Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 9 Aprili 2018

TAARIFA KWA UMMA

- Hakuna maoni

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO


TAARIFA KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI KWA KIPINDI CHA JANUARI HADI MACHI 2018 ILIYOTOLEWA NA MHE. UMMY MWALIMU (MB); WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, TAREHE 9 APRILI, 2018.

Ndugu Wanahabari,
Serikali kupitia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imekuwa ikitoa taarifa ya mwenendo wa mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu na hatua zinazochukuliwa kudhibiti ugonjwa huu Kuanzia Januari hadi kufikia tarehe 31 Machi 2018, jumla ya wagonjwa 1448, wametolewa taarifa, na kati ya hao 27 wamepoteza maisha.

Kwa kipindi cha Januari wagonjwa 365 na vifo 9 walitolewa taarifa, Februari wagonjwa 996 na vifo 18 na Machi wagonjwa 87 bila kifo. Mwenendo wa takwimu hizi za ugonjwa wa Kipindupindu zinaonyesha kuwa idadi ya wagonjwa na vifo imepungua kwa kiasi kikubwa. Aidha, Mkoa wa Dodoma umeongoza kwa kipindi cha Januari hadi Machi kwa kuripoti jumla ya wagonjwa 583 kati ya 1,448 walioripotiwa nchi nzima sawa na asilimia 40.3%, ikifuatiwa na Ruvuma 374 (25.8%), Rukwa 276 (19.1%), Iringa 88 (6.1%), Morogoro 56 (3.9%), Songwe 37 (2.6%), Kigoma 25 (1.7%) na Manyara 9 (0.6%).

Kwa mwezi Machi 2018, jumla ya wagonjwa 87 bila kifo wametolewa taarifa, ambapo ni pungufu kubwa sawa na asilimia 91.3% ukilinganisha na mwezi Februari 2018 ambapo kulikuwa na jumla ya wagonjwa 996 na vifo 18. Kwa mwezi Machi mikoa na halmashauri ambazo zimeendelea kutoa taarifa ya ugonjwa wa Kipindupindu nchini ni Dodoma (Mpwapwa-35, Chamwino-15, Dodoma Mjini-6, Kongwa-5), Ruvuma (Nyasa-18, Mbinga-5), Rukwa (Sumbawanga Vijijini-5), na Iringa (Kilolo-2).

Ukilinganisha idadi ya wagonjwa waliotolewa taarifa mwezi Februari na ule wa mwezi Machi, mikoa imeweza kufanikiwa kudhibiti ugonjwa huu kwa kiasi kikubwa. Mfano mkoa wa Morogoro umefanikiwa kudhibiti kikamilifu kutoka wagonjwa 56 mwezi Februari na kutokuwa na wagonjwa wowote mwezi Machi. Mikoa mingine iliyofanikiwa kupunguza idadi ya wagonjwa kwa sehemu kubwa katika kipindi cha mwezi mmoja ni Iringa (punguzo la asilimia 97.7%), Rukwa (punguzo la asilimia 96.1%) na Ruvuma (punguzo la asilimia 92.7%). Mkoa wa Dodoma pia umefanikiwa kupunguza idadi ya wagonjwa kwa takribani asilimia 83% katika kipindi cha mwezi mmoja.

Wizara inatoa pongezi kwa Mikoa kwa jitihada mbalimbali walizozichukuwa kudhibiti ugonjwa huo ambayo imepelekea kupunguza kwa sehemu kubwa kuenea kwa ugonjwa huu katika kipindi cha mwezi wa Machi.

Ndugu Wanahabari,
Ingawa takwimu hizi zinaonyesha kuwa ugonjwa umepungua, bado uwezekano wa kuenea kwa ugonjwa wa Kipindupindu na kupata maambukizi mapya ni tishio hata kama ni Halmashauri moja tu itakuwa na wagonjwa wa Kipindupindu. Tishio hili inaongezeka katika msimu huu wa mvua ambapo inaweza kuongeza kasi ya kuenea kwa maambukizi ya Kipindupindu. Hivyo tunahitaji kuzidisha juhudi za kuzuia ugonjwa huu, kwa kusimamia kikamilifu maelekezo na miongozo stahiki inayotolewa. 

Ni dhahiri kuwa ushirikishwaji wa sekta zote kwa ngazi mbalimbali na jamii kwa ujumla ni muhimu sana katika kukabiliana na ugonjwa wa Kipindupindu.  Wizara inasisitiza kuwa wadau wote wapewe nafasi katika mapambano haya kupitia vikao mbalimbali za kujadili udhibiti wa ugonjwa wa Kipindupindu kwenye Halmashauri na Mikoa. Viongozi wa dini, watu mashuhuri na waganga wa tiba mbadala pia wasaidie kuhamasisha jamii zao kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huu.

