Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 20 Agosti 2018

TAARIFA KWA UMMA

- Hakuna maoni
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU VYETI VYA WAHITIMU WA KADA ZA AFYA

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kuwajulisha kuwa imepokea vyeti vya wahitimu kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).Vyeti hivyo ni kwa wahitimu waliofanya mitihani  2016, mwezi Septemba na Oktoba 2017 kwa Mafunzo ya Astashada na Stashahada ya Uuguzi na Ukunga, Mafunzo ya Astashahda ya Wahudumu wa Afya ya Jamii na Mafunzo ya Sayansi Shirikishi za Afya (Utabibu, Wateknolojia wa Maabara, Famasia, Sayansi ya Afya ya Mazingira, Utunzaji kumbukumbu za Afya, Mazoezi ya viungo ,Utabibu wa Meno na Wateknolojia Macho).
Wizara inawajulisha wahitimu wa mafunzo hayo kuwasiliana na Wakuu wa Vyuo kuanzia tarehe 20/08/2018 ili kuweza kupewa utaratibu wa kwenda kuchukua vyeti vyao kwenye vyuo walivyopatia mafunzo hayo.
Imetolewa na,
KATIBU MKUU (AFYA)
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
20 Agosti, 2018.

Ijumaa, 17 Agosti 2018

PICHA MBALI MBALI ZA MATUKIO YA KUFUNGA KWA MKUTANO WA WAGANGA WAKUU WA MIKOA NA HALMASHAURI.

- Hakuna maoni
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na Waganga wakuu wa Mikoa na Halmashauri wakati wa kufunga mkutano wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri hawapo pichani ,kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa OR-TAMISEMI Dkt. Zainabu Chaula .
 
 Mkurugenzi wa Utawala na Rasirimali watu kutoka Wizara ya Afya Deodata Makani akiongea na Waganga wakuu wa Mikoa na Halmashauri wakati wa kufunga mkutano wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri  hawapo pichani uliofanyika jijini Dodoma.

Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri wakifuatilia kwa makini maada mbalimbali zilizokuwa zinatolewa na wawasilishaji mbalimbali hawapo pichani wakati wa kufunga mkutano wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri uliofanyika jijini Dodoma.

DKT. SUBI AWAHASA WANAWAKE KUWAI KLINIKI PINDI WANAPOHISI WANAUJAUZITO.

- Hakuna maoni
Mkurugenzi wa huduma za kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na  Watoto Dkt.Leonard Subi

Na.WAMJW - Dodoma

Akina Mama wajawazito wametakiwa  kuwahi kliniki mara wanapohisi wana ujauzito na kufuata ushauri wa wataamu wa afya  ili kuwakinga watoto wanaotarajia kujifungua dhidi ya maabukizi ya Virus vya UKIMWI
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa huduma za kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na  Watoto Dkt.Leonard Subi mjini Dodoma hivyo kuwataka wananchi kuchukua hatua katika kujikinga na maradhi mbalimbali ikiwemo Virusi Vya Ukimwa (VVU).
Amesema Utafiti uliofanywa mwaka 2010 maambukizi ya Virus yalikua  asilimia 26  kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto huku utafiti uliofanywa mwaka  2016/2017 unaonesha kuwa maambukizi haya yamepungua na kufikia asilimia 7.6 ambapo Serikali imesema inatarajia maambukizi haya yapungue mpaka asilimia 2 ifikapo 2020-2021.
“Ni  muhimu kwa wajawazito kuhudhuria kliniki na kupima VVU hii itasaidia kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, malezi na makuzi  mzuri ya Mtoto yanategemea wazazi wote wawili yaani baba na mama wazazi wote wanaaswa kushirikiana hasa katika kupima afya afya ili mtoto atakaezaliwa asiwe na maambukizi ya VVU”Alisema Dkt.Subi. 
Aliongeza kuwa  moja ya changamoto inayokwamisha mpango huu ni  wanaume kukumbatia mila na destuli za kutoandamana na wenzi wao kliniki wakati wa kipindi cha ujauzito,
“hivyo familia au makabila ambayo bado yanaona kwamba mwanaume kumsindikiza mwenzi wake kliniki ni kujishushia hadhi waachane nazo”.
Aidha, Dkt.Subi amewataka vijana kuchukua hatua za kwenda katika vituo vya afya kupata elimu ya uzazi na kupima afya zao maana wao ndio mama au baba wanaotarajiwa,mimba za utotoni ni hatari kwa afya zao na kama kuna tatizo lolote wafike katika vituo vya afya ili kupata msaada wa kitalaamu.
Alisisitiza kuwa vituo vya kutolea huduma za afya vyote nchini hivi sasa vinatoa huduma ya elimu bure kuhusiana na afya ya uzazi na endapo mama mjamzito atagundulika ana maambukizi ya VVU ataanzishiwa dawa ambazo zitamkinga mtoto asizaliwe na maambukizi ya  Virus vya UKIMWI.


