Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 31 Julai 2019

SERIKALI YANUNUA MAGARI 12 YA HUDUMA YA DHARURA NA UOKOZI

- Hakuna maoni
Mkuu wa kitengo cha afya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl.Julius Nyerere George Ndaki akimuonesha ufanyaji kazi wa  mashine za kupima joto(thermo scanner) Naibu Waziri Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati alipotembelea eneo la wasafiri wanaoenda nje ya nchi  zilizofungwa kwenye uwanja mpya wa ndege terminal three

Naibu Waziri Dkt.Faustine Ndugulile akionesha kadi za homa ya manjano"Yelow Fever" ambazo zinatolewa na wizara ambapo wizara imefunga kifaa maalum cha kubaini kadi feki ambazo wasafiri huzinunua bila kuchanjwa chanjo hiyo

Dkt.Ndugulile akioneshwa utofauti wa kadi halisi na kadi feki za homa ya manjano.Dkt.Ndugulile amewasihi wananchi wanaotarajia kusafiri nje ya nchi kuacha kununua kadi feki bali kuhakikisha wanapata chanjo hiyo kwenye vituo rasmi vilivyoelekezwa na wizara  ya Afya

Naibu Waziri akikagua vifaa vingine vilivyofungwa terminal three kwa ajili ya kubaini wahisiwa wa Ebola

Katika kuelekea Mkutano wa Kimataifa wa SADC wizara ya afya imejipanga kukabiliana na dharura kwa wageni watakaoshiriki mkutano huo.Pichani.Dkt.Ndugulile akikagua magari ya wagonjwa wa dharura yaliyopo ofisi za Toyota

 Naibu Waziri akikagua kifaa cha huduma ya dharura kilichopo kwenye magari hayo

Naibu Waziri akikagua moja ya chumba cha dharura kilichoandaliwa kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya washiriki wa mkutano wa SADC

Mkuu wa Kitengo cha Dharura Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt.Juma Mfinanga (kulia)akimueleza jambo Naibu Waziri wakati alipotembelea kujionea hali ya utayari ya kuwahudumia washiriki wa mkutano wa SADC ambao watapata dharura na hivyo kupatiwa huduma za afya kwenye hospitali hiyo



SERIKALI YANUNUA MAGARI 12 YA HUDUMA YA DHARURA NA UOKOZI

NA.Catherine Sungura,WAMJW-DSM

Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imenunua magari kumi na mbili kwa ajili ya huduma za dharura nchini.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa wizara hiyo Dkt.Faustine Ndugulile wakati alipofanya ukaguzi kwenye ofisi za Toyota jijini hapa.

Dkt.Ndugulile amesema magari hayo yameletwa muda muafa ikiwa  zimesalia siku chache kuanza mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo magari hayo pamoja na mabasi mawili ya uokozi yatatumika kutoa huduma za kiafya kwenye mkutano huo na baada ya hapo yatagaiwa kwenye maeneo yaliyoanishwa kwa uokoaji wa majeruhi wa ajali.

"Magari na Mabasi hayo yatatumika kwenye mkutano wa SADC na baadae yatasambazwa katika vituo vya dharura nje ya hospitali ambapo yatatumika kusafirishia majeruhi pindi ajali inapokuwa imetoka.

"Tutayatumia katika mkutano wa SADC, pamoja na ambulance hizo 12 kuna mabasi makubwa mawili ambayo yana huduma zote za msingi ndani ambapo watu wapatao 20 wanaweza kubebwa na kupatiwa msaada wa ajali," alisema.

Alisema serikali imejipanga  pia katika njia ya anga kwa kutumia  ndege  pindi mtu anapohitaji huduma ya dharura kupelekwa haraka katika eneo jingine hususani hospitali ya Taifa Muhimbili.

"Ni utaratibu ambao Serikali inauweka kuhakikisha waathirika wa ajali wanapata huduma za dharura na ajali, mapema iwezekano na tunasema ndani ya masaa yaliyowekwa ya kuwahudumia majeruhi," alisema Dkt.Ndugulile

Naibu Waziri huyo alisema wameagiza magari ya zimamoto na uokozi kwamba si tu liwe na uwezo wa kuzima moto bali linakuwa na vifaa vya kisasa, kwa mfano ikiwa gari limepata ajali, milango inashindwa kufunguka, iweze kukatwa ili kuokoa majeruhi, iwezekane.

"Haya ni maendeleo makubwa kwa Serikali katika kuhakikisha majeruhi wanapata huduma za dharura za awali mapema inavyowezekana, kwani wengi hufariki dunia kwa sababu hukosa zile huduma za awali za dharura katika lile li-saa limoja la kwanza," alisema.

Dk. Ndugulile aliongeza "Inawezekana anavuja damu, anashindwa kupumua vizuri, tuna imani magari, mabasi na mafunzo tuliyowapa wataalamu huduma hizi zitaimarika.

