Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 15 Januari 2018

SERIKALI YAANZA KUTUMIA MFUMO WA NYOTA KATIKA KUVIPIMA VITUO VYA AFYA NA HOSPITALI NCHINI

Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (mwenye tisheti ya mistari) akipokea maelekezo ya ramani ya jingo jipya la Mama na Mtoto katika kituo cha Afya Nkomolo, anaemfuatia ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Boniface Kasululu na wa mwisho ni Mhandisi Mwakyembe.

Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akikagua jokofu la Chanjo wakati alipotembelea katika Kituo cha Afya cha Nkomolo kilichopo Nkasi Mkoani Rukwa wakati wa Ziara yake ya kukagua Huduma za Afya Mkoani Rukwa.

Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akikagua Bin Kadi ambayo inaonesha idadi ya Dawa zilizoingia na zilizobaki katika stoo ya dawa ya Kituo cha Afya Nkomolo Mkoani Rukwa.

Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akikagua Idadi ya watu waliohudhuria Kituoni hapo kupitia mfumo wa Kompyuta katika stoo ya dawa ya Kituo cha Afya Nkomolo Mkoani Rukwa.

Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akipokea maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Majengo Mhandisi Mwakyembe kutoka Ofisi ya Mkoa wa Rukwa.

Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiendelea na ziara yake katika kituo cha Afya Nkomolo, anaemfuata ni Mhandisi Mwakyembe na Mbunge wa Nkasi kaskazini Mh.Kessy Ally.


Na WAMJWW. RUKWA-NKASI
Serikali yaanza kutumia mfumo wa nyota kupima huduma zitolewazo na Vituo vya Afya, Hospitali na Zahanati nchini ili kupima utendaji kazi wa watumishi wa Sekta ya Afya katika kutoa huduma kwa wananchi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea Kituo cha Afya cha Nkomolo Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa, ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya kukagua shughuli za utoaji wa huduma za Afya na kuamsha hali kwa wananchi katika kujihusisha na shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
 
“Tumeanza utaratibu wa kutoa nyota katika vituo vya Afya, imeanzia nyota sifuri mpaka nyota tano, sifuri maana yake kituo hicho hakifai kutoa huduma ya Afya na nyota tano maana yake kinafanya vizuri sana” Alisema Dkt. Ndugulile.
 
Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile aliridhishwa na hali ya upatikanaji wa Dawa katika kituo hicho, hivyo kuwatoa hofu wananchi na kusisitiza kuwa hawapaswi kuuziwa dawa zote muhimu kwani Serikali imeboresha hali ya upatikanaji wa Dawa katika vituo vyote vya Afya nchini.

“Dawa zote za msingi tunazo zakutosha, hivyo hatutarajii kuona mtu aje hapa kutibiwa kisha aambiwe akanunue katika vituo binafsi, Hali ya upatikanaji wa Dawa ni nzuri katika kituo hiki na ni asilimia 85 ” aliendelea Dkt. Ndugulile.

Aidha, Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini Mh. Ally Kessy aliupongeza uongozi wa Mkoa kwa kusimia vizuri ujenzi wa kituo hicho, uliojumuisha Thieta, Wodi ya mama na mtoto mochwari na maabara mpaka hatua ya kupaua kwa jumla ya kiasi cha shilingi Bilioni 290 kwa kutumia nguvu kubwa ya wananchi (fixed akaunti). 

Akiwasilisha taarifa ya Mkoa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt Boniface Kasululu amesema kuwa Mkoa wa Rukwa umeendelea kuboresha huduma za Afya ya mama na mtoto katika maeneo ya vijijini kama juhudi za kupunguza tatizo la vifo vya wanawake na watoto wachanga vitokanavyo na matatizo ya uzazi.

Dkt. Boniface aliendelea kusema kwamba, Zaidi ya vituo 214 kati ya 223 vilivyopo, vinatoa huduma muhimu za mzazi na mtoto jambo linalosaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto wachanga licha ya upungufu mkubwa wa vituo hivyo.

