Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 20 Januari 2020

SERIKALI YAENDELEA KUIMARISHA MIKAKATI YA KUDHIBITI MAGONJWA YA MLIPUKO.

Baadhi ya miundombinu ya ndani, katika kituo cha tiba ya magonjwa ya mlipuko Buswelu Mwanza.

Moja kati  ya kituo cha tiba ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola na Kipindupindu chenye thamani ya shilingi  Bilion 1.1 kilichomalizika na kukabidhiwa kwa Serikali,  kilichopo  Mawenzi Kilimanjaro.

Nyumba ya Mtumishi katika Kituo cha tiba ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola na Kipindupindu.

Kituo cha tiba ya Magonjwa ya mlipuko kilichokabidhiwa kwa Serikali baada ya kumalizika, kilichopo Buswelu, Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza chenye thamani ya shilingi Bilion 1.1.

Na Rayson Mwaisemba, WAMJW- KILIMANJARO, MWANZA

Wananchi wametakiwa kuondoa  hofu, pindi wakikutana na magonjwa ya mlipuko au mhisiwa  mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola.

Wito huo umetolewa na Mhandisi Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Francis Mbuya wakati wa kukabidhi majengo ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Ebola Mkoani Mwanza na Kilimanjaro.

"Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea na jitihada za kuimarisha mikakati ya kudhibiti magonjwa ya milipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola na Kipindupindu,hivyo mnapo muhisi mtu ana dalili,toeni taarifa" Amesema Mhandisi Mbuya

Aidha, Amesema kuwa Wizara ya Afya, imekuwa ikitekeleza ujenzi wa miradi mbali mbali nchini ya ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za Afya katika Hospitali mbali mbali za Rufaa nchini pamoja na za kanda lengo ni kupambana na magonjwa aina yoyote ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola na Kipindupindu.

"Miradi hii imejengwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali ya Mawenzi Mkoani Kilimanjaro na Buswelu Mkoani Mwanza inalenga kupambana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola na Kipindupindu.

Miradi yote miwili (Buswelu Mwanza na Mawenzi Kilimanjaro) imegharimu jumla ya shilingi Bilion 2.2 kutoka Milion 897 iliyotengwa kwa kila mradi, hii ni kutokana na maboresho yaliyofanyika katika miradi hiyo ili kuweza kutoa huduma bora kwa Wananchi.

"Kwa Buswelu mradi umegharimu kiasi cha shilingi Billion 1.1 kutoka Milion 897 iliyotengwa, hii inatokana na sababu ya maboresho kutoka na kutembelewa na Wataalamu mbali mbali kutoka Bank ya Dunia ili kuhakikisha tunakuwa na viwango ambavyo vinakubalika kimataifa, sawa na mradi wa Mawenzi Kilimanjaro", alisema.

Mbali na hayo, Mhandisi Mbuya amewaasa Watumishi wa Hospitali kuhakikisha wanatunza miundombinu ya vituo hivi katika kipindi chote cha kutoa huduma, ambavyo umeigharimu Serikali pesa nyingi.

Mwisho.

0 on: "SERIKALI YAENDELEA KUIMARISHA MIKAKATI YA KUDHIBITI MAGONJWA YA MLIPUKO. "