA KUDHIBITI MAGONJWA YA MLIPUKO.
Jumatatu, Januari 20, 2020
-
Hakuna maoni
Baadhi ya miundombinu ya ndani, katika kituo cha tiba ya magonjwa ya mlipuko Buswelu Mwanza.
Na Rayson Mwaisemba, WAMJW- KILIMANJARO, MWANZA
Wananchi wametakiwa kuondoa hofu, pindi wakikutana na magonjwa ya mlipuko au mhisiwa mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola.
Wito huo umetolewa na Mhandisi Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Francis Mbuya wakati wa kukabidhi majengo ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Ebola Mkoani Mwanza na Kilimanjaro.
"Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea na jitihada za kuimarisha mikakati ya kudhibiti magonjwa ya milipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola na Kipindupindu,hivyo mnapo muhisi mtu ana dalili,toeni taarifa" Amesema Mhandisi Mbuya
Aidha, Amesema kuwa Wizara ya Afya, imekuwa ikitekeleza ujenzi wa miradi mbali mbali nchini ya ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za Afya katika Hospitali mbali mbali za Rufaa nchini pamoja na za kanda lengo ni kupambana na magonjwa aina yoyote ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola na Kipindupindu.
"Miradi hii imejengwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali ya Mawenzi Mkoani Kilimanjaro na Buswelu Mkoani Mwanza inalenga kupambana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola na Kipindupindu.
Miradi yote miwili (Buswelu Mwanza na Mawenzi Kilimanjaro) imegharimu jumla ya shilingi Bilion 2.2 kutoka Milion 897 iliyotengwa kwa kila mradi, hii ni kutokana na maboresho yaliyofanyika katika miradi hiyo ili kuweza kutoa huduma bora kwa Wananchi.
"Kwa Buswelu mradi umegharimu kiasi cha shilingi Billion 1.1 kutoka Milion 897 iliyotengwa, hii inatokana na sababu ya maboresho kutoka na kutembelewa na Wataalamu mbali mbali kutoka Bank ya Dunia ili kuhakikisha tunakuwa na viwango ambavyo vinakubalika kimataifa, sawa na mradi wa Mawenzi Kilimanjaro", alisema.
Mbali na hayo, Mhandisi Mbuya amewaasa Watumishi wa Hospitali kuhakikisha wanatunza miundombinu ya vituo hivi katika kipindi chote cha kutoa huduma, ambavyo umeigharimu Serikali pesa nyingi.
Mwisho.
Moja kati ya kituo cha tiba ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola na Kipindupindu chenye thamani ya shilingi Bilion 1.1 kilichomalizika na kukabidhiwa kwa Serikali, kilichopo Mawenzi Kilimanjaro.
Nyumba ya Mtumishi katika Kituo cha tiba ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola
na Kipindupindu.
Kituo cha tiba ya Magonjwa ya mlipuko kilichokabidhiwa kwa Serikali baada ya kumalizika, kilichopo Buswelu, Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza chenye thamani ya shilingi Bilion 1.1.
Na Rayson Mwaisemba, WAMJW- KILIMANJARO, MWANZA
Wananchi wametakiwa kuondoa hofu, pindi wakikutana na magonjwa ya mlipuko au mhisiwa mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola.
Wito huo umetolewa na Mhandisi Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Francis Mbuya wakati wa kukabidhi majengo ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Ebola Mkoani Mwanza na Kilimanjaro.
"Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea na jitihada za kuimarisha mikakati ya kudhibiti magonjwa ya milipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola na Kipindupindu,hivyo mnapo muhisi mtu ana dalili,toeni taarifa" Amesema Mhandisi Mbuya
Aidha, Amesema kuwa Wizara ya Afya, imekuwa ikitekeleza ujenzi wa miradi mbali mbali nchini ya ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za Afya katika Hospitali mbali mbali za Rufaa nchini pamoja na za kanda lengo ni kupambana na magonjwa aina yoyote ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola na Kipindupindu.
"Miradi hii imejengwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali ya Mawenzi Mkoani Kilimanjaro na Buswelu Mkoani Mwanza inalenga kupambana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola na Kipindupindu.
Miradi yote miwili (Buswelu Mwanza na Mawenzi Kilimanjaro) imegharimu jumla ya shilingi Bilion 2.2 kutoka Milion 897 iliyotengwa kwa kila mradi, hii ni kutokana na maboresho yaliyofanyika katika miradi hiyo ili kuweza kutoa huduma bora kwa Wananchi.