Jumatatu, 13 Agosti 2018

WAZIRI UMMY AMSHUKURU BALOZI WA CANADA NCHINI TANZANIA KWA KUBORESHA SEKTA YA ÁFYA.

- Hakuna maoni

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiagana na Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe. Ian Myles mapema leo katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam baada ya mazungumzo juu ya Maboresho katika Sekta ya Afya.

Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe. Ian Myles (Wapili kushoto) akimweleza jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu mapema leo wakati alipotembelea katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam. Wakwanza kushoto ni ofisa wa Ubalozi wa Canada Susan Steffen.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimsikiliza kwa makini Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe. Ian Myles (Hayupo kwenye picha)

Picha ya Pamoja ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa na Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe. Ian Myles baada ya kikao cha kumuaga Balozi huyo kilichofanyika mapema leo katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.

WAZIRI UMMY AMSHUKURU BALOZI WA CANADA NCHINI TANZANIA KWA KUBORESHA SEKTA YA ÁFYA. 

Na WAMJW - DSM 

Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameishukuru Serikali ya Canada kupitia Balozi wake nchini Tanzania kwa ushirikiano walioonesha katika kuboresha sekta ya Áfya hususani katika Kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Ameyasema hayo mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Áfya jijini Dar es salaam wakati akiagana na Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe. Ian Myles anayetarajia kuondoka hivi karibuni hapa nchini.

Nae Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe Ian Myles  ameishukuru Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Áfya kwa kuendelea kutatua changamoto za sekta ya Áfya nchini.

Ijumaa, 10 Agosti 2018

TAMKO KUHUSU UGONJWA WA EBOLA ULIOTOKEA KATIKA NCHI JIRANI YA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO

- Hakuna maoni
TAMKO KUHUSU UGONJWA WA EBOLA ULIOTOKEA KATIKA NCHI JIRANI YA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO

Utangulizi
Ndugu wanahabari, 
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea kutoa taarifa kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Nchi hiyo ya DRC imetangaza tena kuwa na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola mnamo tarehe 1 mwezi Agosti, 2018, ambapo jumla ya wagonjwa 26 na vifo 10 vilitolewa taarifa na wagonjwa 4 kati yao walithibitishwa kimaabara kuwa na ugonjwa wa Ebola. Wagonjwa hawa wametokea katika vijiji/Maeneo ya Mangina ikiwa ni kama km 30 tu magharibi mwa mji wa Beni kwenye jimbo la Kivu Kaskazini linalopakana na nchi ya Uganda ikiwa ni kama km 100 tu, na pia likiwa karibu sana na nchi ya Rwanda. 
Huu ni mlipuko wa 10 wa ugonjwa wa Ebola kutokea nchini DRC, na umetokea wiki moja baada ya nchi hiyo kutangaza kuisha kwa mlipuko mwingine uliotokea mwezi Mei mwaka huu ambao ulikuwa katika jimbo la Equator, Magharibi mwa DRC, umbali wa zaidi ya km 2,000 kutoka eneo la huu mlipuko mpya uliotokea.
Ndugu wanahabari,
HADI SASA HAPA NCHINI TANZANIA HAKUNA MGONJWA YOYOTE ALIYEHISIWA AU KUTHIBITISHWA KUWA NA VIRUSI VYA EBOLA. Hata hivyo, kugunduliwa kwa ugonjwa huu kwenye jimbo la Kivu Kaskazini linalopakana na nchi za Uganda na Rwanda ni jambo la kutuweka kwenye wasi wasi kwani eneo hili liko karibu sana na nchi yetu kuliko eneo lingine lolote ambako ugonjwa huu umeshawahi kutokea kwenye nchi ya DRC. Hivyo nchi yetu ipo hatarini kuambukizwa ugonjwa huu kutokana na ukaribu na muingiliano wa watu, hasa kuhusiana na wasafiri wanaotoka na kuingia hapa nchini. 
Kwa sababu hizi, watanzania hatuna budi kuchukua tahadhari ya hali ya juu ili kujikinga na kudhibiti na ugonjwa wa Ebola.  Hivyo Wizara inapenda kutoa tahadhari ya ugonjwa huu kwa wananchi wote katika Mikoa yote ya Tanzania, lakini hasa ile inayopakana na nchi jirani za DRC, Uganda na Rwanda. Mikoa hiyo ni pamoja na Mwanza, Kagera, Kigoma, Katavi, Rukwa na Songwe. Aidha tahadhari na hatua stahiki zichukuliwe katika maeneo yote ya mipakani ambapo abiria wanaingia nchini kutoka nchi jirani.

