Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 30 Desemba 2020

ONGEZENI KASI KATIKA HUDUMA ZA MAABARA - DKT. MHAME

 Mwakilishi wa Katibu Mkuu,Wizara ya Afya na Mkurugenzi Msaidizi wa Tiba Asili/Mbadala Dkt. Paul Mhame akifungua kikao kazi cha usambazaji wa miongozo inayosimamia huduma za tiba kwa Waganga Wakuu wa Mikoa,Wataalamu wa Maabara ngazi ya Mikoa na...

Jumatano, 23 Desemba 2020

WAFAMASI WAKUMBUSHWA KUHUISHA LESENI ZAO KABLA MWAKA KUISHA

 Msajili wa Baraza la Famasi Bi. Elizabeth Shekalaghe akisisitiza jambo wakati akiongea na afisa habari wa Wizara ya Afya,ofisini kwake jijini Dodoma.   WAFAMASI WAKUMBUSHWA KUHUISHA LESENI ZAO KABLA MWAKA KUISHANa. Catherine Sungura,WAMJW-DodomaWafamasia, fundi dawa sanifu na wasaidizi...

Jumamosi, 19 Desemba 2020

SERIKALI KUJA NA MFUMO WA TEHAMA WA UFUATILIAJI DAWA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha kujadili hali ya utoaji huduma za afya nchini ambacho kimewakutanisha Wakurugenzi wa Wizara pamoja na Taasisi zake kilichofanyika...

Ijumaa, 18 Desemba 2020

SERIKALI KUBORESHA MAENEO YA KUTUPA TAKA:DKT. SUBI

 Mkurugenzi wa huduma za kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi akitoa maelekezo  kwa Maafisa Afya mazingira (hawapo kwenye picha) katika kilele cha wiki ya usafi wa mazingira kitaifa...

Alhamisi, 17 Desemba 2020

WATAALAM WA TIBA ASILI WATAKIWA KUFANYA UTAFITI WENYE USHAHIDI

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bw. Edward Mbanga akiongea na wataalam wa tiba asili/mbadala kutoka taasisi za serikali na vyuo vikuu mbalimbali vinavyojishughulisha na tafiti za dawa za tiba asili nchini. Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt.Eliud...

Jumatano, 16 Desemba 2020

TIMIZENI WAJIBU WENU KWA WELEDI NA MAADILI.

 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Prof. Mabula Mchembe akifungua Mkutano wa Maafisa Afya mazingira uliofanyika Jijini Dodoma. Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, ambae pia ni Mkurugenzi wa huduma za Kinga Wizara...

TANZANIA YAVUKA VIWANGO VYA KIMATAIFA VYA UTOAJI WA CHANJO

Prof. Mabula Mchembe, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na WatotoDkt. Leonard SubiMkurugenzi wa Huduma za KingaWizara ya Afya Na. Catherine Sungura,WAMJW-DodomaKatibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendheleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Prof. Mabula Mchembe...

Alhamisi, 10 Desemba 2020

DKT. GWAJIMA AWATAKA VIONGOZI WA WIZARA YA AFYA KUSHIRIKIANA ILI KUONGEZA UFANISI KAZINI

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima akifurahia jambo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel baada ya kuwasiri katika ofisi za Wizara...

Jumatatu, 7 Desemba 2020

"WATUMISHI WA AFYA MSHIKIRI KATIKA KUCHANGIA MAENDELEO YA SEKTA YA AFYA" - MGANGA MKUU WA SERIKALI

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi

 


Na WAMJW – Mwanza.

 Mganga mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi amewata watumishi wa afya kushiriki kikamilifu katika kuchangia Maendeleo ya sekta ya afya na si kuiachia Serikali na Jamii pekee.

 

Amesema hayo akiwa kwenye kikao kazi na timu ya uongozi wa afya ndani ya Mkoa wa Mwanza kilichofanyika Wilayani Misungwi kujadali mikakati ya uboreshaji wa huduma za afya mkoani humo.

 

“Kwanini tushindwe kuchangia uboreshaji wa huduma za afya, lazima tuwe na moyo wa kujitoa kuchangia, hizi ni mali zetu sote sisi pamoja na watoto wetu sote tutatibiwa huko” Ni lazima sasa Hospitali zetu zianze kuwa na jicho la kutoa huduma huku zilijenga uwezo wa kifedha na kupunguza utegemezi toka serikali, bila kuathiri huduma kwa wananchi wasio na uwezo wa kulipia.. amesema Prof. Makubi.

 

Amesema hatuwezi kuitegemea Serikali na wafadhili pekee kutuletea Maendeleo ya huduma za afya katika maeneo yetu hivyo na watumishi wanapaswa kushiriki katika kuboresha huduma hizo katika maeneo waliyopo.

 

Aidha Prof. Abel Makubi alitumia nafasi hiyo pia kuendesha shughuli ya michango kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za afya ndani ya Mkoa huo ambapo juma ya Tsh 6,850,000/= fedha ambayo itaenda kutumika katika ujenzi wa jengo kwa ajili ya huduma kwa watoto waliolazwa mahututi (NICU)

 

Prof. Makubi amesema kuwa Mkoa wa Mwanza una uhitaji mkubwa wa huduma hiyo hivyo ufinyu wa eneo katika Hospitali ya Bugando unasababisha watoto walio wagonjwa kukosa huduma kwa wakati.

 

“Hospitali ya Budango inaendelea kupata wingi wa watoto ambao hawajafikia umri wa kuzaliwa na wengi wakiletwa bugando kunakuwa na shida ya kupata eneo la kuwahudumia, kwa michango hiyo itasaidia kuboresha huduma hizo kwa kuongeza eneo” amesema Prof. Makubi

 

Hata hivyo Prof. Makubi amesisitiza suala la uongozi imara kwa viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia taasisi za afya na kuwasisitiza  kuwajibika ipasavyo katika utumishi wao kwa kuhakikisha watumishi walio chini yao wanatoa huduma bora kwa wananchi.

 

Mwisho

HOSPITALI ZENYE WATAALAM BINGWA ZATAKIWA KUTOA HUDUMA ZA MKOBA KWA WANANCHI WALIO MBALI NA HUDUMA

 Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Makubi akisema jambo kwenye kikao na kamati tendaji ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya BugandoDkt. Caroline Damian Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Tiba anayesimamia Hospitali za Rufaa za Mikoa akisema jambo kwenye...

Ijumaa, 4 Desemba 2020

“VITA YA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA INAHITAJI JUHUZI ZA KILA MMOJA WETU” – MGANGA MKUU WA SERIKALI

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi akisema jambo kwa viongozi wa Mkoa wa Geita katika kikao cha kujadili miundombinu ya Sekta ya AfyaMkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Robert Gabriel akisema jambo kwenye kikao cha mkoa...

Page 1 of 102123»