"Kwa Buswelu mradi umegharimu kiasi cha shilingi Billion 1.1 kutoka Milion 897 iliyotengwa, hii inatokana na sababu ya maboresho kutoka na kutembelewa na Wataalamu mbali mbali kutoka Bank ya Dunia ili kuhakikisha tunakuwa na viwango ambavyo vinakubalika kimataifa, sawa na mradi wa Mawenzi Kilimanjaro", alisema.
Mbali na hayo, Mhandisi Mbuya amewaasa Watumishi wa Hospitali kuhakikisha wanatunza miundombinu ya vituo hivi katika kipindi chote cha kutoa huduma, ambavyo umeigharimu Serikali pesa nyingi.
Mwisho.
Jumamosi, 18 Januari 2020
HOSPITALI YA MUHIMBILI - MLOGANZILA KUJENGA KITUO CHA UPANDIKIZAJI VIUNGO VYA BINADAMU DSM
Jumamosi, Januari 18, 2020
-
Hakuna maoni
Naibu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dkt.
Julieth Magandi (katikati) akitoa taarifa wakati wa ziara ya maafisa habari kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake katika kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya.
Baadhi
ya Maofisa habari na wanahabari wakifuatilia Naibu Mkurugenzi wa
Hospitali hiyo(hayupo pichani) wakati akitoa taarifa ya maboresho
yaliyofanywa katika hospitali ya Muhimbili Mloganzila
Muuguzi Rose Chasuka akielezea namna mashine ya kupima mapafu inavyofanya kazi wakati wa ziara hiyo.
Mmoja
wa wanahabari akiwa kwenye mashine ya kupima mapafu akionesha namna ya
mashine hiyo inavyofanya kazi wakati wa ziara hiyo. Mashine hiyo ni
miongoni mwa mashine pekee hapa nchini.
Mtaalam kutoka kitengo cha Radiolojia MNH-Mloganzila, Dkt. Ahmed Sauko akionyesha namna mashine ya MRI inavyofanya kazi |
Na Mwandishi wetu - Dar Es Salaam
Hospitali
ya Rufaa ya Taaluma na Tiba ya Mloganzila (MAMC) inatarajia kujenga
kituo cha Umahiri cha upandikizaji Viungo (Centre of Excellence for
Organ Transplant ) kitakachosaidia kupunguza gharama kwa Watanzania
walizokuwa wakizifuata nje ya Nchi.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila, Dkt.Julieth Magandi amesema hayo leo wakati wa ziara ya Maafisa habari wa Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Taasisi zake katika muendelezo wa kampeni ya kutangaza mafanikio ya Serikali ya awamu ya Tano inayojulikana kama ‘TUNABORESHA SEKTA YA AFYA’.

Dkt. Magandi
amebainisha kuwa, tayari bajeti ya fedha imetengwa na Serikali ya Awamu
ya Tano na kinatarajiwa kujengwa katika eneo jirani na Hospitali hiyo ya
Mloganzila.
“Katika mwaka wa fedha 2019/2020 Serikali imetenga fedha kiasi cha Tsh. Bilioni 8 kwa ajili ya uanzishwaji wa kituo cha Umahiri cha Upandikizaji viungo.
Kitaalamu tunaita ‘Centre Excellence for Organ Transplant’ na vitu vingi vitapandikizwa hapa” alisema Dkt. Magandi.

Amevitaja
viungo ambavyo vitapandikizwa katika kituo hicho kitakapokamilika ni
pamoja na Upandikizaji wa Ujauzito (In Vitro fertilization-IVF)
kupandikiza Uloto (Bone marrow), upandikizaji wa Ini (Liver Transplant),
Macho (Corneal transplant), Figo (Kideney transplant).
pamoja na kituo cha wataalam kujifunzia (Skills lab).
Aidha, akielezea mipango iliyopo ya hospitali hiyo ni pamoja na ujio wa huduma ya upandikizaji Uloto (Bone marrow transplant) huduma ambayo itaanza kutolewa kwa mara ya kwanza hapa nchini.

