Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula akimkabidhi mmoja wa wahitimu wa kada ya Famasi cheti cha taaluma pamoja na usajili katika warsha iliyofanyika jijini Dodoma. |
Na Emmanuel Malegi- Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula amewasihi
wahitimu wa kada ya famasi kutoka vyuo mbalimbali nchini na nje ya nchi
kuheshimu na kufuata misingi na miongozo ya taaluma hiyo ili kuweza kutoa
huduma bora kwa wananchi.
Dkt. Chaula amesema hayo mapema leo wakati alipohudhuria
warsha fupi ya kuwatunuku vyeti vya kuhitimu na usajiri wahitimu zaidi ya 100
waliohitimu shahada ya Famasi katika vyuo mbalimbali nchini.
“Ninaomba mkawe wanyenyekevu mkiwa maeneo yenu ya kazi,
kuzingatia kanuni na misingi ya taaluma ni jambo muhimu la kufuata kwa kila
mmoja wetu, nidhamu mahala pa kazi huleta umakini katika kazi yako, jamii
inawategemea ili muweze kutoa huduma nzuri kwa wananchi”. Amesema Dkt. Chaula.
Dkt. Chaula ameendelea kusisitiza kuwa taaluma hiyo ni
muhimu sana nchini kwani wagonjwa wanategemea kupata dawa sahihi ambazo zitatolewa
na wafamasia hao ili ziwasaidie kupona maradhi yanayowasumbua.
Aidha, Dkt. Chaula amewataka Wahitimu hao kushirikiana kwa
karibu na madaktari pamoja na wahudumu wengine wa afya wakiwemo manesi ili
waweze kusaidia katika kutoa huduma bora za afya na kusaidia wananchi kupata
nafuu na kupona kabisa maradhi yanayowasumbua.
Kwa upande wake Msajili wa Baraza la Famasi nchini Bi.
Elizabeth Shekalaghe amewataka wahitimu hao kwenda kuisaidia jamii na kuziba
baadhi ya mapengo ya taaluma hiyo ambayo ina watumishi wachache na uhitaji ni
kubwa nchini ambapo hivi sasa Tanzania ina wafamasia takribani 1200
waliosajiliwa na Baraza hilo nchi nzima.
Homework writing service is a common thing among students. Some students do not have time to do their homework, while others are just lazy. Some may have an issue with their homework writing skills. In all these cases, a homework writing service can be of great help.
JibuFuta