Ugonjwa wa Ebola
Ugonjwa wa Ebola husababishwa na virusi vya Ebola ambavyo huambukiza kwa njia zifuatazo; 
Kugusa Damu au majimaji kutoka kwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo, 
Kugusa maiti ya mtu aliyekufa kwa ugonjwa huo, 
Kugusa wanyama (Mizoga na wanyama wazima) walioambukizwa kama vile Sokwe na Swala wa msituni. 
Dalili za Ugonjwa
Dalili za Ugonjwa huanza kuonekana kwa mtu aliyeambukizwa baada ya siku 2 hadi 21 tangu kupata maambukizi. Dalili hizo ni pamoja na;
Homa kali ya ghafla, 
Kulegea kwa mwili,
Maumivu ya misuli, 
Kuumwa kichwa na vidonda kooni. 
Mara nyingi dalili hizo hufuatiwa na kutapika, kuharisha, vipele vya ngozi na pia figo na Ini kushindwa kufanya kazi. 
Kwa baadhi ya wagonjwa kutokwa na damu ndani na nje ya mwili. 


Namna ya Kujikinga na ugonjwa wa Ebola:
Ugonjwa wa Ebola unaweza kuzuilika. Njia kuu za kujikinga na ugonjwa huu ni:-
Kuepuka kugusa au kuingiwa na mate, damu, mkojo, jasho, kinyesi, machozi na majimaji mengine yanayotoka mwilini mwa mgonjwa mwenye dalili za ugonjwa  wa Ebola
Kuepuka kushughulikia maiti ya mtu aliyefariki akiwa na dalili za Ebola; badala yake watoe taarifa kwa uongozi wa kituo cha huduma za Afya kwa ushauri.
Kuepuka kula nyama za Wanyama wa porini kama sokwe, swala na popo na pia kugusa mizoga ya Wanyama hao
Kuepuke mila na desturi  zinazoweza kuchelewesha kupata huduma muhimu na kuzidi kueneza ugonjwa wa Ebola.
Kuzingatia usafi wa mwili
Kutoa taarifa mapema kwa viongozi wa Serikali na wa huduma za Afya katika ngazi zote pale anapotokea mtu mwenye  dalili za Ebola.
Kuwahi katika vituo vya huduma za Afya pale mtu anapoona dalili za ugonjwa huu.