“Katika maboresho na kuongeza huduma kwa Watanzania. Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na Muhimbili-Upanga tunatarajia kuanzisha huduma ya upandikizaji Uloto. Huduma hii itaanza kutolewa Februari mwaka huu na hii itakuwa ya kwanza hapa nchini kwani haikuwepo hapa nchini”. Alisema Dkt. Magandi.
Hata hivyo katika kuboresha huduma za Wagonjwa mahututi (ICU), wapo mbioni kupokea wataalam Sita kutoka Nchi ya Cuba ambao wamebobea kwenye huduma hizo huku pia wakitarajia kuwa msaada mkubwa kwa wataalam wazawa wa ndani ambao watapata ujuzi kutoka kwao.
Hadi sasa Hospitali hiyo imekuwa ikipokea wagonjwa mbalimbali wanaohudumiwa kwenye kitengo hicho.
Hospitali hiyo ya Muhimbili-Mloganzila ilifunguliwa rasmi Novemba 2017 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ikiwa chini ya uendeshaji wa Chuo kikuu cha Afya na tiba shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) iliyo chini ya wizara ya Elimu, sayansi na teknolojia na baadae Oktoba 3,2018 ilikuja kubadilishwa usimamizi na uendeshaji na kuhamishiwa wizara ya Afya na kuwa chini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili hivyo kuitwa ‘Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila.
DKT.ZAINAB CHAULA AMEWATAKA VIONGOZI WA VIKUNDI KAZI VYA KITAALUMA KUTEKELEZA MALENGO KATIKA SEKTA YA AFYA
Jumamosi, Januari 18, 2020
-
Hakuna maoni
Na.Catherine Sungura,Dodoma
Viongozi wa vikundi kazi vya kitaaluma nchini wametakiwa,kuhakikisha malengo ya mipango mkakati wa sekta ya afya yanatekelezwa ipasavyo.
Rai hiyo imetolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula wakati wa kikao cha mashirikiano baina ya serikali na wadau wa sekta ya afya nchini Tanzania (Health SWAP in Tanzania) kilichofanyika jijini hapa.
Dkt. Chaula amesema kuwa viongozi wote wanatakiwa kutekeleza wajibu wao kulingana na taratibu ambazo wamejiwekea kwa kuhakikisha wao kama viongozi wa vikundi kazi toka serikalini wanakuwa mstari wa mbele katika kutoa dira na mwelekeo wa utekelezaji wa malengo yote ya kimkakati katika sekta ya afya.
“Nina imani mtaendelea kuboresha utendaji kazi wa vikundi kazi hivi kwa kushirikiana na wadau wengine pamoja na kutoa ushauri wa kitaalam katika maeneo ya kimkakati ya uboreshaji wa huduma”.Alisisitiza Dkt. Chaula
Aidha, Katibu mkuu huyo aliwataka viongozi hao kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kuandaa mpango mkakati wa sekta ya afya wa awamu ya tano(2020-2025) na kutoa maoni na mapendekezo ya idadi ya vikundi kazi zilizowasilishwa na.idara ya sera na mipango wizarani hapo.
Serikali ya Tanzania ilianza utekekezaji wa mashirikiano katika sekta ya afya na wadau mbalimbali wakiwemo wadau wa maendeleo,mashirika yasiyo ya kiserikali,asasi za kiraia na wizara mbazo zinatekeleza shughuli za sekta ya afya mwaka 1999
TIBA YA SARATANI YA DAMU YAANZA KUTOLEWA MUHIMBILI
Jumamosi, Januari 18, 2020
-
Hakuna maoni
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),
Dkt. Hedwiga Swai (wa kati kati) akizungumza na maafisa mawasiliano kutoka Wizara ya
afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na taasisi
zilizo chini ya wizara hiyo kuhusu maboresho yaliofanywa na MNH. Kushoto
ni Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa MNH, Dkt.Sufiani Baruani na uapnde wa kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi, Dkt. Praxeda Ogweyo.
Na Mwandishi Wetu - Dar Es Salaam
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeanza kutoa tiba ya awali ya saratani ya damu kwa wagonjwa wenye tatizo hilo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Muhimbili, Dkt.
Hedwiga Swai wakati akizungumza na maafisa mawasiliano kutoka Wizara ya
afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na taasisi
zilizo chini ya wizara hiyo wakati walipoitembelea hospitali kwa lengo
la kujionea maboresho mbalimbali yaliofanywa kwenye kampeni ijulikano kwa jina la Tumeboresha Sekta ya afya.