Kwa upande mwingine Dkt. Boniface Kasululu alisema kwamba Mkoa unaendelea kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwapeleka watoto katika vituo vinavyotoa huduma za chanjo, Hadi kufikia Mwezi Novembe 2017 jumla ya Watoto 48,494 wenye umri wa chini ya mwaka mmoja walipewa chanjo, kati ya watoto 50,245 waliotarajiwa ambao ni sawa na asilimia 96 jambo lililoufanya mkoa kuvuka lengo la kitaifa la asilimia 90.

DKT. FAUSTINE AWAAGIZA VIONGOZI WA MKOA WA RUKWA KUTOKOMEZA UDUMAVU UNAOSABABISHWA NA LISHE DUNI

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipitia ramani ya jengo jipya la mama na mtoto linaloendelea kujengwa katika hatua ya kuboresha huduma katika kituo cha Afya cha Mazwi.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akiteta jambo na viongozi mbali mbali katika moja ya jengo jipya linalojengwa ikiwa ni moja ya jitihada za kuboresha kituo cha Afya cha Mazwi.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akiongoza msafala wa ukaguzi wa jingo jipya katika kituo cha Mazwi Wilaya ya Sumbawanga  mkoani Rukwa.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akijiridhisha na uwepo wa Dawa katika stoo ya Dawa katika kituo cha Afya cha Mazwi.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akikagua Dawa katika stoo ya Dawa katika Kituo cha Afya Mazwi, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Mkoa wa Rukwa wilaya ya Sumbawanga, pembeni yake ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Boniface Kasululu.


Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akiwa ndani ya jingo jipya la wodi ya kina mama wajawazito, katika ziara yake ya kukagua huduma zinazotolewa katika kituo hicho.


Na WAMJWW. RUKWA-SUMBAWANGA
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Rukwa kuhakikisha wanapambana na kutokomeza udumavu kwa watoto unaosababishwa na ukosefu wa Lishe bora.
Ameyasema hayo akiwa katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua shughuli za utoaji huduma za Afya, na uhamasishaji wa vikundi vidogo vidogo vya wanaweke vya ujasiriamali  katika Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa.
”Mkoa wa Rukwa haupaswi kuwa na utapiamlo hata kidogo, asilimia 60 ya udumavu ndani ya Rukwa ni kiasi kikubwa sana, katika mkoa ambao una chakula na ardhi yenye rutuba nzuri ni jambo la kushangaza kuona tatizo hili”, Alisema Dkt. Ndugulile
Dkt. Ndugulile aliendelea kwa kusema kuwa, Siku 100 za mwanzo tangia mtoto anazaliwa ni muhimu na nyeti sana katika kuhakikisha  anapata maziwa ndani ya miezi sita, na anapoanza kula ale vyakula vyenye lishe ya kutosha ili ubongo wake ukue vizuri.
Aidha, Dkt. Ndugulile ametoa maelekezo kwa sekretarieti ya Mkoa na viongozi wa kisiasa kushirikiana kwa pamoja katika kutoa elimu ya kutosha kwenye kila mikusanyiko watakayofanya kuhusiana na masuala ya Lishe bora ili kutokomeza janga hili linalosumbua idadi kubwa ya watoto katika Mkoa huu.
Kwa upande wake Mbunge wa Sumbawanga Mh. Aishi Hilaly amemshukuru Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile  kwa kuwakumbuka katika mgao wa fedha za kuboresha Vituo vya Afya cha Mazwi, pia hakusita kupaza sauti juu ya ombi la gari la kubebea wagonjwa litakalosaidia kupunguza hadha kubwa wanayokumbana nayo inayotokana na kukosekana kwa gari hilo.
Nae Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Boniface Kasululu Mkoa unaendelea kupambana na magonjwa ya mlipuko hasa ugonjwa wa kipindupindu kwa kutoa elimu ya Afya na Usafi wa mazingira kwa wananchi, ili kuhakikisha magonjwa haya yanakuwa historia katika mkoa wa Rukwa.
Aidha, Dkt. Kasululu alimuomba Dkt. Faustine kupunguza hadha ya upungufu wa madaktari bingwa na mabingwa wa fani nyingine, Dkt. Kasululu alisema kuwa hadi kufikia Desemba 2017 Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa inajumla ya madaktari bingwa 5 ambao ni sawa na asilimia 21 kati ya madaktari 24 wanaohitajika.


