Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab A.S Chaula
Na.Catherine Sungura,Dodoma
Viongozi wa vikundi kazi vya
kitaaluma nchini wametakiwa,kuhakikisha malengo ya mipango mkakati wa
sekta ya afya yanatekelezwa ipasavyo.
Rai hiyo imetolewa jana na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Zainab Chaula wakati wa kikao cha mashirikiano baina ya serikali na
wadau wa sekta ya afya nchini Tanzania (Health SWAP in Tanzania)
kilichofanyika jijini hapa.
Dkt. Chaula amesema kuwa viongozi
wote wanatakiwa kutekeleza wajibu wao kulingana na taratibu ambazo
wamejiwekea kwa kuhakikisha wao kama viongozi wa vikundi kazi toka
serikalini wanakuwa mstari wa mbele katika kutoa dira na mwelekeo wa
utekelezaji wa malengo yote ya kimkakati katika sekta ya afya.
“Nina imani mtaendelea kuboresha
utendaji kazi wa vikundi kazi hivi kwa kushirikiana na wadau wengine
pamoja na kutoa ushauri wa kitaalam katika maeneo ya kimkakati ya
uboreshaji wa huduma”.Alisisitiza Dkt. Chaula
Aidha, Katibu mkuu huyo aliwataka
viongozi hao kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kuandaa mpango
mkakati wa sekta ya afya wa awamu ya tano(2020-2025) na kutoa maoni na
mapendekezo ya idadi ya vikundi kazi zilizowasilishwa na.idara ya sera
na mipango wizarani hapo.
Serikali ya Tanzania ilianza
utekekezaji wa mashirikiano katika sekta ya afya na wadau mbalimbali
wakiwemo wadau wa maendeleo,mashirika yasiyo ya kiserikali,asasi za
kiraia na wizara mbazo zinatekeleza shughuli za sekta ya afya mwaka 1999
0 on: "DKT.ZAINAB CHAULA AMEWATAKA VIONGOZI WA VIKUNDI KAZI VYA KITAALUMA KUTEKELEZA MALENGO KATIKA SEKTA YA AFYA"