Hatua zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa na Wizara kufuatia kupatikana kwa taarifa ya Ugonjwa huu huko DRC 
Kufuatia kuwepo kwa taarifa hizi tangu mwezi Mei 2018, hatua zifuatazo zinaendelea/zimechukuliwa na Wizara ili kujiandaa kukabiliana na mlipuko huo:
Kufanya tathmini ya utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola nchini (Operational readiness assessment) kwa nchi nzima kwa kushirikiana na WHO na kuainisha mapungufu ambayo yanapaswa kufanyiwa kazi. Mapungufu hayo yanaendelea kuyafanyiwa kazi ili kujenga uwezo na utayari katika nchi yetu.
Tumetengeneza mpango mkakati wa kujiandaa na kupambana na mlipuko wa Ebola endapo utatokea nchini (Costed Ebola Contingency Plan). Mpango huu umeandaliwa kwa kushirikiana na WHO. Mpango umeainisha maeneo ya kujenga uwezo kwa wakati huu wa kujiandaa, pamoja na hatua za kuchukua endapo ugonjwa utaingia ikiwa ni pamoja na gharama zake.
Tumefanya mafunzo ya Timu za dharura (Rapid Response Teams) ngazi ya Taifa na katika Mikoa ya Dar es Salaam, Songwe, Rukwa, Katavi, Kigoma na Kagera
Tumeimarisha ufuatiliaji wa wasafiri mipakani (travellers entry screening) kwa kutumia vifaa vya kupima joto la mwili (thermo scanners) na fomu maalum za wasafiri
Wizara imepokea vifaa vya kukabiliana na Ebola kutoka WHO vikiwemo; Thermo scanners, Vifaa Kinga, au PPE, kama vile gloves, body bags, vifaa vya ufungashaji wa sampuli nk. Vifaa hivyo vimeanza kusambazwa mikoani kupitia MSD
Uelimishaji wa umma umefanyika na unaendelea kufanyika kwa kupitia vyombo vya habari vya kitaifa na kijamii, na mitandao ya kijamii. Vile vile vipeperushi na mabango vinaendelea kuandaliwa
Vikao vya uratibu vimefanyika katika ngazi ya taifa na mikoa ambayo ipo katika hatari zaidi. Pia ufuatiliaji wa karibu unaendelea kupitia Kituo cha ufuatiliaji wa magonjwa ya dharura cha Wizara (Public Health Emergency Operation Centre is on High Alert) 
Wataalam kutoka ngazi ya Taifa kwa sasa wako katika mikoa ya Kigoma Katavi Rukwa Kagera Kilimanjaro Mwanza Songwe na Mbeya kufanya tathmini ya utayari katika ngazi ya mikoa na Wilaya (Readiness Assessment)
Maandalizi yanaendelea kwa ajili ya kutekeleza kazi nyingine kama ifuatavyo:
Kufanya mafunzo katika mikoa iliyo salia ikiwemo Mwanza, Kilimanjaro na Mbeya ambayo imesalia katika ile mikoa nane iliyo katika hatari zaidi
Mafunzo ya waandishi wa habari 30 (media orientation)
Zoezi la udhibiti wa matukio ya dharura (simulation exercise) katika ngazi ya Taifa
Mafunzo kwa wasfirishaji wa sampuli kwenda katika maabara

Hitimisho
Nawaomba Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri wote nchini kuchukua Tahadhari na kuendelea kuelimisha wananchi wote juu ya ugonjwa huu na kuwataka kutokuwa na hofu ila kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huu kwani mpaka sasa hakuna mtu aliyethibitishwa kuugua ugonjwa huu hapa nchini. 

Aidha Wizara itaendelea kushirikiana na sekta mbalimbali katika kuimarisha ufuatiliaji na kuendelea kutekeleza mikakati ya kudhibiti ili ugonjwa huu usiingie nchini. Vilevile Wizara itaendelea kutoa taarifa pamoja na Elimu kwa Jamii kadri itakavyohitajika. 
Imetolewa na 

Ummy A. Mwalimu (Mb)
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, 
Jinsia, Wazee na Watoto
10/08/2018

IDADI YA WANAWAKE WANAOTUMIA HUDUMA ZA ZA UZAZI WA MPANGO ZAONGEZEKA NCHINI.

- Hakuna maoni
Waziri wa Maendeleo kutoka nchi ya Uingereza Mhe.  Penny Mordaunt (katikati) akimsalimia mtoto mchanga aliyebebwa na baba yake katika jengo la Kliniki ya Baba, Mama Na Mtoto. Kulia ni Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.





Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisoma mbao ya matangazo katika Zahanati ya Tabata jijini Dar es salaam pindi alipofika kupokea ugeni wa Waziri wa Maendeleo kutoka nchi ya Uingereza.

Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa Elimu juu ya umuhimu wa kukata Bima ya Áfya kwa mtoto (Toto Afya Card) kwa mmoja kati ya wazazi  waliofika katika Zahanati ya Tabata kupata huduma za matibabu ya mtoto.