Ndugu Wanahabari,
Wizara inaendelea kuwasihi wananchi kuungana na Halmashauri, Mikoa, hasa iliyotoa taarifa kipindi cha Januari hadi Machi, pamoja na Wizara katika juhudi za kupambana na kuenea kwa ugonjwa wa Kipindupindu.  Jamii izingatie kanuni za usafi binafsi na usafi wa mazingira, ikiwa ni pamoja na:
1.   Kujenga na kutumia vyoo bora katika maeneo tunayoishi.
2.   Kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni kabla ya kula, baada ya kutumia choo, na baada ya kumsafisha mtoto aliyejisaidia.
3.   Kunywa maji safi na salama yaliyotakaswa kwa dawa (kama vile water guard) au yaliyochemshwa na kupoa.
4.   Kuzingatia ushauri na elimu sahihi kuhusu ugonjwa wa Kipindupindu, ili jamii iondokane na imani potofu kuhusu Kipindupindu.
5.   Kufikisha wagonjwa wa Kipindupindu mapema katika vituo vya kutolea huduma ili wawahi kupata matibabu.
6.   Kutotiririsha maji   taka   ovyo

Vile vile, Wizara inasisitiza yafuatayo yasimamiwe kwenye Halmashauri na Mikoa yote nchini,
1.   Utoaji wa taarifa sahihi za ugonjwa wa Kipindupindu na kwa wakati kwa kufuata miongozo iliyopo.
2.   Usimamizi wa utekelezaji wa miongozo katika kuzuia na kudhibiti ugonjwa ni pamoja na;
o   Usimamizi wa utekelezaji wa sheria ndogondodo za usafi wa mazingira ili kuimarisha matumizi ya vyoo.
o   Usafi wa mazingira pamoja na udhibiti wa biashara za chakula na pombe za kienyeji katika mitaa.
o   Kuzingatia agizo la Mheshimiwa Rais la kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.
3.   Kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yote mijini na vijijini hasa wakati wa mlipuko wa Kipindupindu. Hii ni pamoja na:
o   Mamlaka za maji katika ngazi zote ziweke mkazo wa kuwepo kwa vyanzo mbadala vya maji.
o   Utakasaji wa maji ya bomba kwa njia ya kutumia klorini ufanyike kama miongozo inavyotaka na ufuatiliaji wa ubora wa maji ufanyike kulingana na miongozo.

Hitimisho
Wizara kwa ukaribu itaendelea kufuatilia mwenendo wa ugonjwa wa Kipindupindu nchi nzima. Aidha, Wizara inawashukuru wadau wote wa sekta mbalimbali, wataalamu na watumishi, waandishi wa habari na wananchi kwa michango yao mbalimbali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kipindupindu nchini.  


Asanteni sana

Jumapili, 8 Aprili 2018

MUENDELEZO WA MKUTANO WA UJENZI WA VIWANDA VYA DAWA,VIFAA NA VIFAA TIBA.

- Hakuna maoni








Kikao cha cha kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa nchini, kiliendelea katika ofisi ndogo ya Wizara ya Afya jijini Dar es salaam, kikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage huku wakikutana na kamati ya Simiyu Pharma Project, Keko pharmaceutical 1997 Limited, Tanzania Pharmaceutical Industry (TPI) na PST.

Ijumaa, 6 Aprili 2018

CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI NI SALAMA, WAZIRI UMMY

- Hakuna maoni


Mhe. Ummy Mwalimu (MB) awatoa hofu viongozi wa dini pamoja na wananchi kwa ujumla kwamba chanjo hii haizuii binti kutopata watoto katika maisha yake ya baadae bali ni kinga dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi".  Kinga ni bora kuliko tiba, hivyo ni vyema tukashirikiana kuweza kuwaokoa mabint wetu na vifo".

Chanjo mpya ya kuwakinga wasichana wenye umri wa miaka 14 dhidi ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi itaanza kutolewa mara baada ya uzinduzi wa kitaifa tarehe 10 Aprili, 2018 na itahusisha mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar pia itatolewa kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya Serikali, binafsi na huduma mkoba kwenye shule na sehemu mbalimbali. Chanjo hii itatolewa mara mbili ili kupata kinga kamili(chanjo ya pili itatolewa baada ya miezi sita)

UFAFANUZI KUHUSU TAKWIMU ZA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI NCHINI.

