Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 13 Januari 2020

MAMLAKA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI KUANZISHA KANZI-DATA YA VINA SABA VYA BINADAMU YA TAIFA


Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko akizungumza na wanahanari (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kampeni ya kutangaza mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano inayojulikana kama 'Tunaboresha Sekta ya Afya' mapema leo Jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi anayesimamia Idara ya Huduma ya usimamizi wa vinasaba, David Eliasi akizungumza katika tukio hilo. 

 Viongozi mbalimbali wa Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Maabara ya Serikali wakiwa katika mkutano


Na Mwandishi Wetu - Dar Es Salaam
Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali [GCLA]  ipo katika mkakati wa kuanzisha  Kanzi Data ya taifa ya  Vinasaba vya Binadamu  [DNA]  ambayo itakuwa ikitambua asili ya kila Mtanzania  na kuweza kusaidia chunguzi mbalimbali ikiwemo majanga na kupata majibu kwa kina.
Hayo yameelezwa na Mkemia Mkuu wa Serikali,  Dkt. Fidelice Mafumiko wakati wa ziara ya kampeni ya kutangaza mafanikio ya serikali ya awamu ya tano inayojulikana kama ‘Tunaboresha  Sekta ya Afya’  ambapo amesema kuwa;  Serikali ya awamu ya tano imejipanga kuhakikisha wanafikia malengo  ya kusaidia jamii katika upande huo wa vinasaba.

‘Kwa sasa tupo katika mpango wa kuanzisha Kanzi Data ya Taifa ya  Vinasaba  ambapo eneo hilo kwa sasa tutaliwekea kipaumbele katika bajeti ya fedha ya mwaka huu na tayari tumeshaanza kutengeneza  mpango kazi wazo dhana ya utengenezaji wake na  itajumlisha wadau mbalimbali na Serikali kupitia Wizara ya Afya  na wadau wengine.’ Alisema Mkemia Mkuu wa Serikali  Dkt. Mafumiko.
Dkt. Mafumiko amebainisha kuwa, kutokana na mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano kwa kuboresha rasilimali watu, miundombinu ya utendeajji kazi na vifaa vya kisasa ndio maana wamepewa jukumu hilo la kuanzishwa  kwa Kanzi data hiyo sambamba na kujumuisha wadau mbalimbali.
Nae Mkurugenzi anayesimamia Idara ya Huduma  ya usimamizi wa vinasaba, David Eliasi akizungumzia suala hilo la Kanzi data, amesema kuwa, Mkemia wa Serikali ndio atakuwa msimamizi na inajengwa na watanznia wenyewe  huku akiwataka watanzania  wajivunie juu ya hilo.
‘Serikali ya awamu ya Tano imeweza kuongeza chachu na sasa tunajenga kanzi data ya Kitaifa ya Vinasaba na inajengwa na Watanzania wenyewe. Ni ki tu cha kujivunia na timu ya Kitaifa inasimamia hii ujenzi wake wakiwemo Wizara ya Afya ambayo ni mlezi wetu, pia wapo  EGav- Serikali mtandao, NIDA,RITA,  NEC  na taasisi nyingi tu na wote hao wamekaa pamoja na wamekuja na dhana wa uanzishwaji wa Kanzi data hii ya Kitaifa ‘ alisema David Eliasi.
Ameongeza kuwa kuanzishwa kwa kanzi data hiyo,  itarahisisha upatikanaji wa haraka wa majibu ya vinasava kwani   tayari sampuli zitakuwa zinapatikana kwa haraka zaidi ikiwemo kwenye majanga haswa  ndugu wa marehemu kwani watafupisha matokeo ya uchunguzi na majibu kupatikana kwa muda mfupi na upatikanaji wake wa matokeo utakuwa wa haraka zaidi.
‘tutachukua muda mfupi na wa haraka zaidi. Mfano lile janga la Morogoro la moto, ndugu wa marehemu wangepatikana haraka za idi na kutpoa majibu kwa haraka na kwa kina’ alisema Davidi Eliasi.
Mamlaka ya Mkemia mkuu imeeleza kuwa, wametoa vibali  vya kemikali 9994 kwa mwaka  elfu kumi na mbili na tisa kutoka elfu  ishirini na moja mia tatu  thelasini na tisa  
Mwisho

0 on: "MAMLAKA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI KUANZISHA KANZI-DATA YA VINA SABA VYA BINADAMU YA TAIFA"