Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumanne, 21 Januari 2020

"HUDUMA ZA AFYA KWENYE HOSPITALI ZA RUFAA ZA MIKOA ZIMEIMARIKA" - DKT.CHAULA

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula akifafanua jambo wakati wa kakao cha Kamati ya Bunge Huduma na Maendeleo ya Jamii

Na. WAMJW-Dodoma

Wizara ya afya,Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto –Idara kuu Afya  imeendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za kibingwa kwenye mazingira  karibu na wananchi kwenye hospitali zake za rufaa za mikoa hapa nchini

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Zainabu Chaula wakati akijibu maswali kutoka kwa wajumbe wa kamati ya  ya kudumu ya Bunge na huduma  na maendeleo ya jamii jijini hapa.

“Katika kipindi cha Julai hadi Novemba 2019 hospitali za rufaa za mikoa 18 zilitoa huduma za mkoba katika fani za kibingwa  na hii ni katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya karibu na wananchi”.Alisema Dkt. Chaula

Alizitaja huduma za mkoba za kibingwa zilizotolewa ni pamoja na magonjwa ya macho,watoto ,dawa za usingizi,upasuaji wa kawaida,afya ya uzazi na magonjwa ya wanawake.

“Zipo huduma zingine ambazo wananchi walinufaika nazo ikiwemo ya upasuaji wa mishipa ya fahamu na ubongo,sikio,pua na koo,radiologia,afya ya akili,afya ya kinywa na meno pamoja na tiba ya ngozi na huduma za tiba  kwa mazoezi”.

Hata hivyo alisema  katika kliniki hizo  jumla ya wagonjwa 13,107 walihudumiwa kati yao wagonjwa 1,762 walifanyiwa upasuaji.

Kwa upande mwingine Dkt. Chaula alisema jumla ya wagonjwa  2,194,738 walihudumiwa katika hospitali 28 za rufaa za  mikoa ambapo wagonjwa wa nje (OPD) walikuwa 1,891, 713 na wagonjwa wa kulazwa (IPD) walikuwa 303,025 katika kipindi cha julai hadi desemba 2019.
-Mwisho-

0 on: ""HUDUMA ZA AFYA KWENYE HOSPITALI ZA RUFAA ZA MIKOA ZIMEIMARIKA" - DKT.CHAULA"