BAADHI YA MADAKTARI BINGWA KUTOKA MUHIMBILI WANATAKIWA KUHAMIA HOSPITALI YA TEMEKE KUONGEZA NGUVU.


Pix 1 & 2
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwajulia hali baadhi ya wagonjwa wakati alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke ili kuona hali ya utoaji hudfuma kwa wagonjwa katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam.

Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akiongea na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke awapo pichani alipotembelea hospitali hiyo  ili kuona hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Mohammed Mohammed na wa kwanza kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Amani Malima

Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke  Dkt. Amani Malima kushoto wakati alipotembelea Hospitali hiyo ili kuona hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam.


Pix 5 & 6
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu mwenye kilemba cheupe akiongea na baadhi ya wananchi wanaosubiri kupata huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke wakati alipotembelea Hospitali hiyo ili kuona hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa hospitalini hapo leo jijini Dar es salaam.

NA WAMJW-DAR ES SALAAM

BAADHI ya Madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili wanatakiwa kuhamia Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke ili kuongeza rasilimali watu kwa ajili ya kumudu hali ya ongezeko la wanaotaka huduma bora za afya hospitalini hapo. 

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.  Ummy Mwalimu alipotembelea Hospitali hiyo ili kuangalis hali ya utoaji wa huduma za afya kwa wananchi hospitalini hapo. 

"Kubwa nliloligundua hapa ni kuna mlundikano wa idadi kubwa ya wanaohitaji huduma hivyo wale madaktari tunaowatoa Muhimbili hasa madaktari bingwa baadhi tutawahamishia hapa ili kusaidiana na madaktari wa Temeke katika kutoa huduma bora kwa watu wengi zaidi" alisema Waziri Ummy. 

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Serikali ipo mbioni kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kujenga jengo la ghorofa nne ambalo litachangia katika kuondoa tatizo la mlundikano wa wagonjwa hospitalini hapo mapema mwaka huu.

Mbali na hayo Waziri Ummy ametoa rai kwa wananchi wore kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya ili kupata huduma za matibabu kwa wakati sahihi na kwa bei nafuu hasa kwa watoto wadogo wenye kadi inayoitwa Afya toto Kadi kwa bei ya shilingi 50, 400 tu. 

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke Dkt. Amani Malima amesema kuwa wapo mbioni kuagiza vifaa na vifaa tiba pamoja na kuomba kuongezwa watumishi  kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wengi zaidi kama ilivyoelekezwa na Mhe.  Waziri Ummy. 

"Tunakabiliwa na upungufu wa watumishi na ndo mana kuna mlundikano wengi wa wanaohitaji huduma lakini tunamshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kuja na kuona changamoto zetu na kutuhaidi mazuri zaidi katika jitihada za kutoa hufuma bora za afya kwa wananchi" alisema Dkt. Malima. 


Alhamisi, 11 Januari 2018

DKT NDUGULILE AWAASA WANANCHI KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwaonesha nembo ya MSD GOT inayotambulisha kuwa Dawa hiyo inatolewa na Serikali kwa wananchi.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua moja kati ya Friji ya kuhifadhia  chanjo.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa ndani ya duka la Dawa la MSD kufanya ukaguzi juu ya upatikanaji wa Dawa zote, Kulia ni Mfamasia wa duka hilo Bahati Kazimili

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua mashine ya  Utla Sound wakati akiwa katika ziara yake Mkoani Katavi ya kukagua shughuli za utoaji wa huduma za Afya na kutathimini shughuli za maendeleo zinazofanywa na wananchi wenyewe kwa kushirikiana na Serikali.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na mgonjwa katika wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Manispaa Mpanda wakati akiwa katika ziara yake Mkoani Katavi ya kukagua shughuli za utoaji wa huduma za Afya, Kulia ni Mganga Mkuu Manispaa ya Mpanda Dkt. Mahenge