Katika kuhakikisha huduma hiyo inatekelezwa kwa ufanisi, Serikali
imetoa shilingi bilioni 6.2 kwa ajili ya kuanzisha huduma ya kupandikiza
uloto (Bone Marrow Transplant).
“Ukarabati wa miundombinu tayari umekamilika huko Hospitali ya Taifa
Muhimbili-Mloganzila, ununuzi wa vifaa tiba umekamilika kwa asilimia 90,
huku wataalamu mbalimbali wakiwa wameshasomeshwa nje ya nchi na wako
tayari kuanza kutoa tiba hii,” amesema Dkt. Swai
Dkt. Swai amesema gharama ya mtu mmoja kupandikizwa uloto nje ya nchi
ni kati ya shilingi milioni 150 hadi 200 wakati hapa nchini gharama
itakuwa shilingi milioni 50 tu.
Kuhusu huduma bobezi zinazotolewa MNH, ikiwamo upandikizaji figo,
Dkt. Swai amesema wataalamu wa usingizi, wauguzi, wataalamu wa radioloji
hivi sasa wanaweza kutoa huduma wenyewe kwa asilimia 100 wakati
wataalamu wa upasuaji wanatoa huduma ya upasuaji kwa asilimia 100 kwa
mgonjwa anayechangia figo na kwa anayepandikizwa kwa asilimia 95.
Naye, Mkurugenzi wa huduma za upasuaji MNH, Dkt. Sufiani Baruani
amesema MNH imenunua vifaa mbalimbali vya kisasa kwa ajili ya
kufanikisha upasuaji kwa njia ya tundu dogo yenye dhamani ya shilingi
milioni 800 pamoja na mashine ya kisasa ya ultrasound kwa ajili ya
upimaji wa tezi dume.
Akizungumzia mafanikio ya Idara ya Maabara, Mkurugenzi wa Tiba
Shirikishi Dkt. Praxeda Ogweyo amesema maabara ya Muhimbili imekidhi
viwango vya kimataifa na kupata ithibati ya ISO:15189:2012.
Amesema Huduma zinazotolewa katika maabara hii ni ufanyikaji wa
sampuli zote za magonjwa yanayohusiana himatolojia, kemia uhai,
parasaitolojia, mikrobiolojia, huduma za uchagishaji na upatikanaji wa
damu salama pamoja na histopatholojia.
UKUSANYAJI WA DAMU NCHINI WAONGEZEKA, JAMII YAHAMASIKA KUCHANGIA
Jumamosi, Januari 18, 2020
-
Hakuna maoni
Meneja wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Dkt. Magdalena Lyimo akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) juu ya mafanikio waliyoyapata katika kipindi ch amiaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano katika Kampeni ya Tunaboresha Sekta ya Afya inayoratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Meneja wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Dkt. Magdalena Lyimo akionyesha Cheti cha ithibati ya kimataifa ya ubora wa ukusanyaji damu kwa wanahabari (hawapo pichani) katika Kampeni ya kuangalia mafanikio ya Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya ijulikanayo kwa jina la Tumeboresha Sekta ya Afya.
Na Mwandishi Wetu - Dar Es Salaam
Imeelezwa kuwa, Chupa za damu 39379 zimekusanywa kwa mwaka 2018/2019
ukilinganisha na chupa 257557 mwaka 2017/2018 ambapo kwa ukusanyaji
huo umefanya ukusanyaji kuongezeka kutoka asilimia 40 hadi 60 asilimia.
Hayo yameelezwa jana Jijini Dar es Salaam na Meneja Mpango wa Taifa
wa Damu Salama, Dkt. Magdelena Lyimo wakati wa kusoma taarifa yake kwa
Maafisa Mawasiliano kutoka Wizara ya Afya pamoja na taasisi zake kwa
ajili ya kutangaza maboresho ya Sekta hiyo hapa Nchini katika kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya.
Aidha, amebainisha kuwa licha ya kuongezeka kwa kiwango hicho, katika
kuhakikisha wanaongeza huduma, wako katika mpango wa kujenga kituo
kikubwa cha damu Kanda ya Dodoma na tayari TSh. Bilioni 1.3
zimeshatengwa ili kufikia malengo makubwa zaidi ya ukusanyaji damu.