"Natoa rai kwa wananchi, kwani nao wamekuwa wakichangia madhara kwa majeruhi, wanawamalizia wale majeruhi, wakiamini wanawasaidia kuokoa maisha.

"Wahakikishe tu wanamtoa majeruhi na kumuweka pahala pengine mbali na tukio la ajali, kama gari litaweza kulipuka moto ule usimfikie, tunapowabeba 'mzobe mzobe' tunawasababishia madhara zaidi.

"Muhimu tuhakikishe huduma za msingi zinapatikana pale pale, kikubwa ni kuhakikisha yule Mgonjwa anapumua, havuji Damu kwa wingi na njia yake ya Hewa IPO salama.

"Jambo la msingi si kumkimbiza majeruhi hospitalini kwanza bali 'kum-stablize' pale pale eneo la tukio, kama mfupa umevunjika afunge vizuri usining'ingine, abebwe vizuri kama mshipa wa shingo umevunjika usimalizike, kwani wengi kutokana na ule ubebaji huishia kupooza mwili na hata kufa," alisema.

Sambamba na hilo, mapema asubuhi, Dk. Ndugulile alifanya ziara kwenye kitengo cha afya ndani ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA- terminal III), kujionea hali ya utayari wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Ebola.

MWISHO

WATOA HUDUMA ZA AFYA WATAKIWA KUDHIBITI UGONJWA WA EBOLA USIINGIE NCHINI

- Hakuna maoni
Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Prof. Faustin Kamuzora akisema jambo wakati akifungua zoezi la utayari wa kukabiliana na Ugonjwa wa Ebola kwa Watoa huduma za afya katika Mkoa wa Kigoma (hawapo pichani) jana Mjini Bukoba.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiru Taratibu akisema jambo wakati wa ufunguzi wa zoezi la utayari wa kukabiliana ana Ugonjwa wa Ebola kwa watoa huduma za afya Mkoani Kagera (hawapo pichani) jana Mjini Bukoba.

Washiriki wa zoezi la utayari wa kukabiliana na tishio la Ugonjwa wa Ebola kutoka Mkoa wa Kagera wakiwa kwenye majadiliano kuweka mikakati ya ugonjwa huo usiingie nchini.

Wataalam wa Afya katika Mkoa wa Kagera wakiwa katika zoezi la utayari wanajadiliana mikakati ya kudhibiti Ugonjwa wa Ebola usiingie nchini.

Mwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani Dkt. Refeya Ndyamuba (aliyesamama) akisema jambo wakati wa ufunguzi wa zoezi la utayari wa kukabiliana na Ugonjwa wa Ebola nchini kwa watoa huduma za afya katika Mkoa wa Kigoma jana Mjini Bukoba.


Picha ya Pamoja washiriki wa zoezi la utayari wa kukabiliana na Ugonjwa wa Ebola na Mgeni Rasmi, Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Prof. Faustin Kamuzora (aliyeketi katikati).


Na WAMJW – Bukoba, KAGERA

Watoa huduma za afya nchini wametakiwa kuweka juhudi madhubuti kuhakikisha Ugonjwa wa Ebola hauingii nchini Tanzania.

Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Prof. Faustinely Kamuzora alipokuwa akifungua zoezi la utayari jinsi ya kukabiliana na ugonjwa wa ebola kwa wataalam wa afya mkoani humo.

Akifungua zoezi la utayari, Profesa Kamuzora amesema “Tukifanya juhudi zetu za kukabiliana na ugonjwa wa ebola basi maisha yetu hayatokuwa hatarini” na kuendelea “Juhudi hizi zina matunda makubwa kuliko tukaruhusu ugonjwa huo kuingia nchini”

“Mpaka sasa hivi Mwenyezi Mungu ametujaalia hakuna mtu aliyeripotiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola nchini, tukifanya yale ambayo tunaelekezwa na wataalam wetu basi maisha yetu hayatokuwa hatarini” amesema Profesa Kamuzora.

Prof Kamuzola amewataka watoa huduma za afya kufuata taratibu zote zilizowekwa ili endapo ikitokea mtu akabainika kuwa na ugonjwa huo, basi aweze kupatiwa huduma na wakati huo huo mtoa huduma akawa salama.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiru Taratibu amesema kuwa zoezi ya utayari lina lengo la kuzuia maafa yasitokee kwa kuwaweka tayari watalaam wa sekta ya afya kukabiliana na tishio la ugonjwa wa ebola kuingia nchini.

“Tuhakikishe tunazuia ugonjwa wa ebola usiingie nchini, na endapo ikitokea umeingia basi tuhakikishe tunapunguza athari zitokanazo na ugonjwa huo” amesema Bw. Taratibu.