WAMJW-KATAVI

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsioa,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile amewataka wananchi kutumia nguvu  kazi yao katika ujenzi na uboreshaji wa Zahanati katika Wilaya zao kuliko kupeleka pesa nyingi kwa wakandarasi.
Dkt.Ndugulile ameyasema hao wilayani hapa wakati wa ziara ya kikazi ya  kukagua shughuli za utoaji huduma za afya na kutathimini  shughuli za maendeleo ikiwemo ya upanuzi wa miundombinu zikiwemo ya Zahanati
Alisema kutumia nguvu kazi zao itasaidia  kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama ambazo zingeweza kujitokeza kama wangetoa tenda hiyo kwa wakandarasi.”Nyinyi ndio wasimamizi wakuu wa shughuli hizi na mkiharibu tutakuja kuwalaumu nyinyi
Aidha,alisema Serikali imetoa shilingi milioni 400 kwa ajili ya kuboresha miundombinu  ya huduma za afya  nchini  kwa upande wa uzazi wa dharura ikiwemo upasuaji, wodi ya wazazi,maabara ,wodi ya watoto pamoja na nyumba ya mtumishi kwenye vituo vya afya ambapo ujenzi huo unaanza mara moja
Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile ameendele kuwatoa hofu wananchi juu ya hali ya upatikanaji wa dawa, huku akiwasisitiza wananchi wasiuziwe dawa zozote muhimu kwani hali ya upatikanaji wa Dawa ni nzuri maeneo yote na sasa ni wastani wa asilimia 80.

“Katika kituo cha Afya Kanoge, bajeti ya dawa imeongezeka kutoka Milioni 300 mpaka Bilioni 2.5, kwahiyo dawa tunazo za kutosha, hivyo hatutarajii kuona mtu aje hapa aambiwe akanunue dawa sehemu nyingine, wamenithibitishia waganga wangu asilimia 90 ya dawa muhimu zipo” aliendelea Dkt. Ndugulile

Wakati huo huo Dkt. Ndugulile amesisitiza watumishi wa afya juu ya utunzaji wa kumbukumbu za dawa katika stoo ya madawa ikiwemo kuweka za kujua idadi za dawa zilizoingia na kutoka pamoja na utunzaji wa takwimu za mahudhurio ya wagonjwa wa kila siku, jambo linalopunguza ufanisi katika kazi.

Hata hivyo Dkt. Ndugulile amemtaka Mganga Mkuu wa Manispaa ya Mpanda Dkt. Mahenge kuanzisha ofisi ya kushughulikia malalamiko ya watu pindi wanapokutana na changamoto wakati wakipata huduma katika Kituo hicho cha Afya.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Yahaya Hussein wakati akiwasilisha taarifa ya Mkoa alisema kuwa Mkoa wa Katavi unakabiriwa na uhaba mkubwa wa watumishi wa kada ya Afya hali inayopelekea changamoto kubwa katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
“Hadi kufikia Septemba 2017 Mkoa wa Katavi una jumla ya watumishi 693 sawa na asilimia 28 kati ya watumishi 2,437 wanaohitajika, kati ya hao 19 ni watumishi ngazi ya Mkoa na 674 ngazi ya Serikali za mitaa, kwa ujumla Mkoa wa Katavi una jumla ya upungufu wa watumishi 1,744” Alisema Dkt.  Hussein.
Dkt. Yahaya Hussein aliongeza kuwa Mkoa unaendelea kuzisimamia Halmashauri kuhakikisha zinatenga bajeti kwa ajili ya kuwakatia kadi za Afya ya Jamii (CHF) wazee ili kuendelea kupata Huduma za Afya kwa urahisi katika maeneo yao.
Mpaka kufikia Mwezi Septemba 2017 jumla ya wazee 19,248 wametambuliwa, na kati ya hao jumla ya wazee 1,807 sawa na asilimia 9.4 wameshapatiwa kadi za CHF katika Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi.

ALIYOYASEMA NAIBU WAZIRI DKT. NDUGULILE KATAVI

Jumatano, 10 Januari 2018

WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA HOSPITALI YA TAALUMA NA TIBA MLOGANZILA

Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akimjulia hali mgonjwa aliyelazwa kwenye hospitali ya taaluma na Tiba Mloganzila wakati alipotyembelera hospitali hiyo ili kuangalia hali ya utoaji huduma leo jijini Dar es salaam.

Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na baadhi ya wananchi waliokuwa wanasuburi huduma kwenye hospitali ya taaluma na Tiba Mloganzila wakati alipotyembelera hospitali hiyo ili kuangalia hali ya utoaji huduma leo jijini Dar es salaam.. wa kwanza kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo na Huduma za Hospitali hiyo Prof. Aboud Said.

Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiongea na waandishi wa habari alipotyembelea hospitali ya Taaluma na Tiba Mloganzila ili kuangalia hali ya utoaji huduma leo jijini Dar es salaam,wa kwanza kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo na Huduma za Hospitali hiyo prof. Aboud Said.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo na Huduma za Hospitali Mloganzila wa kwanza kulia Prof. Aboud Said. Akizungumza na waandishi wa habari wakati Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati alipotyembelea hospitali ya Taaluma na Tiba Mloganzila ili kuangalia hali ya utoaji huduma leo jijini Dar es salaam.

Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikatiakitembelea maeneo ya Hospitali ya Taaluma na Tiba Mloganzila alipotyembelera hospitali hiyo ili kuangalia hali ya utoaji huduma leo jijini Dar es salaam.. wa kwanza kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo na Huduma za Hospitali hiyo Prof. Aboud Said.

PICHA NA ALLY DAUD.




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo Januari 10 ,2018 ametembelea Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Cha Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila iliyofunguliwa rasmi  na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Novemba 25 ,2017  .
Lengo la kutembelea hospitali hiyo ni kuangalia utoaji wa huduma za afya zinazotolewa katika hospitali hiyo.
Baada ya kutembelea hospitali hiyo Waziri Ummy ameagiza Idara yote ya magonjwa ya ndani (Internal Medicine) iliyopo hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuhamia mara moja katika hospitali hiyo wakiwemo Madaktari,Madaktari Bingwa,Wauguzi pamoja na wataalmu wengine wa idara hiyo.
Wakati huo huo Waziri Ummy ameagiza kuhamisha wagonjwa waliopo wodi namba 3,4,5,6,7 na 8 zilizopo kwenye jengo la Mwaisela Muhimbili na kupelekwa hospital ya Mloganzila isipokuwa wagonjwa walio mahututi na wenye sababu maalumu na baada ya kuondoka wagonjwa hao wodi hizo zifanyiwe ukarabati mara moja. .”Nawaagiza waganga wafawidhi wa hospitali za Rufaa za Temeke,Mwananyamala na Amana kuanzia sasa rufaa zote za wagonjwa wa magonjwa ya ndani zije Mlongazila”, Alisema Mhe.Ummy.

Aidha, Waziri Ummy alisema Wizara imeshapokea Hospitali za Rufaa za Mikoa kutoka TAMISEMI hivyo amemuagiza Katibu mkuu wa Wizara hiyo kukamilisha kuwapangia baadhi ya Madaktari Bingwa waliopo hospitali hiyo ya Taifa na kuwapeleka hospitali za Rufaa za Mkoa na Kanda mapema Februari mwaka huu.
“Tumeomba kibali Utumishi wa Umma ili kuwahamisha Madaktari Bingwa zaidi ya ishirini (20) waliopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) pamoja na mishahara yao,”Madaktari wetu ni Wazalendo wapo tayari kwenda kutoa huduma za matibabu ya kibingwa kwenye hospitali zetu za Mikoa na Kanda”.
Alisema Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kwa dhati kuwahudumia wananchi wote ikiwemo kupata huduma za matibabu ya kibingwa bila kubagua hivyo Wizara yake imejipanga kununua vifaa na vifaa tiba na kuvisambaza kwenye hospitali hizo za rufaa za Mikoa. Alitaja Madaktari bingwa watakaohamishiwa kwenye hospitali za rufaa za mikoa na kanda miongoni mwao ni wa Magonjwa ya akina Mama na  Uzazi, Watoto,Upasuaji wa jumla,Radiolojia,Usingizi Macho pamoja na Magonjwa ya ndani.
Mloganzila ni Hospitali ya Taaluma na Tiba ambayo imewekwa vifaa tiba vya kisasa na teknolojia ya hali ya juu na ina vitanda 571 vya kulaza wagonjwa  na vyumaba 13 vya upasuaji na inatoa huduma masaa ishirini na nne.
Imetolewa na

Catherine Sungura
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Afya
10/1/2018



HAYA NDIYO ALIYOYASEMA WAZIRI UMMY ALIPOTEMBELEA MLOGANZILA

Jumanne, 9 Januari 2018

DKT. FAUSTINE NDUGULILE MKOANI KIGOMA

- Hakuna maoni

DKT. FAUSTINE AVIAGIZA VYOMBO VYA USALAMA MKOANI KIGOMA KUIMARISHA MIFUMO YA UDHIBITI WA UPOTEVU WA DAWA.