Akielezea namna wananchi wanavyohamasika, Dkt. Lymo alisema jamii
imekuwa na hamasa kubwa ya kuchangia damu na mapokea yamekuwa makubwa
karibu maeneo yote ya Nchi.
“Kazi zetu ni kuhakikisha uwepo wa damu salama na ya kutosha na
yenye ubora wa juu na ipatikane kwa wakati unaohitajika, tunahamasisha
uchangiaji damu, tunatoa elimu, tunakusanya, tunapima, tunahifadhi na
pia tunasambaza, pia tuna mwongozo wa uhamasishaji, ukusanyaji,
usambazaji matumizi sahihi ya damu" amesema Dkt. Lyimo
Amesema kuwa Mpango wa Taifa wa Damu Salama una vituo vya kanda saba, kuna Kanda ya Mashariki iko Mkoa Dar es
Salaam, Kaskazini iko Kilimanjaro, Kanda ya Ziwa iko Mwanza, Kanda ya
Magharibi iko Tabora, Kusini iko Mtwara na Kanda za Nyanda za Juu Kusini
iko Mbeya.
“Kila kanda ina mikoa yake ambayo inahudumia. Pia kuna kanda za jeshi, hizi hazina mpaka wa kuhudumia,” alisema Dk. Lyimo.
Ambapo alibainisha kuwa, mpango huo wa damu salama unafanya kazi na
hospitali za kibingwa ili kuweza kurahisisha upatikanaji wa damu kwa
wagonjwa.
Aidha, Dkt. Lymo amesema Mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha
miaka mine wameweza kufanya ununuzi wa mashine 24 za maabara ambazo
zimerahisisha shughuli za upimaji wa maambukizi katika damu na makundi
ya damu kwa muda mfupi.
Aliendela kwa kusema kuwa wamepata mashine mpya 24 ambapo kila kituo cha kanda kimepata mashine na
gharama za mashine hizi ni Sh bilioni 13.2, kila kanda ina mashine nne
ambapo mashine mbili ni za kupima maambukizi ya damu na mashine mbili za
kupima makundi ya damu.
“Hizi za damu zina uwezo wa kupima sampuli 156 ndani ya saa mbili na
ile ya kupima maambukizi inapima aina nne kama Ukimwi, homa ya ini B na C
na kaswende. Hii ina uwezo wa kupima sampuli 100 ndani ya saa mbili,
kwa sampuli 100 tunapata majibu 400 kutokana na kupima ugonjwa zaidi ya
mmoja,” alisema Dk. Lyimo.
Hata hivyo alisema kuna mashine ya kisasa zaidi ambayo inapokea sampuli 600 na inatoa majibu ndani ya saa moja.
“Kwa mfumo wa nyuma, sampuli zilikuwa zinapimwa 88 ndani ya saa tatu
au nne na unapata jibu moja, kwahiyo ililazimu wawepo watumishi wanne
tofauti na sasa hata uwezekano wa kufanya makosa umepungua" alifafanua Dkt. Lyimo
“Mpango wetu ni kuhakikisha tumeimarisha huduma na kanda zote saba
zitafikia vigezo vya kitaifa na kimataifa,” alieleza Dkt. Lyimo.
Kutokana na uhitaji wa mazao yatokanayo na damu, alisema uhitaji wake
utakuwa mkubwa hivyo uimarishwaji unaendelea wa upatikanaji wake.
“Tutaongeza matumizi ya mazao ya damu kama plate late, plasma na hizi
zinahitajika kwa wagonjwa mfano kama saratani, figo na hata moyo, hivyo
tunataka mgonjwa apate kitu anachokihitaji kwa wakati,” alisema Dkt. Lyimo
HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI YAJIVUNIA UBORA TIBA YA UPASUAJI NCHINI
Jumamosi, Januari 18, 2020
-
Hakuna maoni
Mkurugenzi
wa Huduma za Upasuaji Hospitali ya Taifa Muhimbili-Upanga, Dkt. Sufian
Baruani akizungumza na Maafisa Habari na Mahusiano wa Wizara ya Afya na
taasisi zake na wanahabari (hawpao pichani) wakati wa mkutano huo.
Na Mwandishi Wetu - Dar Es Salaam.
HOSPITALI
ya Taifa Muhimbili imejivunia ubora unaotolewa katika Kurugenzi ya
Upasuaji kwa kuongeza huduma nyingi pamoja na ubora wa mashine za kisasa
ambapo wameokoa fedha nyingi kama Watanzania wangefuata huduma hiyo nje
ya Nchi.