- Hakuna maoni

TANZANIA YAPATA TAKRIBANI WAGONJWA WAPYA WA SARATANI 50,000 KILA MWAKA.

- Hakuna maoni
Shekhe wa Mkoa wa Dar es salaam Alhaj Musa Salum akiishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kujali Afya za wananchi, akiwa katika kikao cha kuhamasisha chanjo ya mlango wa kizazi kwa mabinti kilichoandaliwa na Wizara ya Afya kupitia mpango wa chanjo.

Askofu Wa kanisa la mito ya baraka Bruno Mwakibolwa akichangia hoja mbele ya Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu na viongozi wengine wa dini (hawapo kwenye picha)  wakati wa kikao kuhamasisha chanjo ya mlango wa kizazi kwa mabinti kilichofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akitoa mapendekezo mbele ya viongozi wa dini waliokutana mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa kikao cha kuhamasisha chanjo ya mlango wa kizazi.

Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi akimkaribisha Mhe. Ummy Mwalimu ili azungumze na viongozi wa dini.

Meneja Mpango wa Taifa wa Chanjo Dkt. Dafrossa Lymo akiwasilisha taarifa kuhusu masuala ya chanjo nchini mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Viongozi wa Dini (hawapo kwenye picha).

Viongozi wa dini ya Kikristo wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mhe.Ummy Mwalimu wakati wa kikao na viongozi wa dini zote cha kuhamasisha chanjo ya mlango wa kizazi.

Viongozi wa dini ya kiislamu wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mhe.Ummy Mwalimu wakati wa kikao na viongozi wa dini zote cha kuhamasisha chanjo ya mlango wa kizazi.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Sub wakati wa kikao kuhamasisha chanjo ya mlango wa kizazi kwa mabinti kilichofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiwa na viongozi wa dini wakati wa kikao kuhamasisha chanjo ya mlango wa kizazi kwa mabinti kilichofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.


Na WAMJW-Dar es salaam.

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa kila mwaka Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa wapya wa Saratani 50,000 huku Saratani ya mlango wa kizazi ikiongoza ikifuatiwa na saratani ya matiti na saratani ya ngozi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) wakati wa mkutano na viongozi wa dini, uliofanyika mapema leo katika ukumbi wa Serena jijini Dar es salaam.

“Kila mwaka Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa wa Saratani wapya 50,000, katika kila wagonjwa 100 wanaokwenda katika Hospitali ya Ocean Road wagonjwa 32 wanasaratani ya mlango wa kizazi, inafuatia saratani ya matiti ambayo takribani wagonjwa 12 katika wagonjwa 100, saratani ya tatu ni saratani ya Ngozi” alisema Mhe. Ummy Mwalimu.

Aliendelea kusema kuwa Saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti zinachukua takribani asilimia 45 ya wagonjwa wa saratani nchini, huku Saratani ya tezi dume ikiwa na asilimia 2.

Kwa upande mwingine Mhe. Ummy Mwalimu amewaomba viongozi wakuu wa madhehebu ya dini kuwahimiza wananchi kuwapeleka wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 14 kupata chanjo ya kuwakinga na saratani ya mlango wa kizazi inayotarajiwa kuzinduliwa tarehe 10 Aprili,2018 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam

Waziri Ummy amesema kwamba kama viongozi wa dini ni vyema kufikisha ujumbe huu kwa waumini wao na kuwaunga mkono ili kuweza kuwafikia wasichana laki 6 nchi nzima ili kuweza kuwaokoa na vifo vipatavyo asilimia 50 vitokanavyo na saratani nchini"idadi hii ni kubwa sana,hivyo juhudi na ushirikiano zaidi vinahitajika katika kupunguza vifo hivi.

Hata hivyo aliwatoa hofu viongozi hao pamoja na wananchi kwa ujumla kwamba chanjo hii haizuii binti kutopata watoto katika maisha yake ya baadae bali ni kinga dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi".  Kinga ni bora kuliko tiba, hivyo ni vyema tukashirikiana kuweza kuwaokoa mabint wetu na vifo".