Naye Mtaalam wa Afya ya Jamii na Masuala ya Dharura na Maafa kutoka Wizara ya Afya Dkt. Faraja Msemwa amesema kuwa kupitia mazoezi hayo ya utayari wanapata fursa ya kubaini fursa  na changamoto zilizopo katika kudhibiti ugonjwa huo wa ebola usiingie nchini.
“Katika zoezi hili tunaangalia hawa watumishi wetu wa afya tuliowandaa wana uwezo wa kiasi cha kuweza kufuata miongozo iliyoandaliwa” amesema Dkt. Msemwa.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) toka kuripitiwa kuibuka kwa ugonjwa wa ebola nchini Uganda mnamo mwezi Agosti mwaka 2018 jumla ya kesi 2612 za watu kuathiriwa na ugonjwa huo zimeripotiwa huku ukisababisha vifo 1756 (sawa na asilimia 67). Zoezi la utayari limepangwa kufanyika kuanzia leo JULAI 30 mpaka AGOSTI 8 mwaka 2019 ambapo vituo vya kutolea huduma za afya katika Mikoa ya Kagera na Kigoma vitapimwa utayari wao katika kukabiliana na Ugonjwa huo hatari.

Kupitia mazoezi ya utayari, watoa huduma za afya kuanzia ngazi ya jamii wanapata fursa ya kushiriki kwa vitendo namna ya kutambua, kutoa huduma kwa mtu anayehisiwa au kuwa na ugonjwa wa ebola na kuwaondolea woga pindi ikitokea mtu akabainika kuwa na ugonjwa huo.

MWISHO.

Jumapili, 28 Julai 2019

4% YA WANANCHI WAAMBUKIZWA VIRUSI VYA HOMA YA INI

- Hakuna maoni
Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika akitembelea moja ya banda la kufanyia uchunguzi  wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo  katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma, kushoto  kwake ni Mkurugenzi wa Epidemiolojia kutoka Wizara ya Afya Dkt. Janneth Mghamba.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika akiwajulia hali baadhi ya watu waliojitokeza kufanya  uchunguzi homa ya ini, katika  maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo  katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma, Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Epidemiolojia kutoka Wizara ya Afya Dkt. Janneth Mghamba.

Wadau mbali mbali wa Afya wakifuatilia kwa makini taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo  katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika akiteta jambo na mwakilishi wa WHO Dkt. Christine Chakanyuka Musanhu  wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo  katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika akisisitiza jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo  katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma, kushoto ni Mkurugenzi wa Epidemiolojia kutoka Wizara ya Afya Dkt. Janneth Mghamba, na Kulia ni mwakilishi wa WHO anaitwa Dr. Christine Chakanyuka Musanhu

Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika katika picha ya pamoja na Wadau pamoja na Watumishi wa Sekta ya Afya, wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo  katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.


4% YA WANANCHI WAAMBUKIZWA VIRUSI VYA HOMA YA INI

Na WAMJW-DOM

Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa Dkt. Alphonce Chandika amesema kuwa miongoni mwa Watanzania wenye umri kati ya miaka 15-49 wameabukizwa Virusi vya Homa ya Ini aina ya B, hii ni kutokana na Takwimu za Ofisi ya Taifa wa Takwimu 206-2017.

Dkt. Alphonce Chandika amesema hayo leo wakati wa Siku ya Homa ya Ini Duniani ambayo, yenye kauli mbiu ya “Wekeza katika mapambano ya Homa ya Ini “ maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika Jijini Dodoma katika Hospitali ya Benjamini Mkapa.

“kati ya wachangiaji damu 307,835 takribani watu 13,613 sawa na asilimia 4.4 walikuwa na maambukizi ya homa ya ini kwa mujibu wa takwimu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS)” alisema Dkt. Alphonce Chandika.

Dkt. Alphonce Chandika  aliendelea kusema kuwa Mwaka 2017, kati ya wachangiaji damu 233,953 takribani watu 11,417 sawa na asilimia 4.9 walikuwa na maambukizi, aidha asilimia 0.5 ya wachangiaji damu walikuwa na maambukizi ya homa ya ini aina ya C kwa mwaka 2017 na asilimia 0.3 kwa mwaka 2018.

Aidha, Dkt. Alphonce Chandika alisisitiza juu ya kutoa elimu ya kutosha kwa Wananchi juu ya athari za ugonjwa wa  Homa ya Ini katika jamii na kwa nchi kwa ujumla, huku akisisitiza kuwa Serikali itaokoa kiasi kikubwa  cha fedha kama  itawekeza nguvu kwenye kinga, ambacho kinachotumika kwenye matibabu dhidi ya ugonjwa huu wa homa ya ini.