Mshauri wa masuala Ya Afya kutoka ubalozi wa Uingereza DKt. Gloria Ngaiza (wapili Kushoto) akimtafasiria Waziri wa Maendeleo kutoka nchi ya Uingereza Mhe. Penny Mordaunt kilichokuwa kikisemwa na Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Tabata (Wakwanza Kushoto).Wa mwisho Kulia ni Waziri wa Áfya Mhe. Ummy Mwalimu.
IDADI YA WANAWAKE WANAOTUMIA HUDUMA ZA ZA UZAZI WA MPANGO ZAONGEZEKA NCHINI 

Na WAMJW - DSM

SERIKALI kupitia Wizara ya Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto imesema kuwa idadi ya wanawake wanaotumia huduma za Afya za Kisasa za uzazi wa mpango zimeongezeka nchini mpaka kufikia Asilimia 32.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo wakati alipoupokea ugeni  wa Waziri wa Maendeleo kutoka nchini Uingereza katika Zahanati ya Tabata jijini Dar es salaam ukiwa na lengo la kutatua changamoto za Sekta ya Áfya hususani katika huduma za Afya ya mama na mtoto.

"Kupitia Msaada wao tumeweza kuongeza idadi ya wanawake wanaotumia huduma za Kisasa za uzazi wa mpango, hatupo vizuri,  tupo Asilimia 32, tumeweka lengo itapofika 2020 tufikie Asilimia 45 ya wanawake walioolewa wanatumia njia hizi" Alisema Waziri Ummy Mwalimu. 

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa, bado kuna changamoto ya vifo vitokanavyo na uzazi nchini, takribani wanawake 556,000 katika kila vizazi hai laki moja wanafariki na kwa mujibu wa Wataalam uzazi wa mpango utaweza kuchangia Mpaka Asilimia 30 katika Kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. 

Pia Waziri Ummy alisema kuwa Serikali ya Tanzania imechukua hatua kwa kutenga fedha za ndani katika kupambana na changamoto za sekta ya Áfya ikiwemo kuajiri watumishi wa sekta ya Áfya jambo linalosaidia Kupunguza changamoto hizo za vifo vya akina mama wajawazito na mtoto wachanga. 

"Sisi kama Serikali tumejiongeza, tumechukua hatua na kutenga rasilimali fedha za ndani ikiwemo kuajili watoa huduma za afya, kuhakikisha Kwamba tunatatua changoamoto hiyo " alisema Waziri Ummy.

Hata hivyo Waziri Ummy aliishukuru Serikali ya Uingereza kupitia kwa Waziri wa Maendeleo Mhe. Penny Mordaunt kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma za afya hasa katika huduma za mama na mtoto. 

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo kutoka Uingereza Mhe. Penny Mordaunt ameshukuru Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Áfya kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhudumia wananchi wa Tanzania na kuahidi kupeleka salamu za Tanzania nchini Uingereza.

Jumanne, 7 Agosti 2018

WIZARA YA AFYA YATENGA BILIONI 14 KWA AJILI YA HUDUMA UZAZI WA MPANGO

- Hakuna maoni
Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (MB) akisisitiza jambo katika Mkutano uliowakutanisha viongozi na watendaji wakuu wa Halmashauri na Wilaya kutoka Mkoa wa Tanga wenye lengo la kuendeleza juhudi za Serikali juu ya masuala Ya uzazi wa mpango,  chini ya JhPiego unaofadhiliwa na Melinda Gate.

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe ambae alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kisa Kasongwe akitoa neno umbele ya viongozi na watendaji wakuu wa Halmashauri na Wilaya baada ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Áfya Mhe Ummy Mwalimu.

Mganga mkuu wa Mkoa wa Tanga DKt. Asha Mahita akielezea hali ya huduma za uzazi wa mpango Mkoani Tanga katika Mkutano wa wenye lengo la kuendeleza juhudi za Serikali juu ya Uzazi wa mpango nchini.

 Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la JHPIEGO  Dkt. Dustan Bishanga

Viongozi wa Halmashauri na Wilaya kutoka Tanga leo waliohudhuria kikao chenye lengo la kuendeleza juhudi za Serikali juu ya uzazi wa mpango.

Picha ya pamoja ikiongonzwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akiwa na viongozi wa Halmashauri na Wilaya ya Tanga baada ya Mkutano wenye lengo la kuendeleza juhudi za Serikali juu ya masuala Ya uzazi wa mpango ulio chini ya JhPiego unaofadhiliwa na Melinda Gate.