Chanjo mpya ya kuwakinga wasichana wenye umri wa miaka 14 dhidi ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi itaanza kutolewa mara baada ya uzinduzi wa kitaifa tarehe 10 Aprili, 2018 na itahusisha mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar pia itatolewa kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya Serikali, binafsi na huduma mkoba kwenye shule na sehemu mbalimbali. Chanjo hii itatolewa mara mbili ili kupata kinga kamili(chanjo ya pili itatolewa baada ya miezi sita)

Kwa upande mwingine Mhe. Ummy mwalimu alimshukuru Mhe. Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuongeza bajeti ya dawa za Saratani kutoka shilingi Milioni 700 hadi Bilion 7 jambo lililosaidia sana katika matibabu ya Saratani.

“Nashukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kupandisha bajeti ya dawa za saratani kutoka shilingi Milioni 700 hadi Billion 7, leo nasimama kifua mbele, angalau katika wagonjwa 10, wagonjwa 7 watakwambia tumepata dawa bila malipo yoyote” alisema Mhe. Ummy Mwalimu.


TAARIFA KWA UMMA

- Hakuna maoni


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewaomba viongozi wakuu wa madhehebu ya dini kuwahimiza wananchi kuwapeleka wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 14 kupata chanjo ya kuwakinga na saratani ya mlango wa kizazi inayotarajiwa kuzinduliwa tarehe 10 Aprili,2018 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam

Waziri Ummy amesema kwamba kama viongozi wa dini ni vyema kufikisha ujumbe huu kwa waumini wao na kuwaunga mkono ili kuweza kuwafikia wasichana laki 6 nchi nzima ili kuweza kuwaokoa na vifo vipatavyo asilimia 50 vitokanavyo na saratani nchini"idadi hii ni kubwa sana,hivyo juhudi na ushirikiano zaidi vinahitajika katika kupunguza vifo hivi.

Aidha, alisema hapa nchini kati ya wagonjwa mia moja wa Saratani, wagonjwa 34 wana saratani ya kizazi". saratani  ya mlango wa kizazi inaongoza na inafuatiwa na saratani ya matiti kwa asilimia 13 ya wagonjwa wa Saratani nchini"alisema Waziri Ummy.

Hata hivyo aliwatoa hofu viongozi hao pamoja na wananchi kwa ujumla kwamba chanjo hii haizuii binti kutopata watoto katika maisha yake ya baadae bali ni kinga dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi".  Kinga ni bora kuliko tiba, hivyo ni vyema tukashirikiana kuweza kuwaokoa mabint wetu na vifo".

Chanjo mpya ya kuwakinga wasichana wenye umri wa miaka 14 dhidi ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi itaanza kutolewa mara baada ya uzinduzi wa kitaifa tarehe 10 Aprili, 2018 na itahusisha mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar  pia itatolewa kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya Serikali, binafsi na huduma mkoba kwenye shule na sehemu mbalimbali. Chanjo hii itatolewa mara mbili ili kupata kinga kamili(chanjo ya pili itatolewa baada ya miezi sita)


Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-afya
6/4/2018

WAUGUZI NA WAKUNGA WANATAKIWA KUZINGATIA MAADILI SEHEMU ZAO ZA KA

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wauguzi na wakunga hawapo pichani wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
 

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwakabidhi vyeti vya kufanya vizuri baadhi ya wawakilishi wa  mashirika yanayoshirikiana na Wizara ya Afya wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
 
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Bw. Gustav Moyo akiongea na wauguzi na wakunga hawapo pichani wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
 

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau,wakunga na wauguzi wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
 
Baadhi ya Wauguzi na Wakunga wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
 
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Cha uuguzi na Ukunga Dodoma wakiwakilisha salamu zao kwa kutumia wimbo kwa  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
 
 
Na WAMJW-Dodoma
Serikali imewataka Wauguzi na Wakunga nchini kufuata na kusimamia  misingi ya maadili ya taaluma zao wakati wa kutoa huduma.

Hayo yamesemwa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini. 

Najua kuwa Idara ya Huduma za Uuguzi na Ukunga inalishughulikia suala la maadili kwa wauguzi na wakunga hivyo nitoe msisitizo tena huduma za Uuguzi na Ukunga zinapimwa zaidi na uadilifu wa mtoa huduma hivyo muendelee kusimamia kwa ukaribu misingi ya maadili ya taaluma zenu amesema Dkt Ndugulile.

Aidha, Dkt Ndugulile amewataka Wauguzi na Wakunga kupitia vyama vyao vya kitaaluma kushirikiana na Baraza la Uuguzi na Ukunga kuendelea kuwakumbusha mara kwa mara wauguzi kuhusu maadili ya taaluma yenu.