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akihesabu harambee ndogo aliyoiongoza pindi alipofanya ziara yake katika kata ya Kazuramimba, harambee hiyo itasaidia katika jitihada za kuendeleza ujenzi wa madarasa hayo, katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bi. Mwanamvua Mlindoko

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wazazi juu ya umuhimu wa virutubisho vilivyo kwa mama pindi ananyonyesha katika eneo la kupokea chanjo kwa watoto walio na umri chini ya miaka 5


Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua nembo ya MSD GOT katika dawa inayoonesha kuwa dawa hiyo imetolewa na Serikali na haipaswi kuuzwa

Kundi la wanakijiji wa kata ya Kazuramimba waliojitokeza kumsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile pindi alipofanya ziara katika Kata ya Kazuramimba kujionea ujenzi wa Madarasa ya shule.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisalimiana na baadhi ya wagonjwa katika Hospitali ya Kasulu Mkoani Kigoma




Na.WAMJWW. KIGOMA

Serikali imeviagiza vyombo vya usalama na kamati za Afya za vijiji kuimarisha mifumo yote ya udhibiti wa upotevu wa Dawa nchini, kwa kusimamia na kufuatilia kwa ukaribu hali ya upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba, ili kuondoa ubadhilifu unaofanywa na baadhi ya watu wasio waaminifu.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) katika ziara yake katika Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma ya kukagua utoaji huduma za Afya na kufuatilia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya jamii ambao unasisitiza ushirikishwaji wa jamii katika maamuzi,

“Niwaombe sana ndugu zangu wananchi tuwe walinzi, hiyo dawa ingeweza kukusaidia wewe, au ndugu yako, hivyo kushiriki katika ubadhilifu huo ni kujiumiza mwenyewe” alisema Dkt. Ndugulile.

Katika kupunguza vifo vya kina mama na watoto Dkt. Faustine amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewekeza kiasi cha shilingi Milioni 400 katika Halmashauri 175, kikiwemo kituo cha Afya cha Uvinza , fedha zitakazotumika kuboresha na kujenga vyumba vya kutolea huduma ya dharura wakati wa kujifungua, nyumba za watumishi pamoja na maabara.

Dkt. Faustine aliendelea kusema kwamba, Serikali inaendelea kufanya vizuri barani Afrika na Dunia kwa ujumla kwa upande wa utoaji chanjo, kwani imefikia asilimia 97 ya walengwa  wote wanaohitaji chanjo nchini jambo linalosaidia kutunza Afya za watu katika jamii.

Dkt. Ndugulile aliongeza kuwa anatambua uhaba wa watumishi unaovikabili vituo vingi vya Afya katika Wilaya ya Uvinza ambao umefikia asilimia 66 na kuahidi kulifanyia kazi ombi hilo ili kupunguza  changamoto katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile ameendelea kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuongeza Bajeti ya dawa , kutoka Bilioni 30 mpaka Bilioni 270 wa mwaka huu wa fedha hali iliyosaidia kuimarisha mapambano dhidi ya maradhi mbali mbali.

Aidha, Dkt. Ndugulile aliwapongeza wananchi wa kata ya Kazuramimba kwa kuonesha kwa vitendo utayari wao wa kusukuma guruduma la maendeleo ya elimu katika Kijiji hicho kwa kuamua kujenga madarasa ya shule katika Kijiji cha Nyanganga kilicha kata ya Kazuramimba ili kuweza kuwakomboa watoto wao na janga la ujinga na umasikini.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bi Mwanamvua Mlindoko ameeleza faida ya mradi wa ujenzi wa madarasa ikiwemo ongezeko la ufaulu kutoka wanafunzi 4115  mwaka 2017 huku waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza ni wanafunzi 1641 ambao ni sawa na asilimia 36 tu, hivyo kutokana na ujenzi wa madarasa haya utasaidia wanafunzi 2482 sawa na asilimia 64 kuendelea na elimu.