WIZARA YA AFYA YATENGA BILIONI 14 KWA AJILI YA HUDUMA   UZAZI WA MPANGO

Na.WAMJW-Tanga
 
Viongozi na watendaji wakuu wa halmashauri ya Jiji la Tanga wametakiwa kuwa wabunifu katika kuhakikisha wanawafikia wanawake wengi wanaoishi mjini ili waweze kujiunga na huduma za uzazi wa mpango.
 
Wito huo umetolewa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akifungua mkutano uliowakutanisha Viongozi na watendaji wakuu wa Halmashauri ya Jiji,Wilaya ya Tanga Mjini pamoja na Wilaya ya korogwe wenye lengo la kuendeleza juhudi za uzazi wa mpango nchini.
 
Waziri Ummy alisema kwamba Serikali ya awamu ya tano imejipanga kutokomeza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga  hivyo imejipanga kuwafikia wananchi wengi ili kuweza kupunguza kwa asilimia 30 vifo vitokanavyo na uzazi.
 
“lazima muonyeshe utayari na umakini kama viongozi katika kuwekeza kwenye uzazi wa mpango, mkiwa wabunifu mtawawezesha kuwafikia akina mama wengi wa mjini, hata akina baba kwa kuwapa elimu ya kutosha na kufanya maamuzi ili wapange lini wanataka kuzaa,watoto wangapi na watofautiane kwa miaka mingapi”.Alisema Waziri Ummy.
 
Aidha, aliwataka viongozi kutumia fedha hizo kuziweka kwenye vitu endelevu ili mradi huo uongeze wanawake wengi kutumia njia za uzazi nchini.
 
“Msiweke mipango ya mardi huu kwenye semina bali mradi huu uwe njia ya kufungua miradi mingine kutoka kwa wadau wa maendeleo” alisema Waziri Ummy.
 
Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa Serikali kupitia Wizara ya afya kwa mwaka huu wa fedha 2018/2019 umetenga shilingi bilioni 14 kwa ajili ya afya ya uzazi wa mama na mtoto tofauti na miaka ya nyuma ambapo kabla Serikali ya awamu ya tano haijaingia madarakani wizara ilikua ikitenga shilingi bilioni 2 kwa ajili ya matumizi kitengo hicho.
 
Naye Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Bi.Kisa Kasongwe ambaye alimuakilisha Mkuu wa Mkoa wa Jiji la Tanga alisema halmashauri ya Jiji la Tanga ipo tayari kutoa ushirikiano na shirika hilo kwani mradi huo utaleta hali nzuri kwa akina mama pamoja na watoto wachanga.
 
Wakati huo huo Kaimu Mwakilishi Mkazi wa shirika la jhpiego Dkt.Dustan Bishanga alisema kuwa mradi huo unakuja kuongeza rasiliamali ambazo hazitoshi katika kusimamia  na kutekeleza katika uwekezaji wa uzazi wa mpango.
 
“Mradi huu utafanikiwa endapo viongozi  wa Jiji la Tanga  mtatekeleza  na kufanya mpango huu kufanikiwa hivyo mtapelekea tuwaletee mradi mwingine wa afya ya uzazi kwa vijana endapo mradi huu wa kwanza mtaufanikisha ipasavyo”.Alisema Dkt.Bishanga.
 
Mradi wa “Tupange pamoja” ulianzishwa mwaka 2016 na kutekelezwa na halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Arusha ambapo kwa jiji la Dar es Salaam walipatiwa shilingi milioni 250 kwa ajili ya kutekeleza uzazi wa mpango kwa halmashauri zote na hivi sasa unaanza kwa Jiji la Tanga.
 
Idadi ya akina mama wanaotumia uzazi wa mpango kwa Jiji la Tanga ni asilimia 31 ambapo kitaifa inatakiwa kufikia asilimia 45 hadi mwaka 2020 na vifo vya akina mama kwa halmashauri hii imepungua kutoka vifo 69 mwaka 2014 hadi vifo 45 kwa mwaka 2017.



JAMII YA TANZANIA INATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA ILI KUEPUKA KIPINDUPINDU.

