Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumamosi, 18 Januari 2020

UKUSANYAJI WA DAMU NCHINI WAONGEZEKA, JAMII YAHAMASIKA KUCHANGIA

Meneja wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Dkt. Magdalena Lyimo akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) juu ya mafanikio waliyoyapata katika kipindi ch amiaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano katika Kampeni ya Tunaboresha Sekta ya Afya inayoratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.


Meneja wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Dkt. Magdalena Lyimo akionyesha Cheti cha ithibati ya kimataifa ya ubora wa ukusanyaji damu kwa wanahabari (hawapo pichani) katika Kampeni ya kuangalia mafanikio ya Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya ijulikanayo kwa jina la Tumeboresha Sekta ya Afya.


Na Mwandishi Wetu - Dar Es Salaam
Imeelezwa kuwa, Chupa za damu 39379 zimekusanywa kwa mwaka 2018/2019 ukilinganisha na chupa 257557 mwaka 2017/2018 ambapo kwa ukusanyaji huo umefanya ukusanyaji kuongezeka kutoka asilimia 40 hadi 60 asilimia.


Hayo yameelezwa jana Jijini Dar es Salaam na Meneja Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Dkt. Magdelena Lyimo wakati wa kusoma taarifa yake kwa Maafisa Mawasiliano kutoka Wizara ya Afya pamoja na taasisi zake kwa ajili ya kutangaza maboresho ya Sekta hiyo hapa Nchini katika kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya.


Aidha, amebainisha kuwa licha ya kuongezeka kwa kiwango hicho, katika kuhakikisha wanaongeza huduma, wako katika mpango wa kujenga kituo kikubwa cha damu Kanda ya Dodoma na tayari TSh. Bilioni 1.3 zimeshatengwa ili kufikia malengo makubwa zaidi ya ukusanyaji damu.


Akielezea namna wananchi wanavyohamasika, Dkt. Lymo alisema jamii imekuwa na hamasa kubwa ya kuchangia damu na mapokea yamekuwa makubwa karibu maeneo yote ya Nchi.


“Kazi zetu ni kuhakikisha uwepo wa damu salama na ya kutosha na yenye ubora wa juu na ipatikane kwa wakati unaohitajika, tunahamasisha uchangiaji damu, tunatoa elimu, tunakusanya, tunapima, tunahifadhi na pia tunasambaza, pia tuna mwongozo wa uhamasishaji, ukusanyaji, usambazaji matumizi sahihi ya damu" amesema Dkt. Lyimo


Amesema kuwa Mpango wa Taifa wa Damu Salama una vituo vya kanda saba, kuna Kanda ya Mashariki iko Mkoa Dar es Salaam, Kaskazini iko Kilimanjaro, Kanda ya Ziwa iko Mwanza, Kanda ya Magharibi iko Tabora, Kusini iko Mtwara na Kanda za Nyanda za Juu Kusini iko Mbeya.


“Kila kanda ina mikoa yake ambayo inahudumia. Pia kuna kanda za jeshi, hizi hazina mpaka wa kuhudumia,” alisema Dk. Lyimo.

Ambapo alibainisha kuwa, mpango huo wa damu salama unafanya kazi na hospitali za kibingwa ili kuweza kurahisisha upatikanaji wa damu kwa wagonjwa.


Aidha, Dkt. Lymo amesema Mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mine wameweza kufanya ununuzi wa mashine 24 za maabara ambazo zimerahisisha shughuli za upimaji wa maambukizi katika damu na makundi ya damu kwa muda mfupi.


Aliendela kwa kusema kuwa wamepata mashine mpya 24 ambapo kila kituo cha kanda kimepata mashine na gharama za mashine hizi ni Sh bilioni 13.2, kila kanda ina mashine nne ambapo mashine mbili ni za kupima maambukizi ya damu na mashine mbili za kupima makundi ya damu.


“Hizi za damu zina uwezo wa kupima sampuli 156 ndani ya saa mbili na ile ya kupima maambukizi inapima aina nne kama Ukimwi, homa ya ini B na C na kaswende. Hii ina uwezo wa kupima sampuli 100 ndani ya saa mbili, kwa sampuli 100 tunapata majibu 400 kutokana na kupima ugonjwa zaidi ya mmoja,” alisema Dk. Lyimo.


Hata hivyo alisema kuna mashine ya kisasa zaidi ambayo inapokea sampuli 600 na inatoa majibu ndani ya saa moja.


“Kwa mfumo wa nyuma, sampuli zilikuwa zinapimwa 88 ndani ya saa tatu au nne na unapata jibu moja, kwahiyo ililazimu wawepo watumishi wanne tofauti na sasa hata uwezekano wa kufanya makosa umepungua" alifafanua Dkt. Lyimo


“Mpango wetu ni kuhakikisha tumeimarisha huduma na kanda zote saba zitafikia vigezo vya kitaifa na kimataifa,” alieleza Dkt. Lyimo.

Kutokana na uhitaji wa mazao yatokanayo na damu, alisema uhitaji wake utakuwa mkubwa hivyo uimarishwaji unaendelea wa upatikanaji wake.


“Tutaongeza matumizi ya mazao ya damu kama plate late, plasma na hizi zinahitajika kwa wagonjwa mfano kama saratani, figo na hata moyo, hivyo tunataka mgonjwa apate kitu anachokihitaji kwa wakati,” alisema Dkt. Lyimo

0 on: "UKUSANYAJI WA DAMU NCHINI WAONGEZEKA, JAMII YAHAMASIKA KUCHANGIA"