Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Ijumaa, 31 Januari 2020

WAFAMASIA WATAKIWA KUFUATA MISINGI YA KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI

Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula akizungumza na Wahitimu wa kada ya Famasi (Hawapo pichani) wakati wa warsha fupi ya kutoa vyeti vya kuhitimu na usajili iliyofanyika katika ukumbi wa Takwimu jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Huduma za Afya kutoka TAMISEMI Dkt. Ntuli Kapologwe akiongea neno kwa wahitimu wa kada ya Famasi (Hawapo pichani) wakati wa warsha fupi ya kutoa vyeti vya kuhitimu na usajili iliyofanyika katika ukumbi wa Takwimu jijini Dodoma.

Mfamasia Mkuu Bw. Daud Mmasi  akizungumza na wahitimu wa kada ya Famasi (Hawapo pichani) wakati wa warsha fupi ya kutoa vyeti vya kuhitimu na usajili iliyofanyika katika ukumbi wa Takwimu jijini Dodoma.

Msajili wa Baraza la Famasi nchini Bi. Elizabeth Shekalaghe akiongoza kiapo cha Wafamasia waliohitimu kutoka vyuo mbalimbali nchini walipokutana katika warsha fupi ya kukabidhi vyeti vya taaluma na usajili iliyofanyika katika ukumbi wa Takwimu Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula akimkabidhi mmoja wa wahitimu wa kada ya Famasi cheti cha taaluma pamoja na usajili katika warsha iliyofanyika jijini Dodoma.


Picha mbalimbali zikionesha Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula (aliyekaa katikati) na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu na Sekretarieti ya Baraza la famasi katika warsha fupi ya kutoa vyeti vya taaluma na usajili kwa wahitimu hao. 


Na Emmanuel Malegi- Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula amewasihi wahitimu wa kada ya famasi kutoka vyuo mbalimbali nchini na nje ya nchi kuheshimu na kufuata misingi na miongozo ya taaluma hiyo ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi.

Dkt. Chaula amesema hayo mapema leo wakati alipohudhuria warsha fupi ya kuwatunuku vyeti vya kuhitimu na usajiri wahitimu zaidi ya 100 waliohitimu shahada ya Famasi katika vyuo mbalimbali nchini.

“Ninaomba mkawe wanyenyekevu mkiwa maeneo yenu ya kazi, kuzingatia kanuni na misingi ya taaluma ni jambo muhimu la kufuata kwa kila mmoja wetu, nidhamu mahala pa kazi huleta umakini katika kazi yako, jamii inawategemea ili muweze kutoa huduma nzuri kwa wananchi”. Amesema Dkt. Chaula.

Dkt. Chaula ameendelea kusisitiza kuwa taaluma hiyo ni muhimu sana nchini kwani wagonjwa wanategemea kupata dawa sahihi ambazo zitatolewa na wafamasia hao ili ziwasaidie kupona maradhi yanayowasumbua.

Aidha, Dkt. Chaula amewataka Wahitimu hao kushirikiana kwa karibu na madaktari pamoja na wahudumu wengine wa afya wakiwemo manesi ili waweze kusaidia katika kutoa huduma bora za afya na kusaidia wananchi kupata nafuu na kupona kabisa maradhi yanayowasumbua.

Kwa upande wake Msajili wa Baraza la Famasi nchini Bi. Elizabeth Shekalaghe amewataka wahitimu hao kwenda kuisaidia jamii na kuziba baadhi ya mapengo ya taaluma hiyo ambayo ina watumishi wachache na uhitaji ni kubwa nchini ambapo hivi sasa Tanzania ina wafamasia takribani 1200 waliosajiliwa na Baraza hilo nchi nzima.

 -MWISHO-


1 on: "WAFAMASIA WATAKIWA KUFUATA MISINGI YA KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI"
  1. Homework writing service is a common thing among students. Some students do not have time to do their homework, while others are just lazy. Some may have an issue with their homework writing skills. In all these cases, a homework writing service can be of great help.

    JibuFuta