Nae, Mkurugenzi msaidizi wa Epidemiolojia kutoka Wizara ya Afya Dkt. Janneth Mghamba amesema kuwa huduma  hii ya chanjo ya homa ya Ini imeanza kutolewa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa za Sokoture Mwanza,Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi Kilimanjaro, Hospitali ya Rufaa ya Geita, Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Hospitali ya Temeke, Hospitali ya Mwananyamala, Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, Hospitali ya Rufaa ya Iringa, Hospitali ya Muimbili, Moi, Ocean Road  na vituo vyote vya mipakani.

Mwisho.

Jumamosi, 27 Julai 2019

MKAKATI WA KUZUIA MBU NA WADUDU DHURIFU NCHINI WAZINDULIWA LEO

- Hakuna maoni

Picha ya Juu ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Picha ya Chini ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo wakizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa wa Kitaifa wa Upuliziaji wa dawa za kuua wadudu dhurifu wakiwemo Mbu ili kupunguza Magonjwa ya Malaria na Dengue pamoja na magonjwa Mengine. Uzinduzi huu umefanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar Es Salaam.


Baadhi wa Mabwana Afya kutoka Manispaa mbalimbali za jiji la Dar Es Salaam wakipita mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu kumuonesha zana zinazotumika katika kupuliza dawa za kuangamiza wadudu dhurifu katika hafla ya uzinduzi wa mkakati wa kupuliza dawa ili kutokomeza wadudu dhurifu.
Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa wa Kitaifa wa Upuliziaji wa dawa za kuua wadudu dhurifu wakiwemo Mbu ili kupunguza Magonjwa ya Malaria na Dengue pamoja na magonjwa Mengine.

Baadhi ya mashine za kupulizia dawa za kuua mbu na wadudu dhurifu kwa binadamu zikiwa katika magari tayari kwa ajili ya ufunguzi wa mkakati wa taifa wa kudhibiti wadudu dhurifu. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu mapema leo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) akizindua rasmi mkakati wa upuliziaji dawa kwa ajili ya kutokomeza wadudu dhurifu ikiwemo mbu. Wa pili kulia ni Waziri wa TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) akiwa na Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo (katikati) mapema leo wakizindua mashine za kupuliza dawa ya kuua mbu na wadudu dhurifu zitakazosambazwa badae kwenye baadhi ya mikoa ikiwemo Tanga na Dar Es Salaam.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo Jafo wakijaribu moja ya mashine za FOG maalumu kwa ajili ya upuliziaji wa dawa za kuua wadudu wadhurifu katika maeneo mbalimbali nchini.

Katibu tawala wa mkoa wa Dar Es Salaam Bw. Abubakar Kinenge (kushoto) akikabidhiwa moja ya mashine za kupuliza dawa za kuua wadudu dharifu na Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo (Kulia) wakati wa  uzinduzi wa kitaifa wa mkakati wa kupuliza dawa za kuua wadudu dhurifu wakiwemo mbu na wengineo nchi nzima.

Picha ya Pamoja kati ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa OR-TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo wakiwa na Wakurugenzi na viongozi mbalimbali toka Wizara ya Afya na Serikali ya Mkoa wa Dar Es Salaam wakati wa uzinduzi wa mkakati wa taifa wa kutokomeza wadudu dhurifu uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar Es Salaam.
Na.WAMJW-DSM

Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi mahiri wa Mhe. Dkt.John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewekeza vya kutosha katika kudhibiti mbu anayesababisha  malaria hali ambayo imepelekea kupungua  kwa kiwango cha ugonjwa wa Malaria nchini.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akizindua mkakati wa Taifa wa kudhibiti mbu na wadudu wadhurifu jijini hapa.

“Kiwango cha Malaria nchini kimepungua  kutoka asilimia 18.1 mwaka 2008 hadi asilimia 7.3 ya sasa. Hatahivyo, juhudi zinahitajika zaidi kutokomeza ugonjwa huu".Alisema Waziri Ummy Mwalimu

Aidha, alisema takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadiria kuwa asilimia 17 ya magonjwa ya kuambukiza husambazwa na wadudu na kusababisha zaidi ya vifo millioni  moja kila mwaka." Kwa mfano, malaria peke yake inakadiriwa kusababisha vifo 400,000 kila mwaka na wengi wanaofariki ni watoto chini ya miaka 5"Aliongeza Waziri Ummy Mwalimu

Kwa upande wa ugonjwa wa homa ya Dengue Waziri huyo alisema   Mwaka huu ugonjwa wa Dengue umethibitishwa kuwepo hapa nchini hususani katika jiji la Dar es Salaam,Tanga na mikoa mingine. Kuanzia  Januari 2019 hadi kufikia tarehe 21 Julai 2019 jumla ya wagonjwa waliothibitishwa kuwa na homa ya dengue hapa nchini ni 6588 na vifo 6 .