Akizungumza katika ziara ya Maafisa Mawasiliano kutoka Wizara ya Afya na Taasisi ya 'Tumeboresha Sekta ya Afya', Mkurugenzi wa huduma za upasuaji Dkt. Sufian Baruani alisema kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya tano
Wameweza kufanya mambo mbalimbali ikiwemo upanuzi wa vyumba, ununuzi wa vifaa vipya zikiwemo mashine za kisasa sambamba na kuongeza wataalam wa kibingwa.
"Hospitali ya Taifa Muhimbili-Upanga tumefanya upanuzi wa vyumba vya upasuaji kutoka 11 hadi 20 na umepunguza wagonjwa kukaa muda mrefu kusubiria huduma hii.
Awali muda ulikuwa hadi wiki 6-8, kwa mfano idara ya watoto hivi sasa muda umepunhua hadi wiki 2" alisema Dkt. Baruani.
Katika kuongeza huduma, 2017 waliweza kuanzisha huduma ya kupandikiza vifaa vya usikivu na kuweza kuwafanyia Wagonjwa 34 na kugharimu shilingi Bilioni 1.2.
"Katika maboresho ya Sekta ya Afya. Muhimbili tulikuja na huduma hii ya kupandikiza vifaa vya Usikivu ambayo ni gharama sana kwa mgonjwa mmoja.
Kabla ya hapo tulikuwa tunapeleka wagonjwa nje ya nchi kwa gharama ya shilingi Milioni 100 kwa Mgonjwa mmoja ambapo kwa hapa Muhimbili sisi Mgo jwa mmoja anagharimu shilingi milioni.35." Alisema Dkt. Buriani.
Na kuongeza kuwa, toka mwaka 2003 hadi 2016 Serikali iliweza kupeleka wagonjwa 50 nchini India.
"Tumeweza kuokoa fedha nyingi sana. Wagonjwa 34 tuliowapa huduma hapa kwetu kama wangeenda nje gharama ingekuwa Bilioni 3.4, hivyo Hospitali imeokoa bilioni 2.2.
Lakini pia awamu hii ya tano, Hospitali imenunua mashine ya kupima Usikivu (ABR) na kukarabato chumna cha usikivu" alisema Dkt. Buriani.
Katika kuhakikisha huduma zinakuwa bora zaidi kama hapa nchini, vifaa mbalimbali wameweza kuagiza ambapo vitakuwa msaada kwa Taifa katika uboreshaji wa huduma.
"Tumeagiza vifaa vyenye thamani ya milioni 800 kwa ajili ya upasuaji wa matundu madogo.
Pia tumeagiza vifaa vya shilingi milioni 700 ili kuboresha huduma za macho. Vifaa hivi ni kwa ajili ya kupima matatizo mbalimbali ya macho pamoja na vifaa vya kutengeneza miwani." Alisema Dkt. Baruani.
Dkt. Baruani ameongeza kuwa, katika huduma ya tezi dume, wameshanunua mashine ya kisasa yenye thamani ya milioni 70 , ambapo itasaidia kuchukulia vipimo vya tatizo hilo.
Kurugenzi hiyo ya upasuaji pia imeongeza viti viwili toka 7 hadi 9 pamoja na kununua vifaa vya maabara vya kutengenez meno ya bandia.
"Awali wagonjwa walikuwa wanaipata huduma hii ya meno bandia hospitali binafsi kwa sasa tumeimarisha.
Lakini pia kuna huduma hazikuwepo awali. Hizi ni huduma za matibabu za uvimbe wa taya (Haemangioma) kwa kutumia mionzi yaani interventional radiology ambapo toka mwaka 2017 hadi sasa wagonjwa 302 wamehudumiwa kwa gharama nafuu ya milioni 8 kwa kila Mgonjwa na endapo wangeenda nje ya nchi wangegharimu milioni 100 kwa mgonjwa mmoja.
"Huduma ya pili ni ya urekebishaji wa mifupa ya uso na taya ambapo hadi sasa wagonjwa 120 wamenufaika kwa grama ya shilingi milioni 3.5 kwa mgonjwa mmoja na endepo wangeenda nje ya nchi kwa kila mgonjwa mmoja angegharimu milioni 70." Alisema Dkt. Buriani.