- Hakuna maoni
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na Wadau mbalimbali wa sekta ya Afya hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa kikao cha kujadili mikakati ya kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu nchini kilichofanyika leo jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora akiongea na Wadau mbalimbali wa sekta ya Afya hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa kikao cha kujadili mikakati ya kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu nchini kilichofanyika leo jijini Dodoma.

Afisa wa kudhibiti na kukinga magonjwa kutoka Shirika la Afya Duniani WHO nchini Tanzania Dkt. Grace Saguti akiongea mbele ya wadau mbalimbali wa Sekta ya afya wakati wa kikao cha kujadili mikakati ya kupambana na kipindupindu kilichofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi wa kwanza  akifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa mwezeshaji hayupo pichani wakati wa kikao cha kujadili mikakati ya kupambana na kipindupindu kilichofanyika jijini Dodoma.


Wadau mbalimbali wa sekta ya afya wakimsikiliza  kwa makini Katibu Mkuu Wizara ya Afya  Dkt. Mpoki Ulisubisya hayupo pichani wakati wa kikao cha kujadili mikakati ya kupambana na kipindupindu kilichofanyika jijini Dodoma.


NA WAMJW-DODOMA


SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesisitiza jamii ya Tanzania juu ya utumiaji wa maji safi na salama ili kuweza kupambana na ugonjwa wa kipindupindu kwa urahisi.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara ya Afya) Dkt.  Mpoki Ulisubisya wakati wa ufunguzi wa kikao cha siku tatu cha kujadili mikakati ya kukabiliana na ugonjwa kipindupindu nchini kinachoendelea jijini Dodoma.

"Ili kupambana na ugonjwa huu Watanzania  wanatakiwa kutunza mazingira hasa kutumia vyoo bora pamoja na kutumia maji safi na salama katika jamii inayotuzunguka" alisema Dkt. Ulisubisya.

Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa hadi sasa kwa takwimu iliyopo inaonesha kuwa watu elfu 32 wameugua na watu 600 wamepoteza maisha kutokana na kipindupindu hapa nchini.

Dkt. Ulisubisya amesema kuwa ili kuweza kutokomeza ugonjwa huo mpaka kufikia 2030 wadau mbalimbali ikiwemo Wizara ya maji, TAMISEMI,  na wadau wengine wa afya wanatakiwa kushirikiana na Wizara ya Afya pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO) katika kuweka mikakati ya kupambana na ugonjwa wa kipindupindu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora amesema kuwa Serikali itaendelea kuwaweka pamoja wataalam mbalimbali kwa ajili ya kuzuia ugonjwa wa kipindupindu nchini Tanzania.

Aidha Prof. Kamuzora amesema kuwa tayari wameshaandaa madawati mbalimbali ya wataalamu katika ofisi yake ili kuwexa kuweka mifumo ya  kushughulikia kwa uharaka magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu.

Naye Afisa wa kudhibiti na kukinga Magonjwa kutoka Shirika la Afya Duniani hapa  nchini Dkt. Grace Saguti amesema kuwa kutokana na ushirikiano wa wadau mbalimbali Serikali ya Tanzania imeweza kufanikiwa  kutokomeza ugonjwa wa Kipindupindu kwa sehemu kubwa ya Tanzania.

 "Mpaka hivi sasa mikoa inayokabiliwa na ugonjwa wa kipindupindu  katika maeneo yake ni Rukwa, Songwe na Arusha lakini maeneo yote yaliyobaki tumefanikiwa kutokomeza ugonjwa huo" alisema Dkt. Saguti.


Jumatatu, 6 Agosti 2018

SERIKALI YATARAJIA KUDAHILI WANAFUNZI 380 WA KADA ZA AFYA.

- Hakuna maoni
Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (MB) akisisitiza jambo mbele ya watumishi wa Serikali na wanafunzi wa Kada ya uuguzi leo wakati wa hafla ya makabidhiano ya Majengo ya chuo cha uuguzi Tanga.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela akiwasamia wanafunzi wa Kada ya uuguzi wakati alipomkaribisha mgeni rasmi, Waziri wa Áfya Mhe. Ummy Mwalimu katika hafla ya makabidhiano ya Majengo ya chuo cha uuguzi Tanga.

 Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa chuo cha uuguzi Tanga  Felister Bulali  akitoa maelekezo ya namna ya kumuudumia Mtoto aliyetoka kuzaliwa , mbele ya Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wapili Kushoto),  Wakwanza ni mkuu wa chuo hicho Bi. Leah Makala na watatu ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe Martine Shigela.

Waziri wa Áfya Mhe Ummy Mwalimu akiteta jambo juu ya kifaa cha kujifunzia chenye umbo la Mtoto,  wakati wa hafla ya makabidhiano ya Majengo ya chuo cha uuguzi Tanga. Wakwanza ni mkuu wa chuo hicho Bi Leah Makala.

Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akisakata ngoma na kikundi cha ngoma cha kinamama leo wakati wa hafla ya makabidhiano ya Majengo ya chuo cha uuguzi Tanga

Bweni la ghorofa nne la wanafunzi lenye uwezo wakulaza wanafunzi 380 kwa wakati mmoja likiwa ni baadhi ya majengo yaliyogharimu kiasi cha shilingi Bilion 3.5.

Picha ya pamoja ikiongonzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martine Shigela wakiwa na baadhi ya watumishi wa Serikali wakati wa Hafla ya makabidhiano ya Majengo ya chuo cha uuguzi Tanga.


SERIKALI YATARAJIA KUDAHILI WANAFUNZI 380 WA KADA ZA AFYA KATIKA CHUO CHA UUGUZI TANGA.

Na WAMJW - TANGA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, inatarajia kufanya udahili wa wanafunzi kwa asilimia 100 kutoka wanafunzi Mia moja na Hamsini (150) hadi Mia tatu themanini wa kada za Afya nchini katika chuo cha Uuguzi Bombo Tanga.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) wakati wa hafla ya makabidhiano ya majengo ya chuo cha Uuguzi Tanga, yaliyojengwa kupitia ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kupambana na UKIMWI, KIFUA KIKUU (TB) na MALARIA (Global fund).

Waziri ummy aliendelea kusema kuwa  majengo yaliyokabidhiwa ni juhudi za Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo katika kuhakikisha wanazalisha wataalamu wa kada za Afya, hususani Wauguzi na Wakunga jambo litalowawezesha kuwa Wataalamu bora.

“Udahili wa wanafunzi umeongezeka kutoka 190 hadi 260, Huwa tunapata shida sana, wanafunzi wengi wanafaulu na tunakuwa hatuna nafasi ya wapi  pakuwapeleka, kwahiyo tunawashukuru Global fund , tunaweza kudahili hadi wanafunzi 368” Alisema Waziri Ummy Mwalimu.

Aidha, amemwagiza Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali watu  kutoka Wizara ya Afya kushirikiana na NACTE  kuwachukua wanafunzi wote waliosoma na kufaulu vizuri masomo nya Sayansi na wenye vigezo na wenye vigezo katika kada ya Afya.

Waziri Ummy aliongeza kuwa, kutokana na jitihada hizo kumekuwepo na ongezeko la wahitimu ngazi ya astashahada na Stashahada kwa mafunzo kutoka wahitimu 4473 mwaka 2012/2013 hadi 7561 kwa mwaka 2016/2017 , ongezeko hili ni sawa na Asilimia 69.

Wakati huo huo Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Otilia Gowelle amesema kwa mwaka huu wa fedha , Wizara imetenga shilingi Bilion 8 kwaajili ya ukarabati wa majengo chakavu katika chuo hicho.

Aliendelea kuwa Wakufunzi 143 wamepangiwa kufanya kazi katika vyuo vya Afya nchini, vikiwemo vyuo vya Wauguzi na Wakunga ambao ndio msingi wa kupunguza athari ya uzazi pamoja na vifo vya wakina mama wajawazito wakati wa kujifungua.

Nae Mwakilishi wa Global Fund Dkt. Hiltruda Temba amesema kuwa, Global fund  imeboresha miundombinu yakufundishia katika vyuo 14 na kuwezesha kufadhili zaidi ya wanafunzi 1500 wa kada za Uuguzi na Ukunga wa Technolojia dawa, Technolojia maabara na Tabibu katika kipindi cha Mwaka 2015/2016 hadi 2017/2018, pamoja na kutenga shilingi Billion 1.1 kwaajili yakuboresha mifumo ya Afya.

MWISHO.