Alitaja mikoa hiyo ni Mkoa wa Dar es Salaam umeongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi ( 6,170 na vifo 4), Tanga (316 na kifo kimoja), Pwani ( 57), Morogoro (22), Lindi (8), Arusha (5), Dodoma (3 na kifo kimoja), Kagera (2), Singida (2),Ruvuma (2) na Kilimanjaro.

Hata hivyo Waziri Ummy alisema kutokana na kuendelea kujitokeza kwa magonjwa yaenezwayo na wadudu na,kusababisha madhara kwenye jamii,wizara yake imeandaa mkakati huo wa kudhibiti mbu na wadudu wengine wadhurifu wa mwaka 2019-2024 ikiwa na lengo la kuhakikisha wanadhibiti mbu na wadudu wengine wadhurifu kwa njia ya utengamano na kuhakikisha jamii inashiriki kikamilifu.

Katika kuimarisha udhibiti huo wizara imeagiza zenye uwezo mkubwa wa kupulizia zipatazo 8 na zinapelekwa katika mkoa wa Dar es Salaam,Tanga na Dodoma.

Kwa upande wake Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo amemshukuru Waziri Ummy kwa kuzindua mkakati huo huku akionesha nia ya dhati ya kuendeleza mkakati huo katika Mikoa yote nchini huku akiwataka Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuhakikisha wanatenga bajeti ya kununua mashine ili kuweza kufikia malengo ya kutokomeza kabisa Malaria, Dengue na magonjwa mengine yanayosababishwa na wadudu dhurifu.

MWISHO

Ijumaa, 26 Julai 2019

KAMBI YA UPASUAJI NA MATIBABU YA MOYO YAZINDULIWA TAASISI YA JAKAYA KIKWETE

- Hakuna maoni

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akipokea zawadi kutoka kwa mgeni wake Naibu Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Watu wa China wakati walipozindua Kambi ya matibabu na upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Jakaya Kikwete Jijini Dar Es Salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa na Naibu Waziri wa Afya wa China Bw. Li Bin (waliosimama) wakishuhudia kusainiwa kwa makubaliano ya kambi ya upasuaji na matibabu ya moyo katika Taasisi ya Jakaya Kikwete yatayoratibiwa kwa ushirikiano wa madaktari wa JKCI na wa jimbo la Shadong nchini China. Kushoto anayesaini ni Prof. Mohamed Janabi na kulia ni mwakilishi kutoka Shadong.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea katika uzinduzi wa kambi ya matibabu na upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Jakaya Kikwete Jijini Dar Es Salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Kulia) akiwa na Naibu Waziri wa Afya wa China Bw. Li Bin wakifuatilia maelezo ya daktari (hayupo pichani) wakati walipotembelea chumba cha uangalizi maalumu kwa wagonjwa wa moyo kilichopo taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar Es Salaam.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akisalimiwa na mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete wakati alipotembelea baadhi ya wodi ili kuona hali ya huduma za matibabu zinazotolewa kwenye taasisi hiyo kabla ya uzinduzi wa kambi ya matibabu na upasuaji wa moyo mapema leo.

Picha ya Pamoja ya Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, Naibu Waziri wa Afya wa China Bw. Li Bin, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi, Mwenyekiti wa Bodi ya JKCI Prof. William Mahalu wakiwa na Wataalamu wa upasuaji na matibabu ya moyo kutoka jimbo la Shadong la nchini China.

Na WAMJW-DSM

Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Jamhuri ya watu wa China imezindua kambi ya huduma za hali ya juu za upasuaji na matibabu ya moyo kwa wananchi wenye matatizo hayo.

Kambi hiyo imezinduliwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kwa kushirikiana na Naibu Waziri wa Afya wa Jamhuri ya watu wa China Bw. Li Bin ili kutoa huduma za matibabu ya moyo pamoja na upasuaji lengo likiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa rufaa za wagonjwa kwenda nje ya nchi kufuata huduma hizi.

“Kupitia kambi hii  Watanzania watapata huduma za hali ya juu za upasuaji na matibabu ya moyo, itatusaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa rufaa za wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya huduma hizi, pia kambi itatoa mafunzo ya juu katika ujuzi wa kisasa kwenye upasuaji na Tiba ya moyo kwa wataalamu wetu kwa kushirikiana na madaktari kutoka jimbo la Shadong”. Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema tatizo la magonjwa yasiyoambukizwa Tanzania na duniani kote limeongezeka kwa kasi ambapo takwimu za sasa kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) inaonesha ukubwa wa tatizo hili kuwa takribani watu Milioni 17 hupoteza maisha kila mwaka ikiwa ni sawa na asilimia 60 ya vifo vyote huku akiongeza kuwa vifo hivyo asilimia kubwa vinatokea katika nchi zinazoendelea kama Tanzania.