Mteja anapokuja kwenye vituo vya kutolea huduma anategemea kupata huduma ya upendo na huruma, anategemea kupewa maneno ya faraja na matumaini hivyo basi, wale wote wanaoichafua taaluma yenu kwa kutotekeleza wajibu wao kwa wakati, kuwadhalilisha, kuwashambulia au kutowasikiliza wateja wenu wabainishwe na wahimizwe kujirekebishaamefafanua Dkt Ndugulile.

Ninawapongeza sana kwa kuweka msisitizo kwa mambo yanayohusiana na kupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga hiyo ni moja ya agenda muhimu ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuliameongeza Dkt. Ndugulile.

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amesema kuwa serikali inazifanyia kazi changamoto zinazowakumba Wauguzi na Wakunga  kwa namna mbalimbali ambapo hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuongeza kiwango cha bajeti kwa ajili ya kuimarisha hali ya upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba, na vitendanishi katika Bohari ya Dawa.

kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Bw. Gustav Moyo amesema kuwa kongamano hilo limeandaliwa ili kuwakumbusha wauguzi na wakunga maadili ya taaluma yao pindi wanapokuwa sehemu zao za kazi.

Aidha Bw. Moyo amesema kuwa Akizungumzia Kongamano hilo limebeba kauli mbiu isemayo isemayo Kuelekea Huduma za Uuguzi na Ukunga Zinazozingatia Ubora, Utu, Huruma na Usalama wa Wagonjwa; Katika Kupunguza Vifo vya Akinamama na Watoto.
 

Alhamisi, 5 Aprili 2018

WAWEKEZAJI 38 WAONESHA UTAYARI UJENZI WA VIWANDA VYA DAWA NA VIFAA TIBA,...

- Hakuna maoni


Aliyoyasema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. UMMY MWALIMU katika kikao cha kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa nchini, kilichokutanisha wadau mbalimbali wa Uwekezaji katika Sekta ya Dawa, Vifaa na Vifaa tiba

HUDUMA ZA DRARURA ZABORESHWA KATIKA HOSPITALI YA KANDA YA RUFAA MBEYA.

- Hakuna maoni

Jumatano, 4 Aprili 2018

SERIKALI YAWATAKA WAWEKEZAJI KUJITOKEZA KWA WINGI KATIKA UJENZI WA VIWANDA VYA DAWA

- Hakuna maoni
Wadau na Wafanyabiashara wa Sekta ya Dawa wakifuatilia kwa umakini taarifa kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (Hayupo kwenye picha) katika kikao cha kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya Dawa, tukio limefanyika mapema leo jijini Dar es salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akichangia hoja mbele ya Wadau na Wafanyabiashara wa Sekta ya Dawa katika kikao cha kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya Dawa.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akisisitiza jambo mbele ya wadau na  Wafanyabiashara katika kikao cha kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda uliofanyika katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiteta jambo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage katika kikao cha Wadau wa Sekta ya Dawa katika kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa nchini.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Idara Kuu ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya.

 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijageakiteta akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wake Prof. Elisante Ole Gabriel.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage wakiwa na Wadau wa Sekta ya Dawa katika kikao cha kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya Dawa na vifaa Tiba hapa nchini.


Na WAMJW. Dar es salaam.

SERIKALI yawataka Wadau wa Uwekezaji nchini kujitokeza kwa wingi kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya dawa ili kusaidia kupunguza gharama kubwa za matumizi zinazotokana na kununua, kusafirisha na kuhifadhi dawa zinazotoka nje ya nchi.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe.  UMMY MWALIMU katika kikao cha kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa nchini, kilichokutanisha wadau mbalimbali wa Uwekezaji katika Sekta ya Dawa, Vifaa na Vifaa tiba

Waziri Ummy alisema kuwa Serikali imekuwa ikitumia zaidi ya tirion moja kunuua dawa kutoka nje, hivyo kupitia uwekezaji wa viwanda vya dawa nchini itasaidia kupunguza adha hiyo nchini kwa kiwango kikubwa.

Nae Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji nchini Mhe. Charles Mwijage amewataka wote wenye nia ya kuwekeza katika Ujenzi wa viwanda vya dawa, vifaa na vifaa tiba lazima wahakikishe wanashirikiana na taasisi za Utafiti zilizopo nchini ili kuangalia mahitaji na aina dawa zinazohitajika.

Aidha, Mhe. Charles Mwijage amesema kuwa Uwekezaji na ujenzi wa Viwanda nchini utasaidia kupunguza tatizo la ajira na kuchochea Maendeleo ya ukuaji wa Uchumi katika ngazi ya watu na taifa kwa ujumla.