Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumanne, 7 Januari 2020

DKT. NDUGULILE AHOJI UPATIKANAJI WA TAARIFA ZA DAWA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA IRINGA.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akikagua nyaraka mbalilmbali wakati alipotembelea kukagua stoo ya dawa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii.




Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akikagua nyaraka mbalilmbali wakati alipotembelea kukagua stoo ya dawa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii.


Na Mwandishi Wetu - Iringa.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile ameutaka uongozi wa Mkoa wa Iringa unatoa taarifa zaya upatikanaji wa dawa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.

Agizo hilo limekuja mara baada ya ziara ya yake mkoani humo alipotembelea hospitali hiyo kujionea utoaji wa huduma za afya kwa wananchi katika Hospitlai hiyo.

Akiwa hospitalini hapo Dkt. Ndugulile ameonyesha kutoridhishwa na utendaji kazi wa baadhi ya wauguzi katika wodi ya Mama na Mtoto kwa kutozingatia utoaji huduma hasa kuhakikisha wazazi na watoto wanapewa dawa kwa wakati zinazotakiwa na kwa idadi sahihi.

Ameongeza kuwa lengo la mgonjwa kupewa huduma ni kuhakikisha anapona na sio kufanya aendelee kupata tabu na shida hivyo Serikali ya Awamu ya Tano imewekeza fedha nyingi katika kuhakikisha Sekta ya Afya inaboreshwa nchini.
"Haiwezekani mgonjwa kanunua dawa zake kwa fedha zake lakini bado hata hamzingatii kumpatia dawa mnategemea ataponaje” alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha Dkt. Ndugulile ameutaka uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa kuhakikisha wanaratibu utoaji wa huduma hospitalini hapo ili kuepukana na malalamiko ya wagonjwa na kupoteza imani ya wananchi kwa Hospitali hiyo.

"Tukiendelea hivi tutaondoa imani kwa wananchi wetu katika utoaji wa huduma za afya sisi tunatakiwa kutoa huduma kwa wananchi na sio kuwapa kero wananchi" alisema Dkt. Ndugulile.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Atupele Mwandiga amemuahikikishia Naibu Waziri Dkt. Ndugulile kusimamia utoaji huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa na kusimamia vilivyo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma inayostahili.

Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya tano imetoa kiasi cha Billioni 7 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Wilaya na maboresho katika Zahanati na vituo vya Afya mkoani humo katika kuhakikisha inaboresha Sekta ya Afya hivyo watasimamia Sekta hiyo kikamilifu.

"Mhe. Naibu Waziri tutahakikisha hatutopoteza imani ya wananchi katika utoaji huduma za afya na tutatendea haki rasimali fedha tulizopewa na Serikali katika kuboresha Sekta ya Afya Mkoani kwetu" alisema Dkt. Atupele

Wakati huo huo Dkt. Ndugulile ametembelea na kujionea utendaji kazi utoaji wa huduma kwa wananchi katika Ofisi ya Bima ya Afya (NHIF), Kampeni ya masuala ya Lishe, Kiwanda cha Ruaha Milling na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilolo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile yuko katika ziara ya siku mbili mkoani Iringa kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii mkoani humo.

MWISHO.
 

0 on: "DKT. NDUGULILE AHOJI UPATIKANAJI WA TAARIFA ZA DAWA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA IRINGA."