Jumatano, 3 Januari 2018

MAGONJWA YASIYO YAKUAMBUKIZA YACHANGIA ASILIMIA 27 YA VIFO VYOTE NCHINI

Kaimu Mkurugenzi magonjwa yasiyo yakuambukiza Dkt. Sarah Maongezi akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo katika picha) katika kikao kilichofanyika mapema leo katika ukumbi wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road kikihusu tuzo ya Elimu kwa jamii waliopata kutoka Shirikisho la kimataifa la magonjwa yasiyo yakuambukiza mwishoni mwa mwaka katika mkutano wa kimataifa uliofanyika katika falme zakiarabu.

Kaimu Mkurugenzi magonjwa yasiyo yakuambukiza Dkt. Sarah Maongezi akipokea tuzo ya Elimu kwa jamii kutoka kwa Mwenyekiti wa TANCDA Dkt. Tatizo Waane mapema leo katika ukumbi wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road, Wapili kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TANCDA Andrew Swai.

Kaimu Mkurugenzi magonjwa yasiyo yakuambukiza Dkt. Sarah Maongezi akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo katika picha) katika kikao kilichofanyika mapema leo katika ukumbi wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road kikihusu tuzo ya Elimu kwa jamii waliopata kutoka Shirikisho la kimataifa la magonjwa yasiyo yakuambukiza mwishoni mwa mwaka katika mkutano wa kimataifa uliofanyika katika falme zakiarabu, pembeni yake ni Mwenyekiti wa TANCDA Dkt. Tatizo Waane.


Na WAMJWW, Dsm

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yasema kuwa magonjwa yasiyo yakuambukiza yanachangia kiasi kikubwa katika vifo vyote vinavyotokea hapa nchini.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa magonjwa yasiyokuwa yakuambukiza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Sarah Maongezi wakati akipokea tuzo kutoka kwa TANCDA waliopata mwishoni mwa mwaka huu kutoka katika Shirikisho la Kimataifa la Magonjwa yasiyo yakuambukiza.

“Muongeze juhudi katika kupambana na magonjwa hayo ambayo yanachangia asilimia27 ya vifo vyote hapa Tanzania” Alisema Dkt Maongezi.

Dkt Maongezi aliendelea kusema kwamba Serikali imedhamiria kwa nia kabisa katika kupambana na magonjwa haya kwa kuamua kushirikiana na Asasi mbali mbali nchini ili kutimiza azma hiyo ya kupambana na magonjwa haya.

“Serikali pekee yetu hatuwezi na ndio maana tukashirikiana na Asasi kama TANCDA  inayojumuisha vyama vingine kama vile, Taasisi ya Saratani, Taasisi ya Magonjwa ya Moyo, Taasisi ya Mfumo wa Hewa na Taasisi ya Kisukari ambazo kwa ujumla zimejenga ushirikiano katika kupambana na magonjwa haya” Aliongeza Dkt. Maongezi.

Aidha Dkt. Maongezi amewahasa TANCDA kuongeza juhudi na kasi zaidi katika kupambana na magonjwa haya ili kuisaidia jamii kubwa ya Watanzania inayoangamia kutokana na kukosa elimu juu ya magonjwa hayo.

Dkt. Maongezi amewashukuru Waandishi wa Habari wote kwa mchango mkubwa wanaoendelea kuutoa katika kuisaidia jamii ya Tanzania hususani katika kupambana na Magonjwa yasiyo yakuambukiza kwa kuandika Makala za magazetini na vipindi vya Redioni na Tv, na kuwahasa kuendelea kufanya kazi hivyo ya kuelimisha jamii kwa juhudi.

Nae Makamu Mwenyekiti wa TANCDA Pro Andrew Swai ametoa wito kwa Asasi hizo kufanya tafiti zaidi katika maeneo mbali mbali bila kusahau vijijini, ili kuweza kufahamu idadi kamili ya watu waliohathirika na maradhi hayo na kurahisisha kufikisha ujumbe katika maeneo hayo.

“TANCDA inatakiwa kujitanua ili waweze kuwafikia watu wote, pia ule ujumbe unaopelekwa uweze kuwafanya watu ili aweze kubadilika”. Alisema Prof. Andrew Swai.