Aidha, Waziri Ummy ameongeza kuwa sababu kuu ya maradhi ya moyo nchini kama zilivyo nchi nyingine za kiafrika ni homa ya Rumatiki (Rheumatic Fever). Hivyo inakisiwa kuna watoto kuanzia umri wa mwaka 1-15 kati ya watoto 1000 wa shule waliobalehe wana ugonjwa huu.

Waziri Ummy ametaja sababu nyingine ya magonjwa ya moyo kuwa ni ya kurithi au kuzaliwa nayo kwa asilimia 0.35, ikimaanisha kuwa kuna takribani watoto 5000 wanaozaliwa na magonjwa ya moyo ya kurithi na karibu asilimia 50 wanahitaji upasuaji ili kurekebisha kasoro zilizopo katika mioyo yao kwa mwaka.

Hata hivyo, Waziri Ummy ameishukuru Serikali ya China katika kupunguza mzigo wa maradhi haya nchini kufuatia kuanzishwa kwa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete na sasa timu bora ya madaktari wa moyo kutoka jimbo la Shadong imekuja kutoa huduma katika kambi ya upasuaji na matibabu ya moyo inayoendelea katika taasisi hiyo.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya wa China Bw. Li Bin amesema Serikali ya China itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuimarisha huduma za sekta ya afya nchini ikiwa ni kuenzi ushirikiano ulioanzishwa na waasisi wa mataifa hayo. Serikali ya China imesaidia kujenga Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kupitia Rais wa zamani wa nchi hiyo Mh. Hu Jintao na jiwe la msingi liliwekwa mwezi Machi mwaka 2010 na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.

MWISHO

Alhamisi, 25 Julai 2019

SERIKALI YA CHINA NA TANZANIA KUENDELEZA USHIRIKIANO KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA.

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Afya kutoka China Mhe. Lin Bin wakiwa wameshikilia dawa ambazo hutengenezwa nchini China mapema leo wakiwa Ikwiriri-Rufiji Mkoani Pwani kuzindua Mradi wa Ushirikiano baina na China na Tanzania katika Kupambana na Ugonjwa wa Malaria Wilayani Rufiji.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) akiangalia kinga za ugonjwa wa malaria pamoja na Naibu Waziri wa Afya kutoka China Mhe. Lin Bin leo Ikwiriri-Rufiji Mkoa wa Pwani kabla ya uzinduzi wa mradi wa  ushirikiano wa pamoja kati ya China na Tanzania kupambana na ugonjwa wa malaria Wilayani Rufiji.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akipima ugonjwa wa Malaria leo Ikwiriir Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani alipoenda kuzindua Mradi wa Ushirikiano wa pamoja baina ya Tanzania na China wa kupambana na ugonjwa wa malaria Wilayani Rufiji

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) pamoja na Naibu Waziri wa Afya China wakisalimia mtoto katika Kituo cha Afya Ikwiriri- Rufiji Mkoa wa Pwani leo kabla ya kuzindua Mradi wa Ushirikiano baina ya Tanzania na China wa kupambana na ugonjwa wa malaria Wilayani Rufiji.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akipokea hundi kutoka Taasisi ya Fosun Pharma ya china kwa ajili ya dawa za malaria katika Wilaya ya Rufiji.
Picha ya pamoja Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wa kati kati mstari wa chini)  akiwa na Naibu Waziri wa Afya China Mhe. Lin Bin aliyeongozana na wataalam wake kutoka China pamoja na wataalam na wadau wa  sekta ya afya nchini


Na WAMJW - Rufiji, Pwani.

Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imeahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya Malaria ili kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi salama isiyo ya maambukizi ya Ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya kutoka Uchina Mhe. Lin Bin alipotembelea Ikwiriri, Rufiji Mkoa wa Pwani katika mradi wa ushirikiano wa pamoja baina ya China na Tanzania katika kudhibiti ugonjwa wa malaria huku akiongozana na mwenyeji wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu.

“China kuwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kimatafa tutaendelea kushirikiana kwa pamoja katika kusaidia Tanzania inafikia malengo ya kutokomeza ugonjwa wa malaria” amesema Mhe. Lin Bin na kuendelea kusema Ugonjwa wa malaria unatibika na kuzuilika

Waziri Lin Bin amesema kuwa ushirikiano baina ya Tanzania na China umeleta manufaa katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria kwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo Wilayani Rufiji kutoka asilimia 25 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 4.9 mwaka 2019.

“Kwa muda wa miaka 60 tumekuwa tukipambana dhidi ya ugonjwa wa malaria ambao umeathiri zaidi ya watu milioni 30, na tangia mwaka 2017 hakuna taarifa zilizolipotiwa kuhusu ugonjwa wa malaria nchini China” amesema Mhe. Lin Bin huku akiipongeza Tanzania kwa mikakati mizuri yenye lengo la kuhakikisha inatokomeza ugonjwa wa malaria.