Hata hivyo alieleza kuwa, Serikali ya awamu ya tano imeweza kusikia vilio vya wanyonge ambapo huduma zote zinazotolewa ni za kibingwa hivyo Watanzania waendelee kuwa na imani na Serikali yao.

Jumatatu, 13 Januari 2020
MAMLAKA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI KUANZISHA KANZI-DATA YA VINA SABA VYA BINADAMU YA TAIFA
Jumatatu, Januari 13, 2020
-
Hakuna maoni
Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko akizungumza na wanahanari (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kampeni ya kutangaza mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano inayojulikana kama 'Tunaboresha Sekta ya Afya' mapema leo Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi anayesimamia Idara ya Huduma ya usimamizi wa vinasaba, David Eliasi akizungumza katika tukio hilo.
Viongozi mbalimbali wa Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Maabara ya Serikali wakiwa katika mkutano
Na Mwandishi Wetu - Dar Es Salaam
Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali [GCLA] ipo katika mkakati wa kuanzisha Kanzi Data ya taifa ya Vinasaba vya Binadamu [DNA] ambayo itakuwa ikitambua asili ya kila Mtanzania na kuweza kusaidia chunguzi mbalimbali ikiwemo majanga na kupata majibu kwa kina.
Hayo yameelezwa na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko wakati wa ziara ya kampeni ya kutangaza mafanikio ya serikali ya awamu ya tano inayojulikana kama ‘Tunaboresha Sekta ya Afya’ ambapo amesema kuwa; Serikali ya awamu ya tano imejipanga kuhakikisha wanafikia malengo ya kusaidia jamii katika upande huo wa vinasaba.
‘Kwa sasa tupo katika mpango wa kuanzisha Kanzi Data ya Taifa ya Vinasaba ambapo eneo hilo kwa sasa tutaliwekea kipaumbele katika bajeti ya fedha ya mwaka huu na tayari tumeshaanza kutengeneza mpango kazi wazo dhana ya utengenezaji wake na itajumlisha wadau mbalimbali na Serikali kupitia Wizara ya Afya na wadau wengine.’ Alisema Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Mafumiko.
Dkt. Mafumiko amebainisha kuwa, kutokana na mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano kwa kuboresha rasilimali watu, miundombinu ya utendeajji kazi na vifaa vya kisasa ndio maana wamepewa jukumu hilo la kuanzishwa kwa Kanzi data hiyo sambamba na kujumuisha wadau mbalimbali.
Nae Mkurugenzi anayesimamia Idara ya Huduma ya usimamizi wa vinasaba, David Eliasi akizungumzia suala hilo la Kanzi data, amesema kuwa, Mkemia wa Serikali ndio atakuwa msimamizi na inajengwa na watanznia wenyewe huku akiwataka watanzania wajivunie juu ya hilo.
‘Serikali ya awamu ya Tano imeweza kuongeza chachu na sasa tunajenga kanzi data ya Kitaifa ya Vinasaba na inajengwa na Watanzania wenyewe. Ni ki tu cha kujivunia na timu ya Kitaifa inasimamia hii ujenzi wake wakiwemo Wizara ya Afya ambayo ni mlezi wetu, pia wapo EGav- Serikali mtandao, NIDA,RITA, NEC na taasisi nyingi tu na wote hao wamekaa pamoja na wamekuja na dhana wa uanzishwaji wa Kanzi data hii ya Kitaifa ‘ alisema David Eliasi.
Ameongeza kuwa kuanzishwa kwa kanzi data hiyo, itarahisisha upatikanaji wa haraka wa majibu ya vinasava kwani tayari sampuli zitakuwa zinapatikana kwa haraka zaidi ikiwemo kwenye majanga haswa ndugu wa marehemu kwani watafupisha matokeo ya uchunguzi na majibu kupatikana kwa muda mfupi na upatikanaji wake wa matokeo utakuwa wa haraka zaidi.
‘tutachukua muda mfupi na wa haraka zaidi. Mfano lile janga la Morogoro la moto, ndugu wa marehemu wangepatikana haraka za idi na kutpoa majibu kwa haraka na kwa kina’ alisema Davidi Eliasi.
Mamlaka ya Mkemia mkuu imeeleza kuwa, wametoa vibali vya kemikali 9994 kwa mwaka elfu kumi na mbili na tisa kutoka elfu ishirini na moja mia tatu thelasini na tisa

Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)