Kwa upande wake Waziri wa Afya Tanzania, Mhe. Ummy Mwalimu ameishuruku Serikali ya China inayoongozwa na Rais Xi Jinping kwa kuendeleza ushirikiano wa enzi uliopo wa baina ya nchi hizo.

Waziri Ummy amesema kuwa ugonjwa wa malaria bado ni tatizo kubwa sana nchini Tanzania, huku takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zikionyesha kuwa asilimia 55 ya vifo vitokanavyo na malaria vinatoka katika nchini saba za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania.

“Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli tumechukua hatu ambali mbali kwa kushirikiana na wadau wakiwemo China kupambana na malaria na yapo mafanikio makubwa ambayo tumeyapata” Amesema Waziri Ummy Mwalimu na kuendelea “Tumeweza kupunguza kiwango cha maambukizi ya malaria kutoka asilimia 14.7 mwaka 2015 hadi 7.3 mwaka 2018”

Amesema kuwa wagonjwa wapya wa malaria wamepungua kwa asilimia 26 kutoka watu 161 katika kila watu 1000 mwaka 2014 hadi kufikia 119 katika kila watu 1000 mwaka 2018 huku vifo vitokanavyo na malaria vimepungua kwa asilimia 55, kutoka vifo 20 katika watu 1000 mwaka 2014 hadi kufikia vifo 9 kati ya watu 1000 mwaka 2018.

“Serikali ya Tanzania itaendela kuchukua hatua kwa kushirikiana na wadau wetu wakiwemo Serikali ya China kuhakikisha tunapunguza kiwango cha maambukizi ya maralia hadi kufikia asilimia 1 ifikapo mwaka 2020” alisema Waziri Ummy Mwalimu.

MWISHO.

Jumatano, 24 Julai 2019

BALOZI WA UFARANSA AFURAHISHWA NA HUDUMA ZA CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI MUHIMBILI

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Mikrobiolojia na Immunolojia chuo cha  MUHAS Prof. Said Aboud, wakati alipofanya ziara katika chuo hicho ili kujionea maendeleo ya shughuli zakitafiti katika chuo hicho, Kulia kwa Waziri Ummy ni Balozi wa Ufaransa Tanzania Frederic Clavier na wamwisho ni  Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Andrea Pembe.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akiambatana na Balozi wa Ufaransa Tanzania Frederic Clavier na Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Andrea Pembe, wakwanza  kushoto ni Mtaalamu wa Mikrobiolojia na Immunolojia chuo cha  MUHAS Prof. Said Aboud.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akipokea maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Mikrobiolojia na Immunolojia chuo cha  MUHAS wwakati alipofanya ziara katika chuo hicho ili kujionea Maendeleo ya shughuli zakitafiti katika chuo hicho, Kulia kwake ni Balozi wa Ufaransa Tanzania Frederic Clavier.

Wataalamu mbali mbali wa masuala ya tafiti pamoja na Watumishi wa Sekta ya Afya, wakifuatilia hotuba kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara katika chuo cha MUHAS ili kujionea Maendeleo ya shughuli zakitafiti

Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu pamoja na Balozi wa Ufaransa Tanzania Frederic Clavier na Wataalamu mbali mbali wa masuala ya tafiti pamoja na Watumishi wa Sekta ya Afya baada ya ziara ya kujionea Maendeleo ya shughuli zakitafiti katika chuo cha MUHAS.


BALOZI WA UFARANSA AFURAHISHWA NA HUDUMA ZA CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI MUHIMBILI

NA WAJMW-DSM

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Bw. Frederic Clavier amefurahishwa na huduma zinazotolewa katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu mapema leo wakati wa kukagua na kufuatilia maendeleo ya ushirikiano kati ya nchi ya Ufaransa na Tanzania katika masuala ya utafiti mafunzo na utoaji wa huduma za Afya katika chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili.

Kwa kiasi kikubwa Waziri Ummy pamoja na Balozi huyo wameridhishwa kwa kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Wataalamu katika chuo hicho ikiwemo utafiti, mafunzo na utoaji wa huduma za afya.

“Binafsi tumeridhishwa na kazi kubwa na nzuri zinazofanywa na wataalamu wetu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili, katika masuala ya utafiti tumeona kazi kubwa inayofanyika katika utafiti juu ya dawa za kuua wadudu”. Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema hakuna sheria nzuri za udhibiti wa dawa hizi nchini hivyo Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Muhimbili na Serikali ya Ufaransa itaendelea kufanya utafiti na kuona jinsi gani itapunguza madhara ya utumiaji wa dawa za kuua wadudu kwa binadamu.

Pamoja na hayo, Waziri Ummy amefurahi kuona ushirikiano ambao Serikali ya Ufaransa inaendelea kuutoa katika huduma za watu wenye tatizo la Seli nundu “Sickle Cell".

“kwa Mujibu wa Tafiti tuna jumla ya watu 200,000 nchini ambao wana tatizo la seli nundu na watoto ambao wanazaliwa ni 11,000 kwahiyo tumejadiliana na Serikali ya Ufaransa kuona ni jinsi gani tunaweza kuboresha huduma za ugunduzi ili tuweze kuwatambua mapema watoto pale wanapozaliwa na tatizo hili na kuhakikisha huduma za matibabu zinapatikana ikiwepo dawa ya kupunguza maumivu inapatikana”. Amesema Waziri Ummy.

Kufuatia hatua hiyo Waziri Ummy amemuomba Balozi Frederic kushawishi makampuni makubwa ya  kutengeneza dawa kutoka Ufaransa yaweze kusaidia katika kuzalisha dawa ya kupunguza maumivu ya Seli nundu inapatikana kwa Watanzania wengi.

Mwisho

Jumatano, 17 Julai 2019

WAZIRI UMMY ATOA MIEZI 3 KUKAMILISHA MRADI WA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA GEITA.

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wakatikati) akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel (Kulia kwa Waziri  Ummy) wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita,

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wapili kushoto) akipokea maelezo ya ujenzi kutoka kwa Mhandisi  kutoka Wizara ya Afya Eng. Mbuya (wakwanza kushoto) wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (watatu kushoto) akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel (wakwanza kushoto) pamoja na Mhandisi kutoka TBA (wapili kushoto) wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita,


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (aliyevaa kitambaa) akitoa maelekezo kwa Mhandisi  kutoka Wizara ya Afya Eng. MBuya wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita, Wakwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel

Baadhi ya miradi ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita yenye thamani ya shilingi Bilion 2.5 inayotarajia kumalizika ndani ya miezi mitatu


WAZIRI UMMY ATOA MIEZI 3 KUKAMILISHA MRADI WA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA GEITA. 

Na WAMJW- GEITA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amefanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi ya ujenzi wa Hospitali za Rufaa za mikoa nchini. 

Katika ziara hiyo Waziri Ummy amemwagiza Mkandarasi kutoka TBA Mkoa wa Geita kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha ndani ya miezi mitatu mradi huo unaisha ili huduma za Afya zianze kutolewa ifikapo Disemba 1, 2019.

"Nimemtaka Mkandarasi afanye kazi usiku na mchana ikiwezekana tukamilishe ujenzi huu hata mwezi wa kumi mwishoni, lengo langu nataka tarehe 1 mwezi Disemba 2019, tunaanza kutoa huduma hapa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita" alisema Waziri Ummy. 

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa Serikali imetoa kiasi cha shilingi Bilion 2.5 ili kukamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa Hospitali hiyo, ambayo itajenga jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la Maabara, jengo la upasuaji pamoja na jengo la mionzi.

Hata hivyo, Waziri Ummy amesema kuwa licha ya kuwepo changamoto ya upungufu wa Watumishi katika Sekta ya Afya, Wizara ya Afya imepata kibali cha kuajiri Watumishi wengine kutoka Wizara ya Utumishi jambo litalosaidia kupunguza Uhaba wa Watumishi katika Sekta ya Afya. 

Waziri Ummy aliendelea, kwa kuwataka Wakurugenzi kujiongeza ili kupambana na uhaba wa Watumishi katika ngazi ya Mkoa, ikiwemo kuajiri baadhi ya Watumishi kupitia mapato ya ndani ili kupunguza changamoto ya uhaba wa Watumishi, huku akitoa Wito kwa vijana waliomaliza vyuo kujitolea katika Hospitali ili kuongeza uzoefu zaidi. 

Mbali na hayo, Waziri Ummy amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kuendelea kujali Afya za Watanzania kwa kuboresha Sekta ya Afya ikiwemo kuboresha miundombinu ya Hospitali na kuhakikisha Dawa, vifaa na vifaa tiba vinapatikana.

Nae, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amemuomba Waziri Ummy kuanza kwa awamu ya pili ya ujenzi wa Hospitali hiyo ili kupata wodi ambazo zitatumika kulaza wagonjwa wataofika kupata huduma za Afya. 

"Uwepo wa wodi ndio utatoa taswira ya kuwa Hospitali hii kuwa ni Hospitali ya Mkoa, ili mtu akipata Rufaa aweze kulazwa na kuchukuliwa vipimo" alisema Mkuu wa Mkoa Mhandisi Robert Gabriel.

#tunaboreshaafya 

Mwisho.